Mahakama
Kuu Kanda ya Dar es Salaam imesogeza mbele tarehe ya kusikiliza maombi
ya dhamana ya msanii wa fani ya maigizo, Elizabeth Michael maarufu Lulu
ambaye anakabiliwa na kesi ya kuua bila kukusudia.
Jopo la mawakili wa lulu ambao wanaongozwa na Wakili Kennedy Fungamtama, Makamu wa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Peter Kibatala na Fulgence Masawe wa Kituo cha Msaada wa Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), waliwaslisha maombi hayo jana kwa mahakama hiyo.

Awali maombi hayo yalikuwa yamepangwa kusikilizwa LEO na Jaji Zainabu Mruke, lakini yamepelekwa mbele mpaka Jumatatu, Januari 28, 2013.
Taarifa ya Mahakama ya kusogeza mbele usikilizwaji wa maombi hayo, kwenda kwa mawakili wa pande zote haikueleza sababu ya kufanya hivyo.
Msanii huyo anakabiliwa na mashtaka ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa msanii maarufu wa fani hiyo nchini, Steven Kanumba.
Kesi hiyo ilifunguliwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu huku Lulu akikabiliwa na shtaka la mauaji ya kukusudia kinyume cha kifungu cha 196.
Katika hatua nyingine za kisheria baada ya kukamilika kwa upelelezi, Desemba 21, 2012, Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) alimbadilishia mashtaka na kuwa ya kuua bila kukusudia.
No comments:
Post a Comment