Sunday, August 5, 2012

KONGAMANO LA HAMASA YA KUFUFUA TIMU YA TUKUYU STAR LAFANA UWANJA WA TANDALE MJINI TUKUYU.


 

Mkuu wa wilaya ya Rungwe Mh. Crispin Meela akizungumza na Mashabiki, Wadau na Wananchi wa Rungwe wakati wa uzinduzi wa Kongamano la kuifufua timu ya Tukuyu Star kwenye uwanja wa Tandale mjini Tukuyu mkoani Mbeya leo, ambapo kulikuwa na michezo mbalimbali ya mpira wa miguu ikishereheswa na ngoma za asili ya watu wa Rungwe ya Ighoma iliyokuwa ikutumbuizwa katika viwanja hivyo, Bonanza lilivuta hisia za watu wengi na wadau wa mkoa wa mbeya na mikoa ya jirani hasa wachezaji waliowahi kuchezea timu ya Tukuyu Star miaka ya 1980 na 1986 huku umati wa watu ukishuhudia tukio hilo. Katika bonanza hilo timu ya Rungwe Veterani imefaikiwa kkuichapa timu ya wadau wa Tukuyu Star Family magolo 3-1, akielezea mpambano huo Kocha wa timu ya Tukuyu Star Family Kenny6 Mwaisabula amesema kushindwa ni sehemu ya mchezo, lakini pia wachezaji wa Rungwe Veterani wako fiti zaidi kimchezo kutokana na kwamba muda mwingi wanafanya mazoezi sana, lakini pia hali ya hewa inawaruhusu kwani wamezoea baridi tofauti na wachezaji wake, Usiku huu kuna kongamano linaendelea mjini Tukuyu ili kujadili mikakati mbalimbali na utaratibu utakaotumika katika kuiendesha Tukuyu Star mpya.


Makamu mwenyekiti wa Tukuyu Stars Family Bw. Peter Mwambuja akizungumza katika bonanza la michezo kwa ajili ya kuhamasisha wadau ili kufufua upya timu ya Tukuyu Star kwenye uwanja wa Tandale mjini Tukuyu leo

Kikosi kizima cha Tukuyu Star Family kikiwa katika picha ya pamoja kulia ni kocha Kenny Mwaisabula Mzazi na kushoto ni Makamu mwenyekiti Tukuyu star Family Peter Mwabuja.
Kikosi cha Tukuyu Star Family na Rungwe Veterani vikiwa katika picha ya pamoja na viongozi wao kabla ya kuanza kwa mchezo wao.
Kocha Koroso naye alikuwepo katika bonanza hilo , Koroso ni mmoja wa makocha waliofundisha mpira nchini Tanzania na nje ya nchi.
Dasi wa Wilaya ya Rungwe Mosess Mwidete akikagua kikosi cha timu ya Rungwe Veterani kabla ya mchezo kati yake na Tukuyu Star Family.
Kikosi cha Tukuyu Star Family kutoka jijini Dar es salaam kikiwa katika picha ya pamoja na kochwa wao pamoja na viongozi kadhaa wa timu hiyo mbele ya gari lao
Mosess Mwidete DAS wa Wilaya ya Rungwe akizungumza na wachezaji wa Tukuyu Star Family na Rungwe Veterani kabla ya mchezo wao kwenye uwanja wa Tandale mjini Tukuyu.
Kikosi cha timu ya Rungwe Veterani kikiwa katika picha ya pamoja kwenye uwanja wa Tandale mjini Tukuyu.
Wadau wa Tukuyu  Star Family  wakijadiliana jambo katika kongamano hilo huku wakishuhudia mpambano wao kati yao na Tukuyu Star Family.
Kocha Kenny Mwaisabula Mzazi akitoa maelekezo kwa wachezaji wake kushoto ni Moses Mkandawile na katikati ni Willy Martin “Gari kubwa”
Mashabiki mbalimbali wakiwa wamefurika kwenye uwanja wa Tandale ili kushuhudia Kongamano hilo.
Ngoma ya Asili ya kinyakyusa inayoitwa Ighoma ikitumbuizwa katika bonanza hilo kabla ya kuanza kwa michezo mbalimbali ya mpira wa miguu.
Timu ya U14 ya Ushirika mjini Tukuyu ikiwa katika picha ya pamoja
Timu ya U14  FOYSA kutoka jijini Mbeya kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kucheza mchezo wake na Ushirika
Mchezaji wa timu ya FOYSA akimiliki mpira mbele ya mchezaji wa timu ya Ushirika wakati timu za U14 zilipopambana katika bonanza hilo.
Ngoma ya asili ya Kinyakyusa ikitumuiza katika bonanza hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Mh. Crispin Meela wa pili kutoka kulia akizungumza mjambo na Mwenyekiti wa kamati ya Kufufua timu ya Tukuyu Star Kenny Mwaisabula, kulia ni Mosess Mwidete RAS wa Rungwe na kushoto ni Peter Mwambuja Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo.
Mashabiki na wadau wa Tukuyu Star wakishuhudia michezo mbalimbali katika bonanza hilo.

MATOKEO YA UALIMU NA UFUNDI - 2012


NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA

MATOKEO YA UALIMU NA UFUNDI - 2012

f

 

 

 

 

 

BOFYA HAPA KUANGALIA

UGANDA MULLS ITS OWN TAX LAW CITING SLOW PROGRESS IN EAC INTEGRATION.


Junior Finance Minister in charge of Planning, Matia Kasaija.

Uganda is mulling a review of the East African Excise Management Act that would allow it to claw back the right to collect taxes from institutions of the EAC and instead vest them with the Commissioner General of the Uganda Revenue Authority (URA).

In a signal Uganda was losing patience with the slow pace on implementation of a common tax regime, it has proposed amendments requiring the powers for tax refunds or rebate taken away from EAC customs officials and given to the Commissioner General of URA.

In the case of failure to pay tax and its interest, the word “Community” is being replaced with the Uganda government.

Under the East African Excise Management Act, a throwback to the first EAC that collapsed in 1977, Uganda’s Customs duty was collected at entry ports manned by its partners in Kenya and Tanzania. 

The law was replaced by the East African Customs Union Management Act (EAUMA) 2005, which provided for a single tax collection centre for the region, Uganda is concerned that seven years later, it is yet to come into force. 

Uganda is apparently also not satisfied with Kenya’s refusal to allow it to post its revenue officers at Mombasa. 

According to the Junior Finance Minister in charge of Planning, Matia Kasaija, while the process for common taxation is ongoing and there is a project to establish a common tax collection centre, progress has been hampered by a lack of trust.

“We failed to agree on who collects taxes for us; we cannot trust Kenya to collect because we don’t know how long it would take for them to remit our share of the taxes,” said Mr Kasaijja.
Mr Kasaijja said Uganda had wanted to place its own tax collectors at the common collecting point but this was rejected. He added that this problem can only be solved when we are one country, a sentiment that observers of the EAC integration agree with.

Lydia Wanyoto, a former member of the East African Legislative Assembly, said the common taxation regime has failed because countries view revenue as a sovereignty issue and no one is willing to give up this important aspect.

URA Commissioner General Allen Kagina said the new law will cater to internal taxes as the Customs Union deals with external taxes.

It is understood that Uganda is also finding it difficult to use fiscal policy to direct policy and giving up on some taxes that have been abolished under the Common Market.  For instance, while other EAC members allow contractors to re-export machinery without paying any taxes, Uganda levies taxes.

T.I.D feat. Mangwear - Kiuno {Official Video}

Saturday, August 4, 2012

MWANZA WATAHADHARISHWA JUU YA EBOLA


SERIKALI mkoani Mwanza, imewataka wananchi kuchukua tahadhali kuhusiana na tishio la ugonjwa wa Ebola ambao umeripotiwa kuuwa watu kadhaa nchi jirani ya Uganda. 


Tahadhali hiyo ilitolewa jana na Mkuu wa mkoa wa Mwanza,Mhandisi Evarist Ndikilo, alipozungumza waandishi wa habari kuhusuiana na ugonjwa huo. 

 Alisema serikali ya mkoa kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, imepanga mikakati ya kukabiliana na tishio la ugonjwa huo hatari unaouwa kwa haraka.


 “Ukiangalia jiji letu la Mwanza lina mwingiliano mkubwa kutokana na kuwa kitovu cha biashara kwa nchi za Maziwa Makuu, hivyo wananchi wanapaswa kuchukua tahadhali kwa kujikinga na kutoa taarifa pindi wanapomwona mtu mwenye dalili za ugonjwa huo,”alisema Ndikilo Alisema shirika la Afya Duniani (WHO) tayari limethibitisha kuwepo kwa ugonjwa wa Ebola nchini Uganda, katika Wilaya ya Kibule, Magharibi mwa nchi hiyo ambapo watu 26 wameriptiwa kuambukizwa na kati yao 14 wamefariki dunia kwa kuambukizwa ugonjwa huo tangu Julai 28, mwaka huu.


 Mhandisi Ndikilo, alieleza kuwa ugonjwa huo huambukiza kwa kugusana na mtu mwenye kuathiriwa na virusi vya Ebola ambavyo hutokana na sokwe pamoja na jamii ya wanyama aina hiyo, ambapo kwa mara ya kwanza ulibainika kuwapo 1976.


 Dalili za ugonjwa huo ni homa kali ya ghafla,vidonda vya koo, upele katika ngozi na kutokwa damu sehemu mbalimbali za mwili na katika kukabiliana na maambukizi Ebola, wataalamu wa wizara ya Afya ambao tayari wapo jijini hapa, watafanya ukaguzi kwa wageni waingiao nchni kupitia njia ya anga, majini na nchi kavu bila usumbufu.


 “Hatua za kuchukua ni kuongeza kasi ya ufuatiliaji, kufanya ukaguzi bila usumbufu kwa wageni wanaosafiri kwa ndege, meli na mabasi kuingia nchini, kutoa elimu kwa wananchi na watumishi wa afya na upatikanaji wa vifaa vya kinga;”alisema Alisema ili kuwalinda wananchi, vipeperushi na vijarida vinavyohusu ugonjwa huo wa Ebola vitasambazwa ili wananchi wapate ufahamu wa dalili zake lakini pia wawe tayari kutoa taarifa pndi wanapomhisi mtu mwenye dalili za gonjwa huo.


 “Pamoja na juhudi za serikali, kupitia vyombo vya habari eneo la mikoa ya Kanda ya Ziwa tuchukue tahadhali kuhakikisha wananchi wanafahamu tatizo hili kwa kusoma vipeperushi na kupashana habari,”alisema Mkuu huyo wa mkoa Tayari watu 14 wamefariki dunia katka wilaya ya Kibule Magharibi mwa nchi ya Uganda tangu kuzuka kwa ugonjwa huo Julai 28 mwaka huu.


Mwaka jana mtu mmoja aliliripotiwa kufa nchini humo kutokana na kuambukizwa virusi vya ugonjwa wa Ebola. Mbali na Uganda, miaka kadhaa iliyopita Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) iliwahi kukumbwa na ugonjwa huo na watu kadhaa kuripotiwa kufa. 
 
 
via:  http://gsengo.blogspot.com

Thursday, August 2, 2012

MSANII NA MTOTO WA MITAANI BALAJA ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUTUHUMIWA KUIBA


Leo hii, maeneo ya manyanya, mtoto wa mitaani ambae pia alishawahi kurekodi wimbo (maumivu) pamoja na video yake, chini ya msaada wa fish crab producer Lamar, amepigwa nusu ya kufa na wananchi baada ya kutuhumiwa kumuibia mtu asiyejulikana aliekuwa kituo cha basi, "watu wamempiga sana, alikua keshaanza kutoka damu mdomoni, mi nimefika pale ndio wakaacha kumpiga" amesema lamar ambae alikua eneo la tukio
Balaja anatokea kahama mkoani shinyanga, mara nyingi amekuwa akiomba nauli ya kurudi kwao ambapo anadai kuishi na bibi yake, lakini kila akidakiswa nauli, kesho unamkuta tena mitaani.

VIA:  http://djfetty.blogspot.com

APONGEZWA KWA KUSAIDIA KUKAMATWA KWA GARI ILIYOSABABISHA AJALI YA KIFO

Na. Luppy Kungalo wa Jeshi la Polisi Dodoma,

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma limempongeza kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la Ally Augustino umri wa Miaka (20) baada ya kufanya kitendo cha kijasiri kwa kudandia gari lililosababisha ajali na kukimbia, kisha kufanya mawasiliano na askari Polisi mkoani humo na kufanikisha kukamatwa kwa gari hiyo.

Akizungumzia Tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamisha Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Bw. ZELOTHE STEPEN alisema lilitokea majira ya saa mbili usiku jana katika kijiji cha Chilonwa Wilayani Chamwino na kusababisha kifo kwa mtembea kwa miguu aliyejulikana kwa jina Daniel Chilomboli, mgogo mwenye umri wa miaka (30)

“ Gari lilipomgonga mtembea kwa miguu huyo lilipunguza kasi kidogo  na kusimama lakini kwa kuwa watu walikuwa wakipiga mayowe na kukusanyika kwa wingi Dereva aliwasha gari na kuanza kuondoka ndipo Kijana huyo bila kuchelewa akalidandia kwa nyuma na kuanza kufanya mawasiliano na Askari kwa kutumia simu” alielezea Bw. Zelothe Stephen

Alilitaja gari lilosababisha ajali hiyo ya kumgonga mtembea kwa miguu  kuwa ni lenye usajili wa namba T.775 ATD  MITSUBISHI CANTER ambalo ubavuni lilonyesha kumilikiwa na Bw. NJIUKA E.R.M WA SANDUKU LA Posta 1018 Dodoma.

Kamanda ZELOTHE STEPEN alipongeza kitendo Cha kijasiri kilichofanywa na kijana huyo kwa kutambua na kutekeleza kwa vitendo  Mkakati wa Polisi Jamii na Ulinzi Shirikishi ambao Jeshi la Polisi linahitaji ushirikiano huo sana toka kwa Wananchi .

“Natoa wito kwa wananchi wote kuiga mfano wa kijana huyu katika maeneo yenu na kuwa na uchungu dhidi ya  watu wasiotaka kufuata sheria, taratibu na kanuni za usalama barabarani kwa kuwafuatilia na kuwatolea taarifa katika vituo vya Polisi ili sheria ichukue nafasi dhidi yao” alitoa wito Kamanda Zelothe.

Bw. Zelothe alisema juhudi za Kulifuatilia gari hilo huku kijana Ally Augustino akiwa amedandia gari hilo lilihusisha pia mawasilianao na Mtendaji wa kata wa eneo hilo la Chilonwa Bw. Emanuel Matewa ambaye alichukua hatua kupiga simu kwa walinzi  wanaokusanya ushuru wa magari akatika eneo hilo la Chilonwa ambao nao walidhibiti eneo lao lakini gari hiyo ilipita njia nyingine.

Aidha Kamanda ZELOTHE STEPEN alisema mawasilianao yaliendelea kufanyika baina ya Kijana huyo na Askari wa Wilaya ya  Chamwino na Dodoma mjini na kufanikiwa kulikamata baada ya Dereva kuonyeshwa alama ya kusimama na askari, na yeye kusimama kisha kufungua mlango na kukimbia kusikojulikana.

Mkuu huyo wa Polisi Mkoa wa Dodoma alisema gari hilo lilikamatwa maeneo ya Chaduru  katika barabara iendayo eneo la Ipagara katika Wilaya ya Dodoma Mjini  na kwamba Jeshi la Polisi linaendelea kumsaka Dereva wa Gari hilo ili kuweza kumfikisha mahakamani kujibu shitaka linalomkabili.

Bw. ZELOTHE amesema tayari maelekezo yameshatolewa kwa Mkuu wa Usalama Barabarani katika Wilaya ya Chamwino kupitia katika vikundi vya Ulinzi Shirikishi katika eneo hilo kwenda kumpongeza kijana huyo na kuwahamasisha wengine waige tabia hiyo ya kishujaa.

Kamanda ZELOTHE STEPEN alitoa Rai kwamba kitendo kilichofanywa na kijana huyo, kiwe chachu kwa   wananchi katika maeneo yao na  kufungua  ukurasa mpya wa ushirikiano wa hali na mali, na utakaowezesha kuunganisha nguvu kati ya Jamii na Polisi na Wadau wengine dhidi ya kero za uhalifu  katika maeneo yao.

UJUMBE WA MAKENE KUHUSIANA NA TUZO ZA BLOGGERZ ZILIZOTOLEWA NA VODACOM.


 
Hivi majuzi niliskia kuwepo kwa tuzo za waandishi wa habari za mtandaoni maarufu kama waandishi wa magazeti tando (blogs). Katika Tuzo hizo ambazo ziliandaliwa kwa vigezo wanavyovijua Vodacom, wametajwa washindi fulani. Kama mdau wa kawaida katika magazeti tando, miongoni mwa waasisi wa Bloger wa kwanza kabisa wa Kitanzania naamini kwa sasa kama nchi hii itakuwa inaendeshwa kishkaji, kirafiki, kima kundi na ikaachwa bila kukemewa basi siku si nyingi tutapoteza ladha ya mashindano yanayopima viwango na ubora wa kazi hali itakayofanya nchi kubakia kuwa ya wababaishaji kila siku.

Eneo hili la magazeti tando niliwahi kulilalamikia kutokana na kukosekana ubunifu hasa inapotokea habari moja inajaa kila blog kama ambavyo ipo katika magazeti ya Tanzania. Kwa kuona hili hili nashangaa blog iliyo na kazi ya kubandika picha za magazeti ya kila siku ama habari za wasanii walio nje au kuchota mawazo ya watu katika FB na twitter, au kusubiri taarifa za Maafisa Habari ikaibuka mshindi kwa kuwa tu eti inaonesha kuwa na wasomaji wengi. Kwamba hamjui kuwa ukiseti weblog yako ihesabu wanaoitembelea itahesabu bila kujali ni nani anaingia mara ngapi?

Kwa mantiki hii kigezo cha idadi ya watu si muwli kuonesha kuwa huyu ni mahiri katika kutoa taarifa katika Blog yake.

Natoa rai, kuwa mliopata nafasi ya kuwa na nguvu katika makampuni msitumie nafasi hizo vibaya kwa kutaka kuidhinisha udhamini wa blog kwa rafiki zenu na kisha kupoteza ladha ya ubunifu katika blog. Najua mmefanya hivi sana katika maeneo kama ya sanaa za urembo na kwingineko lakini kumbukeni hili limezidi na haliwezi kuvumiliwa! Jamhuri hii ilikuwepo kabla yenu na hiki mnachojivunia kwa kuwa kimetengenezwa na urithi wa Baba zenu msitarajie kitabaki kuwa hivi kila siku. 

Tendeni haki japo kidogo jamii hii itawaheshimu.

Kwa masikitiko na hasira kidogo nawasilisha!
Bonny Makene Road to PhD.

Tuesday, July 31, 2012

ORODHA YA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA CHETI MWAKA WA MASOMO 2012/2013

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI ORODHA YA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA CHETI MWAKA WA MASOMO 2012/2013 

MAELEKEZO MUHIMU

Waombaji waliochaguliwa kujiunga na mafunzo ya ualimu katika mwaka wa masomo 2012/13 wanatakiwa kuripoti katika vyuo walivyopangiwa tarehe 12/08/2012. Kwa wale watakaochelewa kupata barua za maelekezo (Joining instruction) kutoka vyuoni wanatakiwa waripoti vyuoni katika tarehe iliyopangwa bila kukosa. Wanafunzi wanatakiwa kufika vyuoni wakiwa na mahitaji yafuatayo:

 1.Vyeti halisi vya Baraza la Mitihani la Tanzania Kidato cha NNE na SITA kulingana na kozi husika.

 2. Ada kwa mwaka ni shilingi 200,000/=. (Muhula wa kwanza shilingi 100,000/= na muhula wa pili shilingi 100,000/=). 

3.Sare ya Chuo kulingana na maelekezo ya chuo husika . 

4. Fedha za matumizi binafsi. 

Aidha, kila Mkuu wa Chuo anatakiwa kuhakikisha wanafunzi wanaosajiliwa chuoni ni wale waliopo kwenye orodha hii tu na SI vinginevyo.

BOFYA HAPA KUANGALIA ORODHA YA MAJINA

ORODHA YA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA STASHAHADA MWAKA WA MASOMO 2012/2013

 WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
ORODHA YA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA STASHAHADA  MWAKA WA MASOMO 
2012/2013


MAELEKEZO MUHIMU
Waombaji waliochaguliwa kujiunga na mafunzo ya ualimu ngazi ya Stashahada katika mwaka wa masomo 2012/13 wanatakiwa kuripoti katika vyuo walivyopangiwa tarehe 12/08/2012. 

Kwa wale watakaochelewa kupata barua za maelekezo (Joining instruction) kutoka vyuoni wanatakiwa waripoti vyuoni katika tarehe iliyopangwa bila kukosa.
Wanafunzi wanatakiwa kufika vyuoni wakiwa na mahitaji yafuatayo:
1.Vyeti halisi vya Baraza la Mitihani la Tanzania Kidato cha NNE na SITA kulingana na kozi husika.


2. Ada kwa mwaka ni shilingi 200,000/=.  (Muhula wa kwanza shilingi  100,000/=  na muhula wa pili shilingi 100,000/=).


3.Sare ya Chuo kulingana na maelekezo ya chuo husika na


4. Fedha  kwa matumizi binafsi.


Aidha, kila Mkuu wa Chuo anatakiwa kuhakikisha wanafunzi wanaosajiliwa chuoni ni wale waliopo kwenye orodha hii tu na  SI vinginevyo.



Saturday, July 28, 2012

BIBI ANAYEFUGA MISUKULE ACHOMEWA NYUMBA

Nyumba ilichomwa moto na kuvunjwa vunjwa.
Nyumba ya bibi Irene iliyo teketezwa leo kwa moto kwa tuuma za uchawi. Bibi huyo ambaye  amekuwa akisadikiwa kuwa na tabia ya kuwachukuwa watoto wa majirani zake kwa nguvu ya giza ameumbuka leo baada ya mtoto mmoja aliye potea kwa muda mrefu kwao na kutajwa kuwa alishafariki dunia kisha leo kijana huyo ana kwa ana akakutana na ndugu yake.

Mshangao ulitawala kwa ndugu huyo ambaye kwa ujasili alianza kumuuliza unaishi wapi na kijana yule ndo akamwelekeza kua nipo kwa bibi mmoja anaitwa bibi Irene na tunaishi na wenzangu wengine ambao nilikutana nao pale kwa bibi wakiongezeka siku baada ya siku.

Bibi huyo ambaye anatajwa kuwa mkali katika vitendo vya ushirikina, kakutwa na hilizi kibao na mara baada ya kupata kichapo ambacho hata ivyo akikuonyesha kumdhuru kwa licha ya kupigwa na mawe, bakora na hata vitu vingine vigumu vya hatari hakutokwa na damu, kuvimba nundu wala kuonyesha makovu ya majeraha mwilini mwake, aliwambia wananchi kua watoto wengine wapo ndani na alipo ambiwa awatoe nje alifanya mandingo yake na walio toka ni bata na kuku.

Kwa sasa bibi huyo anashikiliwa na jeshi la police jijini Mwanza kwaajili ya usalama wake.

Thursday, July 26, 2012

MTOTO WA AJABU MWENYE VICHWA VIWILI AZALIWA TANZANIA


Mwanamke mmoja amejifungua mtoto mwenye vichwa viwili katika hospitali teule ya Wilaya ya Bunda, mkoani Mara.

Mganga Mkuu wa hospitali ya DDH Bunda, Dk. Willam Krekamoo, amemtaja mwanamke huyo kuwa ni Sarah Abenenego (16), mkazi wa mtaa wa Chiringe, mjini Bunda.


Dk. Krekamoo alisema mwanamke huyo alipokelewa hosptilini hapo usiku wa kuamkia jana akiwa anaumwa uchungu, na kwamba muda mfupi alijifungua mtoto wa kike akiwa na vichwa viwili, midomo miwili, macho manne na masikio manne.

Alisema mtoto huyo alizaliwa akiwa pia na mikono miwili na miguu miwili na kwamba baada ya muda mfupi alipoteza maisha.

Alisema uchunguzi unaonyesha kuwa ujauzito ulikuwa wa miezi saba na huo ulikuwa ni uzazi wake wa kwanza na kuongeza kuwa hali ya mwanamke huyo inaendelea vizuri.
 
 
via: NIPASHE

Ukiona dalili hizi 20 kwa mkeo, bora umuache tu!

TUKO kwenye Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, niwape pole wale waliojaaliwa kufunga na niwasihi wale wenye uwezo huo wafanye hivyo ili kumfurahisha Mwenyezi Mungu aliyetuumba.
Lakini nitoe angalizo kwa wale wenzangu na mimi wasiofunga, wajitahidi kutowaharibia swaumu wenzao. Wewe msichana uliyezoea kuvaa kimitego hebu funga breki kipindi hiki ili kutowatia majaribuni wenzako.
Aidha, kama wewe una mpenzi wako ambaye ni Muislam na wewe ni Mkristo, iheshimu imani yake na ikiwezekana mpe sapoti ili aweze kuvuka kipindi hiki salama.
Ndugu zangu, mmoja wa wadau wakubwa wa safu hii aliyejitambulisha kwa jina la Jafari wa Arusha, ameuliza swali ambalo nimeona ni vyema nikamjibu kupitia hapa ili na wengine waweze kufaidika
.
Yeye alitaka kujua jinsi anavyoweza kumbaini mwanamke asiye na mapenzi ya dhati kwa mumewe. Katika kujibu hili nimeorodhesha dalili 20 ambazo ukiziona kwa mpenzi wako ni bora ukamuacha tu.
Moja, Ni mwepesi wa kuanika udhaifu wako kwa watu wengine, ni mgumu wa kukusifia mbele za wenzake badala yake haoni noma kukuponda.
Mbili, anakuwa mgumu sana kukutambulisha kwa rafiki zake na ndugu.
Tatu, haonyeshi kubana matumizi kwa ajili ya maendeleo, kwake ni kufuja mali na anapokosa kupewa fedha ni mwepesi kulalamika.
Nne, anaahirisha mara kwa mara kukutana na wewe tena bila kukueleza sababu za msingi. 
Tano, anapokuwa anatoa maelezo ya mwanaume anayempenda kwenye maisha yake, sifa zake zinakuwa si zile ulizonazo wewe.
Sita, si mtu wa kucheka kwa furaha, hata kama ukimchekesha haoneshi furaha ya moyoni, tena mara nyingine anakuwa mkimya.
Saba, anajaribu kukuunganisha na wanawake wengine, haoni vibaya anaposikia unamfukuzia hata rafike yake badala yake anaweza hata kukutia moyo. Kwa kifupi hana wivu na wewe.
Nane, haumii pale inapotokea amekukosea, ni mwepesi wa kujitenga, kutozungumza na wewe na mwingi wa kukusukumia makosa hata kama yeye ndiye aliyekukosea.
Tisa, hataki kuambatana na wewe katika matembezi na ikitokea anakuwa mtu wa masharti sana. Ni rahisi kukuambia utangulie, yeye anakuja au mnaweza kutoka pamoja lakini yeye akawa anatembea mbali na wewe.
Kumi, siku zote ni mtu wa kupokea tu na si wa kutoa. Analazimisha kukumbatia mali zako na zake pia. Hupenda kufanya mambo yake kwa siri lakini hulazimisha kujua mipango yako.
Kumi na moja, hakumis hata unapokuwa mbali naye, kwa kifupi hathamini uwepo wako na anakuchukulia kama mtu wa akiba kwake.
Kumi na mbili, hakupi moyo pale unaposhindwa katika mambo unayopanga. Hachukui huzuni yako kama yake, hakufariji na hakusaidii pale ulipokwama.
Kumi na tatu, anayeweza kuchochea hisia mbaya kwa watu ili jamii ikuone mbaya, unayestahili kudharauliwa. Anakuwa mstari wa mbele kukuchafua katika maeneo ambayo anastahili kukusafisha.
Kumi na nne, hakupi kipaumbele katika maamuzi, anajiona yeye ndiye wa kwanza na wewe ni mtu wa kufuatia.
Kumi na tano, muwapo faragha anafanya bora liende, hakufikishi pale ambapo ulitarajia. Kwa kifupi anakuwa hana msisimko na wewe.
Kumi na sita, hakuhudumii tendo la ndoa mpaka siku amependa yeye. Ni mwingi wa kutoa sababu za kuchoka, kusingizia ugonjwa.
Kumi na saba, hazungumzii maendeleo yenu, ni mtu anayependa kufikiria maendeleo binafsi na ikiwezekana kuuza vilivyopo ili atimize malengo yake.
Kumi na nane, hataki kuambiwa ukweli na inapotokea akaambiwa huwa mkali na kuja juu mithili ya moto wa kifuu.
Kumi na tisa, hata akukosee vipi ni mgumu wa kuomba samahani na ikitokea umekosea wewe, ni mgumu kukusamehe kiasi kwamba kosa la mwaka jana anaweza kulikumbushia leo.
Ishirini, haoni hatari kukuambia; ‘Kama vipi tuachane, kwani nini....? Wapo wanaume wengi na wananitaka’.

WEMA SEPETU AFANANISHA MAPENZI YAKE NA DIAMOND KAMA YA CRISS BOWN NA RIHANA


MSANII anayeongoza kwa ku-make headlines kwenye vyombo vya habari kila kukicha Wema Sepetu, amedai kuwa mahusiano yake yeye na mpenzi wake Nasseb Abdul ‘Diamond’, ni kama ya nyota wa marekani Rihanna na Chris Brown, huku akiamini kuwa kila kitu wanachokifanya kinakuwa kinafanana.

Wiki iliyopita Rihanna na Chris Brown, walioneka kwa nyakati tofauti huko St. Tropez, France wakila bata na kujiachia, ambapo hiyo pia imetokea kwa Wema na Diamond ambapo nao walionekana pamoja pande za Kigoma, Diamond alipoenda kwenye ziara ya Kigoma all stars inayoshirikisha wasanii wanaotokea mkoa wa kigoma.

Wema akiongea na DarTalk alidai kuwa hakuna mtu anayeweza kumfanya ashindwe kula bata na mpenzi wake huo kwani anaamini kwa kufanya hivyo ndiyo njia moja wapo ya kuwakata vilimi wale wanaozungumza mabaya juu ya mapenzi yao.

Hata hivyo mwandishi wa habari hizi, alitaka kujua mipango yao ya baadaye juu ya mapenzi yao ambapo alidai kuwa juu ya hilo hawezi kuzungumzia kwani ni miezi kadhaa walikuwa katika matatizo hivyo bado wanakula bata na watakapofikia maamuzi ya kuvishana tena pete watafanya hivyo.

“Mapenzi yetu hayana matatizo kwani wanadamu kutofautiana hiyo ni hali ya kawaida, hivyo sioni kama kuna haja ya kuongea sana, na kitendo cha sisi kuonekana pamoja sehemu za bata kuna watu inawauma na sisi hatujali kwani kila mtu ana maisha yake,” alisema Wema.

Mbali na ishu hiyo pia, mwandishi alitaka kujua tena itakuwaje kwa upande wa Jokate, alijibu kwa upande wake hamuoni kama ni mtu wa maana kwani mapenzi yake hakuna wa kukatisha ingawa anaamini Jokate ni mtoto mdogo sana kwake.

 

MH: MKAPA AMEASA JAMII ZA KIAFRIKA ZIHAMASISHWE KUHUSU TOHARA YA HIARI KWA WANAUME.

Mhe. Benjamin Mkapa akiwasili hotelini tarehe 21 Julai 2012, kuhudhuria Kongamano la XIX la Kimataifa la UKIMWI linalofanyika Mjini Washington D.C. Kushoto ni Balozi wa Tanzania Marekani Mhe. Mwanaidi Sinare Maajar. 
Mhe. Benjamin Mkapa akisalimiana na Dr. Ellen Mkondya-Senkoro, Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa HIV/AIDS mara baada ya kuwasili hotelini tarehe 21 Julai 2012, kuhudhuria Kongamano la XIX la Kimataifa la UKIMWI linalofanyika Mjini Washington D.C.
Mhe. Benjamin Mkapa akipewa taarifa na Mhe. Mwanaidi Sinare Maajar, Balozi wa Tanzania nchini Marekani mara baada ya kuwasili Washington D.C kuhudhuria Kongamano la XIX la Kimataifa la UKIMWI kuanzia Julai 22-28, 2012. Wengine kwenye picha ni Dr. Ellen Mkondya-Senkoro, Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa HIV/AIDS na picha nyingine ni Ms. Eileen A. Swai, Msaidizi wa Rais Mstaafu Benjamin Mkapa. 
Mhe. Benjamin Mkapa akiwasili kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Washington Convention Centre Julai 23, 2012 kuhudhuria Kongamano la XIX la Kimataifa la UKIMWI linalofanyika Mjini Washington D.C. 
Ma-Champion wa HIV Free-Generation Rais Mstaafu wa Tanzania Mhe. Benjamin Mkapa na Rais Mstaafu wa Msumbiji Mhe. Joachim Chisano wakifuatilia mojawapo ya mikutano ya Kongamano la UKIMWI kwenye Ukumbi wa Mikutano wa mjini Washington. Pembeni ni Mhe. Mwanaidi SinareMaajar, Balozi wa Tanzania Marekani na Dr. Ellen Senkoro wa Taasisi ya Benjamin Mkapa.
Pichani Juu na Chini ni Ma-Champion wa HIV Free-Generation Rais Mstaafu wa Tanzania Mhe. Benjamin Mkapa, Rais Mstaafu wa Msumbiji Mhe. Joachim Chisano na Rais Mstaafu wa Zambia Mhe. Kenneth Kaunda wakijiandaa kabla ya mjadala kuanza kwenye mojawapo ya mikutano ya Kongamano la UKIMWI kwenye Ukumbi wa Mikutano wa mjini Washington D.C. 
Rais Mstaafu wa Tanzania Mhe. Benjamin Mkapa akihitimisha mjadala kuhusu Mpango wa Tohara ya Hiari kwa Wanaume ili kupunguza maambukizi ya UKIMWI kwenye mojawapo ya mikutano ya Kongamano la UKIMWI kwenye Ukumbi wa Mikutano wa mjini Washington D.C.
Washington DC;Mhe. Benjamin William Mkapa, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewaasa viongozi wa Nchi za Kiafrika kuchukua hatua ya kuhamasisha jamii za kiafrika kuhusu mpango wa tohara ya hiari kwa wanaume (Voluntary Medical Male Circumcision for HIV Prevention) kama mojawapo ya njia ya kupunguza maambukizi ya UKIMWI barani Afrika.
Mheshimiwa Mkapa aliyasema hayo alipokuwa anahitimisha mojawapo ya mijadala ya pembeni (Satelite Session) iliyokuwa inaendelea wakati wa Kongamano la XIX la Kimataifa la UKIMWI linaloendelea Mjini Washington DC, Marekani ambapo watu takribani 22,000 wanahudhuria. Mjadala huo uliovutia mamia ya wajumbe hususan kutoka Afrika kuhusu tohara ya hiari kwa wanaume, uliendeshwa na Bi. Brenda Wilson kutoka Afrika  Kusini ulielezea tafiti za kisayansi kuhusu mpango huo kama njia ya kupunguza maambukizi ya UKIMWI.
Rais Mkapa alisema mpango huu ni muhimu kutekelezwa na viongozi wa nchi za Kiafrika kwani imethibitishwa na tafiti zilizofanyika kwa Waafrika kwamba unapunguza maambukizi kwa asilimia 60, ambapo alisema si jambo dogo katika harakati za kutokomeza UKIMWI. Aliongeza kuwa ni mpango uliopendekezwa na sisi Waafrika wenyewe na ni wa hiari na hivyo hakuna atakayeshurutishwa.
 “Umebuniwa na nchi za magharibi, lakini umetafitiwa na kuthibishwa na sisi Waafrika wenyewe, hivyo ni mpango wetu huu” alisisitiza Rais Mkapa huku akishangiliwa kwa makofi na wajumbe wa mjadala huo.
Ili kutekeleza mpango huu wa tohara ya hiari kwa mafanikio, Mhe. Mkapa alielekeza mambo matatu. Kwanza nchi za kiafrika inabidi zitengeneze sera na mikakati madhubuti ya jinsi ya kukabiliana na janga hili la UKIMWI. Pili mipango na mikakati hiyo imilikiwe na wananchi wa nchi husika ili wao wenyewe wathibitishe ushiriki wao na sio kuonekana kama shuruti .Na mwisho mipango na sera za kukabiliana na UKIMWI itekelezwe kwenye mazingira ya ukweli na uwazi ili jamii za kiafrika ziweze kutambua athari za janga hili la UKIMWI.  Pia serikali nazo zitenge fedha za kusaidia katika mapambano haya na si kutegemea fedha za wafadhili tu.
“Umefika wakati sasa dunia nzima ielekeze nguvu zake kwenye kutokomeza ugonjwa huu hatari ambao unaua maelfu ya watu kila siku” Alisema Mhe. Mkapa na kuongeza kuwa mataifa mbalimbali duniani hutoa misaada haraka sana mara majanga ya dharura yanapotokea,  kama vile mafuriko, ajali n.k. Lakini janga la UKIMWI ni kama dharura  inayoendelea na sasa ni wakati muafaka dunia nzima itazame janga la UKIMWI kama dharura na inayoendelea.
Naye Mwenyekiti mwenza wa Mpango wa Tohara ya Hiari wa PEPFAR Dkt. Emmanuel Njeuhmeli alithibitisha tafiti hizo kwa kutoa mfano wa Zimbabwe ambapo maambukizi ya UKIMWI yanakadiriwa kupungua kwa asilimia 45 ndani ya kipindi cha miaka mitano ya utekelezaji wa mpango huo.
Wengine walioongea katika mjadala huo ni Angelo Kaggwa (Uganda), Mhe. Dkt. Speciosa Wandira (Uganda), Bi. Henrica Okondo (Kenya), Chifu Jonathan Mumena (Zambia), Mhe. Oburu Oginga (Kenya), Mhe. Dkt. Christine Ondoa (Uganda), na Mhe. Blessing Chebundo (Zimbabwe). Mjadala huo pia ulihudhuriwa na marais wastaafu wanaojishughulisha na mapambano dhidi ya Ukimwi  ( wajulikanao kama Champions for AIDS Free Generation)Mhe. Joachim Chisano, Rais Mstaafu wa Msumbiji na Mhe. Kenneth Kaunda, Rais Mstaafu wa Zambia
Mhe. Mkapa amehudhuria Kongamano hili kubwa la UKIMWI kwa mwaliko wa taasisi ya Champions for HIV-Free Generation inayoongozwa na Rais Mstaafu wa Botswana Mhe. Festus Moghae, ambapo Mhe. Mkapa ni mmoja wa Ma-Champion nane wa taasisi hiyo.
Kongamano la XIX la Kimataifa la UKIMWI limeanza Washington DC tarehe 22 Julai hadi 28 Julai 2012 ambapo watu mashuhuri na viongozi mbalimbali wa Marekani wamehudhuria akiwemo Rais wa Marekani Mhe. Barack Obama.  


Imetolewa na Ubalozi wa Tanzania Marekani
Julai 25, 2012

WAZIRI WA UCHUKUZI DR. HARRISON MWAKYEMBE AZINDUA HUDUMA MPYA ZA SHIRIKA LA NDEGE LA QATAR KUTOKA KIA.

Picha ya pamoja mara baada ya Shirika la ndege la serikali ya Qatar (Qatar airways) leo kuzindua  huduma ya safari zake za anga kutoka Kilimanjaro kuelekea sehemu mbalimbali za dunia kila siku na kufanya huduma za safari za anga kufikia zaidi miji 118.
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo,waziri wa mawasiliano na uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe akimkabidhi Mkurugenzi mtendaji wa masoko wa shirika hilo Bw. Marwan Koleilat  kwa niaba ya shirika hilo la ndege la Qatar zawadi ya picha yenye kivuli cha Mlima Kilimanjaro .
Mkurugenzi mtendaji wa masoko wa shirika la Qatar Bw. Marwan Koleilat  kwa niaba ya shirika hilo akimpa Mgeni rasmi katika uzinduzi huo,waziri wa mawasiliano na uchukuzi Dr. Harrison zawadi  ya yenye nembo ya ndege ya shirika hilo la Qatar.
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo,waziri wa mawasiliano na uchukuzi Dr. Harrison akizungumza mbele ya wageni waalikwa wakiwemo na wahariri wa habari kutoka vyombo mbalimbali (hawapo pichani),mapema leo kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa KIA.
Mkurugenzi mtendaji wa masoko wa shirika la Qatar Bw. Marwan Koleilat  kwa niaba ya shirika hilo akizungumza mbele ya wageni waalikwa wakiwemo na wahariri wa habari kutoka vyombo mbalimbali (hawapo pichani),mapema leo kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa KIA.
Kutoka kulia ni Mkurugenzi mtendaji wa masoko wa shirika la Qatar Bw. Marwan Koleilat,Waziri wa Uchukuzi Dr.Harrison Mwakyembe,Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya KADCO, Balozi Hassan Omar Gumbo Kibelloh pamoja na Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki wakijadiliana jambo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya KADCO, Balozi Hassan Omar Gumbo Kibelloh lakizungumza machache na pia kumkaribisha mgeni rasmi na wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla hiyo mapema leo iliofanyika kwenye uwanja wa KIA.
 Wakuu wa uzinduzi wakipga makofi kwa pamoja mara baada ya uzinduzi huo.
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo,waziri wa mawasiliano na uchukuzi Dr. Harrison akipiga makofi wakati kikundi cha ngoma za asili kikitumbuiza,shoto kwake ni Mkurugenzi mtendaji wa masoko wa shirika la Qatar Bw. Marwan Koleilat 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya KADCO, Balozi Hassan Omar Gumbo Kibelloh akimkaribisha Mkurugenzi mtendaji wa masoko wa shirika la Qatar Bw. Marwan Koleilat mara baada ya kuwasili na ndege ya shirika hilo aina ya Ndege namba QR546,shoto kwake ni  Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya KADCO, Balozi Hassan Omar Gumbo Kibelloh akimpokea Mgeni rasmi,Waziri wa Uchukuzi Dr Harrison Mwakyembe mara baada ya kuwasili KIA tayari kwa uzinduzi 
Mgeni rasmi,Waziri wa Uchukuzi Dr Harrison Mwakyembe akishuka kwenye ndege ya Qatar kwenye Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) akiwa ameambatana na Mkewe pamoja na  Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki.
 Ndege ya Qatar ikiwasili kabla ya kuzinduliwa rasmi KIA.
 Ikifanyiwa shower kwa mbwembwe zote.
 Wageni waalikwa mbali mbali wakisubiri kushuhudia uzinduzi huo.
Pichani kulia ni Mkuu wa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro Mhe.Novatus Makunga akizungumza jambo  na Mhariri Mkuu wa gazeti la Tanzania Daima,Bw.Absalom Kibanda.
Baadhi ya Wanahabari Waandamizi wakiwa kwenye uzinduzi huo mapema leo kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
 
 

Wednesday, July 25, 2012

NIGERIA U20 YAWASILI KUIKABILI NGORONGORO HEROES.


 
Kikosi cha timu ya Taifa ya Vijana U20 ya Nigeria (Flying Eagles).

Timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 ya Nigeria (Flying Eagles) inatarajia kuwasili nchini leo (Julai 25 mwaka huu) saa 10 jioni kwa ndege ya RwandAir ikiwa na msafara wa watu 30 wakiwemo wachezaji 18.
Flying Eagles itapambana na Ngorongoro Heroes katika mechi ya kwanza ya raundi ya pili itakayofanyika Jumapili (Julai 29 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.
Mechi hiyo ya kuwania tiketi ya kucheza fainali za 18 za Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 zitakazochezwa mwakani nchini Algeria itachezeshwa na waamuzi kutoka Kenya wakati Kamishna ni Charles Masembe kutoka Uganda.
Flying Eagles inayofundishwa na kocha John Obuh, jana (Julai 24 mwaka huu) ilicheza mechi ya kirafiki na Rwanda (Young Amavubi) kwenye Uwanja wa Amahoro jijini Kigali. Nigeria ililala bao 1-0.
Msafara wa timu hiyo unaongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Nigeria (NFF), Chris Green. Baadhi ya wachezaji walioko katika kikosi cha Flying Eagles ni Chidi Osuchukwu, Alhaji Gero, Shehu Abdullahi, Aminu Umar, Aliyu Mohamed, Uche Agbo, Jonah Usman, Harrison Egbune, Hassan Abubakar na Yahya Adamu.
Viingilio katika mechi hiyo vitakuwa sh. 3,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, bluu na kijani wakati VIP B na C itakuwa sh. 5,000. Kiingilio kwa VIP A itakuwa sh. 10,000.

NUSU FAINALI KOMBE LA KAGAME
Nusu fainali zote mbili za kuwania Klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame) mwaka 2012 zinachezwa kesho Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 15,000 na sh. 20,000.
Azam na AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) zitacheza nusu fainali ya kwanza kuanzia saa 8 kamili mchana, na kufuatiwa na nusu fainali ya pili kati ya Yanga na APR ya Rwanda itakayoanza saa 10 kamili jioni.

via. dewjiblog.com