Mkali wa Bongo Fleva, 20% siku ya jana alisaini mkataba chini la
Label ya Kombinenga inayomilikiwa na mtayarishaji wa muziki Man Water
kutoka katika studio za Combination Sound, 20% aliweza kusaini mkataba
wa miaka mitano kufanya kazi chini ya Label hiyo, ambayo itakuwa
ikimsimamia katika kazi zake.
“Kwa upande wake 20% alisema kuwa sasa amerudi rasmi kuja kuwachinja
tena na kusema amerudisha sauti ya gharama kwa jamii na mashabiki wake,
sauti yenye kuburudisha, sauti yenye kufunza na kutoa burudani kwa watu
wake” alisema 20%
Kwa upande wake Man Water amedai kuwa sasa 20% amerudi rasmi mwaka
2016 chini ya Kombinenga na kuwataka mashabiki wake mkao wa kula kupokea
kazi nzuri zenye ujumbe mzito na wakusisimua kutoka kwa msani huyo
“Twenty Percent is back. …2016
Kaa mkao wakula ngoma zenye jumbe nzito na za kusisimua…kila kitu kiko sawa sasa…new page” aliandika Man Water.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment