Saturday, January 26, 2013

HAYA NI MAGAZETI 16 YA LEO JAN 26, SOMA KURASA ZA MWANZO NA ZA MWISHO… PIA PICHA ZA VURUGU MTWARA! MOJA YA STORI KUBWA

































MWARICK JAPHET MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

Friday, January 25, 2013

Dhamana ya Lulu yapigwa kalenda


Elizabeth Michael maarufu Lulu

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imesogeza mbele tarehe ya kusikiliza maombi ya dhamana ya msanii wa fani ya maigizo, Elizabeth Michael maarufu Lulu ambaye anakabiliwa na kesi ya kuua bila kukusudia.

Jopo la mawakili wa lulu ambao wanaongozwa na Wakili Kennedy Fungamtama, Makamu wa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Peter Kibatala na Fulgence Masawe wa Kituo cha Msaada wa Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), waliwaslisha maombi hayo jana kwa mahakama hiyo.

Awali maombi hayo yalikuwa yamepangwa kusikilizwa LEO na Jaji Zainabu Mruke, lakini yamepelekwa mbele mpaka Jumatatu, Januari 28, 2013.

Taarifa ya Mahakama ya kusogeza mbele usikilizwaji wa maombi hayo, kwenda kwa mawakili wa pande zote haikueleza sababu ya kufanya hivyo. 

Msanii huyo anakabiliwa na mashtaka ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa msanii maarufu wa fani hiyo nchini, Steven Kanumba.

Kesi hiyo ilifunguliwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu huku Lulu  akikabiliwa na shtaka la mauaji ya kukusudia kinyume cha kifungu cha 196.

Katika hatua nyingine za kisheria baada ya kukamilika kwa upelelezi,  Desemba 21, 2012, Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) alimbadilishia mashtaka na kuwa ya kuua bila kukusudia.
MWARICK JAPHET MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

Tuesday, January 22, 2013

KESI YA LULU:WANASHERIA KUOMBA DHAMANA



Msanii wa Filamu za kibongo Elizabeth Michael alias Lulu baada ya kipindi cha nyuma kurudishwa rumande kwa kesi yake inayomkabili kwa kutuhumiwa kumuua msanii mwenzake,The Late  Steven Kanumba,sasa taarifa ambayo tumeipata ni kwamba wanasheria wake ambao ni Peter kibatala na Kennedy Fungamtama na Fulgence Massawe wametuma maombi ya dhamana ya kesi ya Lulu ili isomwe haraka kwasababu muombaji amekaa muda mrefu mahabusu.

Wanasheria hao baada ya kuwasilisha maombi hayo katika mahakama Kuu wanatarajia kesi hiyo kusikilzwa tena siku ya tarehe 25 mwazi huu mbele ya Jaji Zainabu Mruke.
MWARICK JAPHET MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

SAFARI YA IRINE UWOYA NCHINI UINGEREZA YASHINDWA KUZAA MATUNDA


Actress mwenye makeke mengi na vituko vya kila aina Irine Uwoya amesema kuwa safari yake aliyoifanya nchini Uingereza mwishoni mwa mwaka jana bado haijazaa matunda ingawa bado wapo katika mazungumzo na wahusika, ila kwa sasa kitu wanachokizungumzia ni namna watakavyoandika story ingawa hakuweka wazi ni story ya namna gani wakati mtandao wa Dartalk ulipomuuliza.Uwoya amesema kuwa watu hao wameonyesha nia ya kufanya nae kazi ingawa malipo ya mzigo huo bado hayajawekwa wazi na lini watafanya hiyo kazi rasmi. uwoya pia alikataa kuwataja hao watu anaotaka kufanya nao kazi ingwawa baadhi ya mitandao na magazeti mwishoni mwa mwaka jana yalimtaja muigizaji wa Hollywood Hale Berry kuwa anaweza piga mzigo na muigizaji huyu wa swahiliwood. Uwoya alisema "Bado tunaendelea na mazungumzo najua watu wanasubiri kuona ukweli juu ya maneno yangu haya lakini ninachotaka kusema ni kwamba nilienda kwa ajili ya mazungumzo ila bado mambo hayajakaa sawa". Tunamtakia kila la kheri muigizaji wetu huyu katika safari yake ya kuanza kufanya kazi na watu nje ya nchi.
MWARICK JAPHET MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

Monday, January 21, 2013

FLORA MVUNGI: NI LAZIMA SHILOLE AJE KUNIPIGIA MAGOTI LA SIVYO.....


 
Muigizaji maarufu Swahiliwood Flora Mvungi amesema kuwa bifu lake na muigizaji mwenzake Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole haliwezi kuisha hivi hivi kama shilole hatamuomba msamaha na kwenda kukiri kwenye magazeti kwa alichokisema ambacho kilionekana kumkera sana Flora.Swahiliworldplanet lilimtafuta Flora na kumuuliza kama yeye na Shilole wakipatanishwa wanaweza kuondoa tofauti zao na kuwa mashostito walioshibana kama mwanzo, Flora alijibu "Mi sina tatizo but ili mambo yawe sawa ni lazima aniombe msamaha mimi na H.baba kwenye hayo hayo magazeti ambayo alienda kuongea upuuzi la sivyo hayawezi kuisha na sitaki kusuluhishwa kimya kimya, waandishi waitwe akiri alichofanya mambo yawe wazi na baada ya hapo yatakuwa yameisha". Shilole na Flora walikuwa mabest wakubwa huko nyuma lakini wakaja kuwa chui na paka, shilole anadaiwa kumponda Mvungi pamoja na mwandani wake H.Baba kuwa Flora hana maendeleo yoyote tangu aanze uhusiano wake na H.Baba amekuwa anamsikiliza sana huyo H.Baba kama mungu mtu kiasi cha kushindwa kujijengea maisha yake yeye mwenyewe kwasababu anamtegemea na kumsikiliza kwa kila kitu.kwa upande mwingine mastaa hawa wa filamu waliiingia kwenye mtifuano mkali baada ya Flora kudaiwa yeye ndiye alimpokea Shilole na kuishi wote nyumbani kwake miaka kadhaa nyuma wakati shilole anatoka kwao kuja mjini kutafuta maisha lakini Shilole amemgeuzia kibao Flora kuwa asijitape yeye ndio alimpokea Flora mjini na kuishi nae nyumbani kwake.Pia hivi karibuni Flora alikaririwa na gazeti moja akisema "Shilole ananuka wanaume". Hatukufanikiwa kumpata shilole ili kumuuliza kama yupo tayari kuyamaliza wakipatanishwa lakini bado tunamsaka atoe yaliyo moyoni mwake....


MWARICK JAPHET MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

Friday, January 18, 2013

M.D.I. JUU YA MCHAKATO WA KUSOMESHA WANAFUNZI WENYE MAZINGIRA MAGUMU


KAMATI YA M.D.I IMEFIKA LEO KATIKA SHULE YA SECONDARI MAGU NA KUKUTANA NA BAADHI YA MWANAFUNZI HAO.

ANGARIA PICHA ZA MLENZI WA VIJANA PAMOJA NA KAMATI YA M.D.I. WALIPOKUA MAGU SECONDARY.

MLEZI WA VIJANA  MWL. BISECO

KAMATI IKIWA NA MLEZI

Dr, FRANK MGANGA





 KAMATI IKIONGEA NA MWANAFUNZI
 SELEMAN JAPHET


KAMATI NA MLEZI
MWARICK JAPHET MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

Thursday, January 17, 2013

BAADHI YA PICHA ZA MANGULA ALIVYOTUA WILAYANI MAGU.









































MWARICK JAPHET MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.