WILAYA YA RUNGWE – MAUAJI.
MNAMO TAREHE 10.10.2013 MAJIRA YA SAA 14:30HRS HUKO KATIKA ENEO LA KIWIRA STENDI YA MAGARI WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA. MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA MOJA LA ISMAIL S/O ?, MIAKA
25, KYUSA, MKAZI WA UYOLE, ALIUAWA KWA KUPIGWA SEHEMU MBALIMBALI ZA
MWILI WAKE NA KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI
WAKITUMIA SILAHA ZA JADI MAWE, FIMBO NA MARUNGU KISHA MWILI WAKE
KUCHOMWA MOTO. CHANZO NI TUHUMA ZA KUJIHUSISHA NA MATUKIO YA UPORAJI WA PIKIPIKI NA KUWAUWA WAENDESHA PIKIPIKI @ BODABODA. MWILI
WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA MAKANDANA –TUKUYU. MSAKO MKALI
DHIDI YA WAUAJI UNAFANYWA.KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA
MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA
YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI BADALA YAKE WAWAFIKISHE WATUHUMIWA WANAO
WAKAMATA KWA TUHUMA MBALIMBALI KWENYE MAMLAKA HUSIKA ILI SHERIA ICHUKUE
MKONDO WAKE. PIA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA WALIKO
WAHUSIKA WA TUKIO HILO WAZITOE ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO
WAKE.
WILAYA YA CHUNYA – KUPATIKANA NA SILAHA [GOBOLE] BILA KIBALI.
MNAMO TAREHE 10.10.2013 MAJIRA YA SAA 14:00HRS HUKO KATIKA KITONGOJI CHA KININGA KIJIJI CHA KAPALALA WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA THOMAS S/O GERVAS, MIAKA 42,MKIMBU,MKULIMA,MKAZI WA KIJIJI CHA KAPALALA AKIWA NA SILAHA BUNDUKI AINA YA GOBOLE BILA KIBALI. MBINU NI KUFICHA SILAHA HIYO KATIKA KIBANDA CHAKE KILICHOPO SHAMBANI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI
ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUMILIKI SILAHA BILA KUFUATA
TARATIBU KWANI NI KOSA LA JINAI.
[DIWANI ATHUMANI - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments:
Post a Comment