Msanii wa Filamu za kibongo Elizabeth Michael alias Lulu baada ya
kipindi cha nyuma kurudishwa rumande kwa kesi yake inayomkabili kwa
kutuhumiwa kumuua msanii mwenzake,The Late Steven Kanumba,sasa taarifa
ambayo tumeipata ni kwamba wanasheria wake ambao ni Peter kibatala na
Kennedy Fungamtama na Fulgence Massawe wametuma maombi ya dhamana ya
kesi ya Lulu ili isomwe haraka kwasababu muombaji amekaa muda mrefu
mahabusu.
Wanasheria hao baada ya kuwasilisha maombi hayo katika mahakama Kuu wanatarajia kesi hiyo kusikilzwa tena siku ya tarehe 25 mwazi huu mbele ya Jaji Zainabu Mruke.
No comments:
Post a Comment