Friday, October 11, 2013

SHULE ZA SEKONDARI, ZAHANATI NA VITUO VYOTE VYA AFYA VIWEKEWE UMEME HARAKA – RAIS KIKWETE


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. JAKAYA KIKWETE amewaagiza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuhahakisha kuwa shule zote za sekondari za kata, zahanati na vituo vyote vya afya nchini vinawekewa umeme haraka iwezekanavyo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu imeeleza kuwa Rais KIKWETE amesema kwa maeneo yenye umeme wa Gridi ya Taifa, taasisi hizo za umma zipatiwe umeme kutoka kwenye Gridi hiyo na kwa maeneo yasiyokuwa na umeme wa Gridi basi shule na taasisi hizo nyingine ziwekewe umeme wa jua.

Rais KIKWETE pia amewaagiza Wakuu wa Wilaya kusimamia ipasavyo programu ya kusambaza umeme na maji katika vijiji mbali mbali nchini akisisitiza kuwa lengo la kuwapatia umeme Watanzania asilimia 30 ifikapo mwaka 2015 linaweza kufikiwa na kuvukwa kama viongozi wanajipanga vizuri.
MWARICK JAPHET MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

No comments:

Post a Comment