Tuesday, July 5, 2016

Baada ya ajali mfululizo zilizohusisha mabasi, polisi wamekuja na hii taarifa



Ni takribani wiki moja yametokea matukio makubwa matatu ya ajali za barabarani mfululizo ambayo yamehusisha mabasi yanayofanya safari zake mikoani, taarifa ya polisi imesema ajali hizo zimesababisha jumla ya vifo vya watu 46 na majeruhi 73.

Matukio hayo yanahusisha ajali iliyotokea June 28 2016 Misungwi Mwanza  ambapo basi la kampuni ya Super Samy likitokea Shinyanga kwenda Mwanza lilipata ajali kwa kuacha njia na kupinduka hivyo kusababisha vifo wa watu 5 na majeruhi 13.

Tukio lingine ni mnamo July 01 2016  VETA Dakawa katika barabara ya Morogoro/Dodoma malori mawili yaligongana na kuwaka moto na kusababisha vifo vya watu 5 na  na baadae katika eneo hilohilo siku July 02 2016 usiku gari la kampuni ya OTA lilipata ajali kwa kuyagonga mabaki ya malori yaliyopata ajali na kubaki eneo la tukio na kusababisha vifo  vya watu 6 na majeruhi 6

Halikadhalika mnamo July 04 2016 maeneo ya Maweni-Kintiku Singida mabasi mawili ya kampuni ya City Boys yaligongana na kusababisha vifo wa 30 na majeruhi 54 ambapo hadi leo wamebaki majeruhi 33 wakiendelea na matibabu. Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa polisi, kikosi cha usalama barabarani, Mohamed Mpinga amesema
>>>’kwa ajali iliyotokea Maweni Singida siyo ajali ya kawaida bali ni tukio la kufanya mauaji bila kukusudia, hivyo polisi imedhamiria kuwafikisha mahakamani madereva waliohusika na ajali hiyo kwa mashtaka ya mauaji bila kukusudia kutokana na taarifa za awali za chanzo cha kutokea kwa ajali hiyo kwamba madereva wa mabasi hayo walikuwa wakifanya mzaha wakati wa kupishana.

>>>Aidha tumewasiliana na wenzetu wa SUMATRA, kampuni ya mabasi ya City Boys na makampuni mengine yaliyohusika katika ajali yafungiwe kutoa huduma za usafirishaji katika njia zote hapa nchini
MWARICK JAPHET MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

No comments:

Post a Comment