Picha
Juu na Chini ni Baadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa Uvccm
mkoani Arusha kutoka wilayani Monduli wakiingia kwa mara ya pili kupiga
kura za kumchagua mwenyekiti wa umoja huo baada ya zoezi la awali
kuvurugika katika ukumbi wa CCM mkoa.(picha na Mahmoud Ahmad-Arusha).
Mahmoud Ahmad Arusha
Hali
ya tafrani imeibuka katika uchaguzi wa jumuiya ya umoja wa vijana wa
Chama Cha Mapinduzi(Uvccm) mkoa wa Arusha baada ya katibu wa CCM mkoani
hapa,Mary Chatanda kunusurika kipigo baada ya kutuhumiwa kuvuruga
uchaguzi huo kwa lengo la kumpitisha chaguo lake ambaye alitajwa kuwa
ni ,Dk Harold Adamson.
Katika
vurugu hizo Chatanda alinusurika kipigo kutoka kwa wajumbe waliotoka
wilayani ya Monduli baada ya kuamuru zoezi la uchaguzi huo lilirudiwe
kwa madai kwamba wajumbe hao pamoja na wale wanaotoka wilayani Meru
idadi yao ilikuwa na kasoro.
Katika
vurugu hizo makundi ya baadhi ya vigogo wa CCM hapa nchini
yanyohusihswa na waziri mkuu mstaafu aliyejiuzulu,Edward Lowasa pamoja
na Bernad Membe yalijidhihirisha waziwazi ambapo yalikuwa yakitambiana
nje ya ukumbi wa mkutano.
Hatahivyo,katika
hali isiyo ya kawaida polisi pamoja na maofisa wa usalama wa taifa
waliwatimua waandishi wa habari waliokuwa nje ya ukumbi wa mkutano
katika jengo la CCM mkoani hapa kwa amri ya katibu wa CCM wilaya kwa
madai kwamba hawana mashati yenmye rangi ya kijani.
Zoezi
la kupiga kura za uchaguzi wa nafasi ya mwenyekiti wa Uvccm mkoa
lilianza majira ya saa 6;00 mchana ambapo upepo wa awali katika uchaguzi
huo ulionyesha kwenda kwa mgombea,Robinson Meitenyiku anayetokea
wilayani Arusha.
Vurugu
hizo zilianza majira ya saa 9;00 mchana ambapo Chatanda alipoamuru
wajumbe wa mkutano huo watoke nje ya ukumbi kwa madai kwamba kuna baadhi
yao kutoka wilaya za Meru na Monduli walizidi.
Akitangaza
uamuzi huo katibu huyo alisema kwamba wajumbe kutoka wilayani Monduli
idadi yao haikuwa halali pamoja na ile ya wilayani Meru kwamba wajumbe
watano walizidi kitendo kilichopingwa vikali.
Hatahivyo,mara
baada ya wajumbe hao kutoka nje ya ukumbi wa uchaguzi walianza kupaza
sauti kwamba katibu huyo analengo la kuvuruga uchaguzi huo kwa kuwa
anataka kumpitisha mgombea wa nafasi hiyo,Dk Adamson.
Wakati
vurugu hizo zikiendelea ndipo baadhi ya wajumbe kutoka wilayani Monduli
walitishia kumchapa ndani ya ukumbi huo lakini juhudi zao zilizimwa na
baadhi ya walinzi wakiwemo askari wa jeshi la polisi mkoani Arusha.
Mmoja
wa wajumbe hao kutoka wilayani Monduli,Isaac Kadogoo alimwakia vikali
Chatanda ndani ya ukumbi huo na kumtuhumu kwamba kitendo chake cha kukaa
karibu na sanduku la kura kilikuwa na lengo la kutaka kuchakachua kura
hizo.
“Mheshimiwa
katibu rudi ukae meza kuu hata kama wewe ni msimamizi wa uchaguzi huu
ondoka hapo kwenye sanduku la kura tuna wasiwasi na wewe”alisikika
Kadogoo
Wakati
hayo yakijiri nje ya ukumbi wa mkutano huo baadhi ya wajumbe walipinga
kitendo cha Chatanda kuwatoa nje na kusema kwamba ana lengo la kuuvuruga
uchaguzi huo ili chaguo lake lipite.
Hatahivyo,ilipotimu
majira ya saa 9;15 mchana ndipo wajumbe hao walitangaziwa kurudi ndani
ya ukumbi huo kwa lengo la kurudia zoezi la kupiga kura na ndipo
walipojipanga kwa mistari na kuelekea katika ukumbi wa uchaguzi kupiga
kura kwa mara nyingine.
Maofisa
wa usalama wa taifa sanjari na askari wa jeshi la polisi mkoani Arusha
walikuwa wakiranda randa nje na ndani ya ukumbi wa mkutano kuimarisha
ulinzi wakiwemo na baadhi ya maofisa wa Takukuru mkoani Arusha.
VIA: MO BLOG
No comments:
Post a Comment