Actress mwenye makeke mengi na vituko vya kila aina Irine Uwoya amesema
kuwa safari yake aliyoifanya nchini Uingereza mwishoni mwa mwaka jana
bado haijazaa matunda ingawa bado wapo katika mazungumzo na wahusika,
ila kwa sasa kitu wanachokizungumzia ni namna watakavyoandika story
ingawa hakuweka wazi ni story ya namna gani wakati mtandao wa Dartalk
ulipomuuliza.Uwoya amesema kuwa watu hao wameonyesha nia ya kufanya nae
kazi ingawa malipo ya mzigo huo bado hayajawekwa wazi na lini watafanya
hiyo kazi rasmi. uwoya pia alikataa kuwataja hao watu anaotaka kufanya
nao kazi ingwawa baadhi ya mitandao na magazeti mwishoni mwa mwaka jana
yalimtaja muigizaji wa Hollywood Hale Berry kuwa anaweza piga mzigo na
muigizaji huyu wa swahiliwood. Uwoya alisema "Bado tunaendelea na
mazungumzo najua watu wanasubiri kuona ukweli juu ya maneno yangu haya
lakini ninachotaka kusema ni kwamba nilienda kwa ajili ya mazungumzo ila
bado mambo hayajakaa sawa". Tunamtakia kila la kheri muigizaji wetu
huyu katika safari yake ya kuanza kufanya kazi na watu nje ya nchi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment