Tuesday, October 30, 2012

13 WAFARIKI KUTOKANA NA KIMBUNGA SANDY



Mojawapo ya vimbunga vikubwa zaidi kuwahi kupiga Mashariki mwa Pwani ya Marekani kimesababisha mafuriko makubwa katika baadhi ya sehemu za mji wa New York.
Maeneo mengi mjini yamewachwa katika giza baada ya huduma za umeme kukatizwa.
Kimbunga hicho kilipiga ardhi kwenye Pwani ya New Jersey karibu na mji wa Atalanta muda mfupi jana usiku/Dhoruba kali kutoka mjini Florida hadi nchini Canada imepiga Mashariki mwa Marekani na kusababisha mawimbi makali mjini New York.
Maji yamefurika kwenye barabara na katika njia za reli pamoja, maeneo ya kuegesha magari na katika eneo la Ground Zero, eneo ambalo mashambulizi ya Septemba kumi na moja yalitokea.
Sehemu kubwa za mji wa New York ziko kwenye giza baada ya milingoti ya umeme kuharibiwa.
Wagonjwa waliondolewa kwenye hospitali moja baada ya umeme kukatika.
Zaidi ya watu milioni tano walisemekana kukosa umeme katika eneo la Pwani baada dhoruba kali huku takriban wengine milioni moja wakishauriwa kuhama nyumba zao. Athari za kimbunga hicho labda huenda zikajulikana baadaye leo.

VIA: bbc Swahili
MWARICK JAPHET MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

No comments:

Post a Comment