Taarifa
niliyoipokea kutokea ikulu inasema kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa
kifungu cha 48 cha sheria ya tafsiri za sheria (Interpretation of Laws
Act) Sura 1, leo tarehe 5 Julai, 2016 ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa
Bodi ya Benki ya Maendeleo ya TIB Prof. William Lyakurwa.
Kufuatia
hatua hiyo, kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo chini ya kifungu cha 9 (2)
cha ya Sheria ya mashirika ya umma (Public Corporations Act) Sura 257,
Rais Magufuli amemteua Prof. Palamagamba J. A. M. Kabudi kushika nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Maendeleo ya TIB kwa kipindi cha miaka mitatu.
Kufuatia
mabadiliko hayo, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango kwa
mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa kifungu cha 48 cha sheria ya sheria ya
tafsiri za sheria (Interpretation of Laws Act) Sura 1, ametengua uteuzi
wa Wajumbe Bodi ya Benki ya Maendeleo ya TIB.
Aidha, kwa
mujibu wa mamlaka aliyonayo chini ya kifungu cha 9 (1) cha ya Sheria ya
mashirika ya umma (Public Corporations Act, Sura 257) Waziri wa Fedha
na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango ameteua wajumbe wapya wa Bodi
wafuatao kwa kipindi cha miaka mitatu
⦁ Brig. Gen (Rtd) Mabula Mashauri
⦁ Dkt. Razack B. Lokina
⦁ Bi. Rose Aiko
⦁ Prof. Joseph Bwechweshaija
⦁ Bw. Said Seif Mzee
⦁ Dkt. Arnold M. Kihaule
⦁ Bw. Maduka Paul Kessy
⦁ Bw. Charles Singili
⦁ Dkt. Razack B. Lokina
⦁ Bi. Rose Aiko
⦁ Prof. Joseph Bwechweshaija
⦁ Bw. Said Seif Mzee
⦁ Dkt. Arnold M. Kihaule
⦁ Bw. Maduka Paul Kessy
⦁ Bw. Charles Singili
Uteuzi wa Mwenyekiti na Wajumbe wapya wa Bodi unaanza tarehe leo July 5 2016.
No comments:
Post a Comment