Monday, March 11, 2013

PICHA YA UHURU KENYATTA KANISANI BAADA YA USHINDI.

.
.
Baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa Urais nchini Kenya jumamosi iliyopita, jana jumapili march 10 2013 Rais Uhuru Kenyatta alihudhuria ibada ya kumshukuru Mungu.
Standard Media wameripoti kwamba Rais huyu wa awamu ya nne aliwasili Kanisani huko Kiambu akiwa na ulinzi mkali ambao unalingana na levo yake ya Urais.
. 
Vilevile William Ruto ambae anatarajiwa kuapishwa kama Makamu wa Rais alihudhuria ibada ya kumshukuru Mungu kanisani jijini Nairobi.
Ruto alimwaga machozi wakati aliposimama mbele ya umati kutoa ushuhuda wa ushindi wao pamoja na kumshukuru Mungu kwa kuwapigania.
.

Thursday, March 7, 2013

TENGENEZA TANZANIA WASHIRIKI WA TUZO ZA MWANAMAKUKUKA 2012


Wednesday, March 6, 2013

Siri yavunjika kwa Kuvunjika kwa Ndoa ya Monalisa wa Siri ya Mtungi

SIRI ya kuvunjika kwa ndoa ya staa wa filamu Bongo, Yvonny Cherry ‘Monalisa’ imevuja ambapo imeelezwa kuwa tattoo aliyokuwa ameichora mkononi mwake yenye alama ya kopa na mshale ndiyo chanzo.
Akizungumza na Tollywood Newz jijini Dar es Salaam, Monalisa alisema: “Sikuwahi kuwaza hili hata mara moja. Siku moja Kanisani, Mchungaji aliniambia kwamba tattoo yangu ndiyo chanzo cha kunivurugia uhusiano wangu.

“Aliniambia kwamba, alama ya kopa ambayo humaanisha moyo – upendo, halafu mshale kupita katikati yake, humaanisha maumivu na kuteswa katika uhusiano. Lilikuwa jambo jipya kwangu lakini niliamua kufuta haraka sana na sasa nimeweka nyingine ya ua rose.” Source:Globalpublishers

FILAMU YA MWISHO KUCHEZWA NA KANUMBA KUINGIA SOKONI MWEZI UJAO


Filamu ya mwisho kuchezwa na marehemu Steven Kanumba LOVE & POWER itaingia sokoni tarehe 12 mwezi April mwaka huu. Pia marehemu Sharo milionea amecheza katika filamu hiyo. The lead actress is Irine Paul na Patcho Mwamba pia is in the movie. kaa tayari kwa ajili ya kujipatia copy original.


Tuesday, March 5, 2013

MAKAHABA WAAHIDI KUFANYA NGONO BURE KENYA:


WAKATI uchaguzi nchini Kenya ukiendelea makahaba wa Kisumu wametoa kali baada ya kutangaza kutoa ofa ya kufanya ngono bure kama mgombea urais Rail Ondika cord  atashinda.

Makahaba wa nchi hiyo wameamua kufuata nyayo za makahaba wa Nigeria walipoahidi kutoa penzi la bure kama timu yao itashinda katika mashindano ya AFCON  cup yaliyomalizika hivi karibuni, kwa bahati timu yao ilishinda lakini haikubainishwa kama walitimiza ahadi yao au la.

Makahaba hao walitoa ofa hiyo kupitia mtandao wa facebook ambao watu wengi wameunga mkono na kutoa mawazo yao.
`
Makahaba hao walieleza wataibatilisha ofa hiyo kama Uhuru Kenyata atashinda.

Utaratibu huo wa kutangaza ofa za ngono kwa makahaba unawashangaza na baadhi ya watu na kuamini ni njia ya kujitangaza zaidi na si ushabiki

The Kenyan Daily Post

Monday, March 4, 2013

HAYA NDIO MANENO MAFUPI YA DIAMOND KUHUSU KUNUNUA GARI JINGINE NA GHARAMA YA NYUMBA ALIYOMJENGEA MAMA

.
Diamond akiwa mbele ya Prado yake siku alipoamua kuitangaza kwenye media june 2012.

Kupitia post hii millardayo.com inakujulisha kwamba mwimbaji staa ambae ndio mwimbaji Mtanzania alieongoza kwa kuandikwa sana kwenye internet mwaka 2012, Diamond Platnums ametangaza mpango wa kununua gari jingine.
Tofauti na Prado aliyoinunua june 2012, Diamond hajataka kutaja ni aina gani ya gari aliloliagiza sasa hivi lakini kakubali kwamba kaliagiza Japan na litakua la gharama ya juu kuliko Prado.
Ukiachia mbali hilo gari analoliagiza, Diamond amekiri pia kwamba amemaliza kuijenga nyumba yenye gharama ya milioni mia mbili sitini ambayo ameijenga maalum kwa ajili ya mama yake mzazi.
Diamond ambae amekua akiandamwa na maneno maneno ambayo anaamini wanaoyasambaza ni wasiompenda amesema “mimi nikimtanguliza Mwenyenzi Mungu mbele ata mtu atake kunifanya kitu gani haweziii mpaka aandike Mwenyenzi Mungu mwenyewe, ndio maana wao kila wakipiga vita… mimi nazidi kuwa maarufu, nazidi kuwa na hela… sasa hivi nabadilisha Prado nanunua gari jingine….. jamani mtaiona”

VIA:millardayo.com

PENZI LA DIAMOND NA PENNY LAZIDI KUOTA MIZIZI





Damn! is she pregnant already?
863bcc8e7cd711e290cd22000a1f90d7_7
f15a59c07b3511e2b4f022000a1f9ac6_7
0d7bac787b3411e28c6a22000a9f3c64_7
4de83da67d7f11e28f8322000a9f18ae_7
6b15ef6c7cd611e2ad9722000a9e2977_7

R.I.P JUSTUS ESIRI

This is beginning to look like a not too pleasant year for Nigerian Entertainers as we're still mourning the passing away of Goldie, another movie icon, Justus Esiri, has died.Nigeriafilms.com has just gathered that Dr. Sid is now bereft, reports coming in now has it that he lost his dad to diabetes caused by old age. He was said to have passed on about an hour in a Lagos hospital.
More updates to come soon.

CHEKI TAARIFA KUHUSU LILE KANISA LA MASHOGA NIGERIA.

.

Ikiwa ni miezi mitatu tu imepita toka nchi nyingine ambayo ni maarufu Afrika (Kenya) kukumbwa na headlines za kutosha kuhusu raia wake wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja kupeana tuzo hadharani na kufanya sherehe, leo tena headlines zimehamia Nigeria.
Ndani ya miaka mitano iliyopita huko Nigeria kulikua na Kanisa ambalo lina waumini wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja tu liitwalo House of Rainbow lakini Kanisa hilo lilipotea baada ya kushambuliwa na wakazi wa Lagos ambao hawapendezwi na ishu za ushoga na usagaji.
Tarehe 3 March 2013 Mtandao maarufu wa Nigeria wa TFJ umeripoti kwamba kanisa hilo limerejea tena kwa kishindo na kuendelea na huduma zake.

Ni kanisa ambalo mwanzilishi wake ni mchungaji Mnigeria ambae ni shoga Rowland Jide Macaulay na imefahamika sasa hivi kwamba kanisa hilo lipo Ghana na Malawi, France, Netherlands, Cote d’Ivoire na Sierra-Leone.

Matukio punde yanapojiri:Uchaguzi Kenya

Wapiga kura tayari kwa foleni katika mtaa wa Kibera

Hii leo wakenya wanapiga kura katika uchaguzi wa kihistoria chini ya katiba mpya. Foleni tayari zimeanza kushuhudiwa katika vituo.
Kinyang'anyiro ni kikali kati ya Muungano wa Cord na Jubilee wa Raila Odinga na Uhuru Kenyatta.
Kwenye ukurasa huu tutakupasha matukio kila yanapojiri hadi upigaji kura utakapokamilika mwendo wa saa kumi na moja jioni.


10:39 Mwandishi wa BBC aliye mjiniNyeri anasema kila baada ya nyumba kumi kuna kituo cha kupigia kura, wapiga kura wamejitokeza kwa wingi, baadhi ya mashine za tume ya uchaguzi zilifeli lakini baada ya kushughulikiwa mambo yakarejea kuwa sawa.
i
10:31 Mwandishi wa BBC mjini Eldoret Wanyama wa Chebusire vituo vilifungua mapema mambo, yameenda shwari kwa ujumla wake, lakini katika baadhi ya vituo, kumekuwa na mushkil , mashine ziligoma katika kituo cha kupigia kura cha shule ya msingi ya UG, zaidi ya wapiga kura elfu tatu , hadi sasa ni chini ya watu hamsini wamepiga

10:27 Mkuu wa tume huru ya uchaguzi Isaac Hassan anahutubia waandishi wa habari kuhusu changamoto inazokabiliwa nazo tyume hiyo. Isaac anasema vituo vilivyofungua kuchelewa, vitahakikisha wapiga kura wote wamepiga kura

10:22: Ingawaje tume ya uchaguzi IEBC inawakubalia watu wawasindikize wazee au wagonjwa kupiga kura, wapigaji kura wengine wanawakataza kufanya hivyo. Mjini Kisumu katika kituo cha upigaji kura cha Ukumbi wa Aga Khan, mwandishi wetu Ann Mawathe dada mmoja alieyejipandikiza blanketi tumboni ili kuwahadaa watu na akubaliwe kwenda hadi mwanzo wa foleni, alikatazwa kufanya hivyo na wapiga kura wenzake.
Katika kituo hicho hicho, baba fulani aliyekuwa amebeba kipochi cha mkewe aliyekuwa na mtoto mgongoni, naye alirudishwa hadi nyuma kabisa ya foleni hiyo. Pia, mwanamume mwingine aliyejitwika ufahari fulani kwa vile alikuwa kavalia suti, na kutaka kuruka foleni, alikatazwa kufanya hivyo.

Wapiga kura mjini Nairobi katika kituo
09:04 Waziri mkuu Raila Odinga ambaye pia anagombea urais amepiga kura yake katika eneo la Kibera. Amesema licha ya kupata habari za baadhi ya vituo vya kupigia kura kuwa na hitilafu kidogo, wapiga kura wasiwe na wasiwasi kwani mambo yatakuwa shwari
08:43 Mgombea wa urais wa muungano wa CORD, waiziri mkuu Raila Odinga anatarajiwa kupiga kura yake wakati wowote kuanzia sasa

08:30Solomon Mugera anasema kwamba kupiga kura kunachukua takriban dakika 12
08:25 Hassan Majid pia mwandishi wa BBC anasema kuwa polisi wamepata mwili mmoja wa mtu aliyeuawa na mwingine kujeruhiwa kwa kukatwa panga katika eneo la Moshomoroni

08:24 Mwandishi wa BBC mjini Mombasa, Karen Allen anasema kuwa polisi wamepata maiti za polisi wanne ambao wameuawa katika eneo la eneo la Changamwe , Kaskazini mwa Mombasa. Hana taarifa zaidi kwa sasa
yuko katika kituo cha Menengai mjini Nakuru kura ilianza kupigwa saa moja asubuhi na foleni ni ndefu ingawa inakwenda polepole mwendo wa kobe

08:15:Fatma Sanbur yuko mtaani Kibera na anasema watu ni wengi sana lakini hakuna mbinu ya kupanga foleni. Anasema watu wanapangwa kwa orodha ya majina na hata baada ya saa moja tangu waanza kupangga foleni saa kumi na moja, shughuli yab upigaji kura ilikuwa haijaanza
upigaji kura unaendelea bila wasiwasi na kuwa wanatarajia shughuli itakamilika kwa muda bila wasiwasi
Usalama ulidhibitiwa asubuhi na mapema wakati upigaji kura ulipoanza
07:28: Mgombea mwenza wa Uhuru Kenyatta, William Ruro amepiga kura mjini Eldoret

07:32: William Ruto anasema kuwa anajivunia uchaguzi wa Kenya unafanyika kwa amani licha ya dukuduku la wengi. Anasema anawataka wapinzani kukubali matokeo ya uchaguzi vyovyote matokeo hayo yatakavyokuwa.
07:43 Upiga kura bado haujaanza katika baadhi ya sehemu za Kenya. Wapiga kura wanalalamika kuwa katika vituo kadhaa tarakilishi zimegoma na kwa hivyo watasubiri muda kabla ya kupiga kura zao

07:47Eco Seyar Papa akiwa mjini Nairobi anasema Wakenya wamejitokeza kwawingi jijini Nairobi katika eneo la Dagoreti. Foleni zilianza kupigwa kuanzia saa tisa usiku tangu kuanzishwa kwa demokirasia ncini Kenya watu waeneo hili hawajawai kujitokeza kwa mapenzi kama inavyo onekana.
07:50 Mwandishi wa BBC Ann Mawathe yuko mjini Kisumu na anasema ameona foleni ndefu sana watu wakiwa hamasa kupiga kura. Wamepiga foleni tangu saa nane usiku.

Foleni ya watu mjini Mombasa
07:52 Mombasa eneo la Kaloleni mpiga kura mmoja amesema hadi kufikia sasa upigaji kura haujaanza kwani maafisa wa tume ya uchaguzi bado hawajawasili na vifaa vyao

Sunday, March 3, 2013

Waziri Mkuu Pinda katika mahafali ya tano ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph.



Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akimkabidhi zawadi mwanachuo bora wa taluma ya Electronics Communication Engenering , Amanda Chitemo (kushoto) katika Mahafali  ya tano ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph, jijini Dar es salaam  Februari 2, 2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimpongeza, Edith Tomas ambaye alitunukiwa Shahada ya Computer Science and Engenering  katika mahafali ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph yaliyofanyika jijini Dar es salaam Machi 2, 2012. (Picha na Ofisi ya Wazir Mkuu).

HIZI NI KURASA ZA MWANZO NA ZA MWISHO ZA MAGAZETI YA LEO MAR 3 2013.

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.