Tuesday, February 19, 2013

BREAKING NEWS: KANISA LACHOMWA MOTO ZANZIBAR ASUBUHI HII

 
 
Breaking News:Kanisa moja limechomwa moto Visiwani ZNZ alfajiri ya leo na kwa Mujibu wa Kamishna wa polisi mjini MUSA ALI MUSA ,baadhi ya viti vya kanisa vimeungua na kwamba moto huo uliwahiwa kuzimwa kabla ya kusababisha madhara zaidi.Kwa taarifa zaidi endelea kuangalia ITV na Kusikiliza Radio One

SOURCE : ITV

DIAMOND AFANYA SHOW YA KIHISTORIA ARUSHA KWA KIINGILIO CHA SH. 150,000 NA MASHABIKI KUFURIKA, AVAA MAVAZI YA MICHAEL JACKSON


Katika blog yake mwanamuziki Diamond ameandika hivi "Kiukweli Namshukuru Sana Mwenyezi Mungu kwa kuweza kufanikisha usiku wangu huu wa Usiku wa Valentine 
uliofanyika Mjini Arusha ndani ya CLUB SAFARI CARNIVAL
Tareh 16/02/2013....maana ilikua ni mara ya Kwanza kwa Msanii wa kitanzania
kufanya show kwa Kiingilio kikubwa cha (150,000) Laki Moja na Nusu na watu kufurika
pasipo hata mimi kutegemea.....Kiukweli ilinifariji sana na kuona kweli Watanzania
wanathamini na kujali vipaji na sanaa zao tofauti na zamani tulikuwa tukiona show ya
 kiingilio kikubwa ni mpaka msanii wa kutoka nje akija nchini ndo watu ujaa kwa wingi..!
Inanipa hali ya kuzidi kufanya vizuri, kujituma na kuwa mbunifu zaidi ili nami kesho
na kesho kutwa niweze kuiweka Nchi yangu kwenye Ramani nzuri ya
 Tasnia ya Muziki....!!
 
Niushukuru Pia Uongozi mzima wa CLUB SAFARI CARNIVAL,
 MOUNT MERU HOTEL... Ma Boy
Victor,Erick na Wanangu wote Niliokuwa nao Pamoja Arusha..Bila kumsahau
My Blood Ibrah Madharau"
HONGERA SANA PIGA KAZI DIAMOND 












for more photos tembelea www.thisis diamond

Monday, February 18, 2013

HIZI NDO SHULE KUMI ZILIZO FANYA VIZURI MATOKEO YA FORM FOUR 2012


MATOKEO YA FORM FOUR YATANGAZWA.


SERIKALI imetangaza matokeo ya kidato cha nne mwaka 2012 ambapo kwa mwaka huu idadi ya wanafunzi waliofeli imeongezeka na kufikia laki mbili na arobaini.

Mbali na ongozeko la idadi ya wanafunzi waliofeli , ufaulu wa wanafunzi wa kike umekuwa mdogo ukilinganishwa na wa kiume.

Kati ya watahiniwa 126,847 ni watahiniwa 397,136 ndiyo waliofanya mtihani huo, wasichana waliofaulu ni 46,181 wakati wavulana waliofaulu ni 80,686 huku Waliofutiwa mtihani ni 789 kwa kosa la kuandika matusi katika mitihiani yao.

Shule kumi zilizotajwa kufanya vizuri ni pamoja na st. francis ya mkoani mbeya, marian wavulani ya pwani na fedha wavulana ya dar eslsaama.

Vuvugu la chinichini aliloanzisha Mama Sajuki Juu wa Wastara ni Hatari



IKIWA ni takribani siku siku 47 tangu alipofariki staa wa filamu za Kibongo, Juma Kilowoko ‘Sajuki’, kuna madai kuwa tayari visa vimeanza kati ya mkewe Wastara Juma na mama yake mzazi yaani mkwewe, Ijumaa Wikienda limetonywa.
 Wastara Juma.
Kwa mujibu wa chanzo makini, mama Sajuki amekuwa akidaiwa kumfuatilia Wastara kwa kila anachokifanya hadi kufikia hatua ya kuwaambia watu wamchunguze.
Chanzo hicho kilidai kuwa Wastara na mama Sajuki walifikia hatua ya kurushiana maneno mbele za watu huku ulemavu wa mjane huyo wa Sajuki ukitajwatajwa.
“Unaambiwa wakija watu kumuombea dua Wastara na kumwambia atapata mwanaume mwingine, mama Sajuki anashindwa kuvumilia na kujikuta akiangua kilio,” kilidai chanzo hicho.


Mama mzazi wa Sajuki.
Kiliendelea kudai kuwa siku moja Wastara alitembelewa na watu kwenye ofisi yake iliyopo ndani ya nyumba anayoishi, Tabata-Bima, Dar ambapo mama Sajuki alidaiwa kuwafuatilia watu hao akitaka kujua mazungumzo waliyokuwa wakifanya na mkwewe huyo.
Kiliendelea kutiririsha madai kuwa siku ya arobaini ya Sajuki, mama Sajuki aliwaka mbele ya kadamnasi akikasirishwa na kitendo cha Wastara kupiga picha akidai huko ni kujitangaza.

 
HUYU HAPA WASTARA
Hata hivyo, ilidaiwa kuwa sakata hilo lilihamishiwa usiku kwani Wastara naye alikuja juu akiomba waweke kikao ili kuweka mambo sawa mbele ya baba Sajuki, mzee Juma Kilowoko.
Baada ya kujazwa habari hizo, dawati la Ijumaa Wikienda lilimtafuta Wastara ili kusikia upande wake juu ya ishu hiyo ambapo alisema kuwa pamoja na yote, kwa upande wake anamheshimu mama mkwe wake.


MAMA SAJUKI ALIKUWA NA HAYA
Alipotafutwa mama, alikuwa na haya ya kusema:
“Ni kweli nilipata uchungu sana wakati wa arobaini kwani mama aliyekuwa akiendesha dua (Mariam Dedesi), alikuwa akisema tumuombee Wastara apate mwanaume mwingine, kama mzazi ni kweli nililia kwa uchungu na kutamka maneno mazito,” alisema mama Sajuki


MATOKEO KIDATO CHA NNE 2012 YATANGAZWA

MASHAURIANO KUUNDWA KWA SERIKALI MPYA TUNISIA

 

Mashauriano kuhusu kuundwa kwa serikali mpya nchini Tunisia yanakusudiwa kuanza tena. Waziri mkuu Hamadi Jebali anataka kubuni utawala wa kiteknokrasia. Mfumo huu wa kiteknokrasia hujumuisha utawala unaongozwa na wahandisi, wanasayansi na wataalam wengine. Lakini hatua hiyo inapingwa na kiongozi wa chama chake cha Ennahda, Rached Ghannouchi. Bwana Jebali ametishia kujiuzulu iwapo uamuzi wake, anaotarajia kuwa suluhisho la kisiasa nchini humo, utaendelea kupingwa na Ennahda.

Mzozo wa kisiasa ulizuka baada ya kuuawa kwa aliyekuwa kiongozi wa upinzani nchini humo, Chokri Belaid. Familia ya Bwana Belaid ilikilaumu chama hicho kwa kupanga mauaji yake. Chama hicho cha Kiislamu cha Ennahda kimegawanyika kati ya walio na msimamo wa kadri, wakiongozwa na waziri mkuu, na wale wenye itikadi kali, wanaoongozwa na Bwana Ganouchi.


BALOZI MWANAIDI SINARE MAAJAR ATEULIWA KUWA MWENYEKITI WA BODI YA CHUO CHA DIPLOMASIA


Balozi wa Tanzania Nchini Marekani Mhe.Mwanaidi Sinare Maajar akiwa kwenye
Picha ya Pamoja na Rais wa Marekani Barrack Obama,Mara baada ya kukabidhisha

hati ya utambulisho wa Balozi wetu Huyo Nchini Humo tarehe 16.09.2010


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Jakaya Mrisho kikwete

Amemteua Balozi Mwanaidi Sinare Maajar kuwa Mwenyekiti wa Bodi

ya Chuo cha Diplomasia(CFR) Kilichopo kurasini Jijini Dar Es Salaam.

WAFAHAMU WACHEZAJI WA SIRI YA MTUNGI VILIVYO LEO


ANGALIA PICHA ZA UCHAGUZI MDOGO WA M/KITI MTAA WA BANK WILAYANI MAGU BAADA YA KUTANGAZWA MSHINDI - CHADEMA YAONGOZA