Ni kitambo sasa tangu kuwepo kwa taarifa kuwa staa wa Bongo Movie,
Juma Kilowoko, 'Sajuki' ni mgonjwa , huku pia taarifa za karibuni
zikidai kuwa hali ya nyota huyo bado ni tete na kuzua hofu kubwa kwa
mashabiki wake.
Kupitia mtandao huu pekee taarifa rasmi ni kuwa hali nyota huyo kwa
sasa ni njema na yuko tayari tena kuanza kuwatumikia watanzania
kupitia tasnia ya filamu.
Kwenye Exclusive interview aliyofanya na mtandao huu mapema leo Sajuki
amewashukuru watanzania kwa kuwa pamoja nae kwenye wakati wote wa
matatizo mpaka sasa anajisikia yuko vizuri tofauti na ilivyokuwa
awali.
Nashukuru kuwa sasa niko poa, watanzania waelewe hilo, kwa sasa
naweza hata kuendesha gari na karibuni nitaanza kucheza muvi tena
alisema Sajuki.
katika kuonyesha kuwa anathamini i mchango wa Watanzania Sajuki ameachia ngoma ambayo ameamua kuipa jina la Shukurani
VIA:suleimanmagoma.blogspot.com |
No comments:
Post a Comment