Kufuatia
mgomo wa mabasi ya abiria uliofanyika siku mbili zilizopita Baraza la
Ushauri la watumiaji wa huduma za Usafiri wa Majini na nchi kavu
(SUMATRA – CCC) limewataka abiria wote waliokatiwa tiketi za safari na
kushindwa kusafirishwa kwa wakati kudai fidia kwa kampuni za
usafirishaji walizoingia nazo mkataba.
Katibu Mkuu wa Baraza hilo OSCAR KIKOYO Mwenyekiti wa Baraza hilo AYOUB OMARY wamesema kilichofanywa na wasafirishaji abiria ni ukiukwaji wa sheria na hakipaswi kufumbiwa macho kutokana na kuwepo kwa taratibu za kugoma zinazowataka kurudisha leseni za usafirishaji SUMATRA kwa muda wote wanaotaka kugoma.
Katika hatua nyingine Katibu Mkuu huyo wa SUMATRA CCC amesema Jumapili ya tatu ya mwezi Novemba kila mwaka ni siku ya kuwakumbuka waathirika wa ajali za barabarani ambapo na kubainisha kuwa vifo vingi nchini vimekuwa vikisababishwa na ajali za barabarani.
No comments:
Post a Comment