Mwandishi wa habari wa ITV na Radio One, Ufoo Saro, pichani, katika moja ya matukio ya kikazi hapa nchini.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MWANDISHI wa ITV na Radio One, Ufuo Saro amedaiwa kupigwa
risasi ya tumbo na kupelekea kumjeruhi vibaya, huku mama yake mzazi naye akifariki
baada ya kupigwa risasi katika tukio hilo.
Habari
za awali zinasema kuwa mwandishi huyo pamoja na mama
yake wamefanyiwa kitendo hicho na kijana anayedaiwa kuwa ni mpenzi wa
Ufoo
Saro, ambaye inadaiwa alikuwa nao katika mazungumzo eneo la Kibamba nje
kidogo ya jiji la Dar es Salaam ndipo kijana huyo akadaiwa kuwafyatulia
risasi na kisha nayeye kujiua kwa risasi.
Watu mbalimbali katika mitandao ya kijamii wameonyesha
kushangazwa na tukio hilo alilofanyiwa mwanadada huyo anayefanya kazi katika
kituo cha ITV na Radio One, kinachomilikiwa na Kampuni ya IPP, chini ya
Mwenyekiti wake Reginald Mengi.
No comments:
Post a Comment