Mkutano Mkuu 2012 wa watanzania waishio ujerumani Wafana kwa kishindo Frankfurt
"Umoja wa watanzania Ujerumani wapata Uongozi Mpya"
Mkutano
mkuu wa watanzania waishio ujerumani uliofanyika siku ya jumaamosi
tarehe 29. 09 2012 Mjini Frankfurt katika kitongoji cha Raunheim.
ulifanikiwa kutimiza malengo yake na maazimio yake Moja wapo ilikuwa ni
kufanya uchaguzi wa uongozi wa umoja huo,
kabla ya kufanyika uchaguzi
huo na mjadala wa maazimio ya umoja huo,
Mgeni rasmi katika mkutano huo
mwana diplomasia naibu balozi wa Tanzania
nchini ujerumani mheshimiwa Bw. Ali Siwa alitoa nasaha zake na salamu
kutoka Ubalozi wa Tanzania Nchini ujerumani kwa watanzania waliohudhuria
katika mkutano huo, kwanza aliwapongeza watanzania kwa kufanikiwa
kuunda umoja huo wa watanzania waishio
ujerumani ambao ndio mwamvuli mkuu wa mshikamano wa watanzania wote
nchini ujeruman, isitoshe Bw. Ali Siwa aliwaambia watanzania kwamba
ofisi yake ipo wazi wakati wowote iwapo umoja huo utahitaji ushauri
wowote utakaoleta maendeleo ya umoja huo na watanzania kwa ujumla,
aliwaasa watanzania kuwa mshikamano wao na umoja wao ndio utakaokuwa
ufunguo na sauti ya maendeleo yao na vizazi vwao ugenini na nyumbani
pia. baada ya nasaha hizo wananchama wa umoja wa watanzania walichagua
viongozi wao kama ifuatavyo:-
Mwenyekiti:
Mfundo Peter Mfundo, Makamo: M/Mwenyekiti. George Mtalemwa. Katibu: Bi
Tulalumba Mloge. Muweka hazina: Bi Mwamvua Dugala Merkel.
Umoja
huo wa Watanzania Ujerumani (UTU) ndio chombo pekee kilichopata usajili
kwenye serikali ya ujerumani, na kutambuliwa kisheria, ambacho
kinawaunganisha watanzania wote wanaoishi ujerumani, na ndio Daraja
linalowaunganisha watanzania waliopo Nyumbani na kwengineko ughaibuni.
Kwa watanzania wanaopenda kujiunga na umoja wa watanzania ujerumani
(UTU) milango ipo wazi, wasiliana na
No comments:
Post a Comment