Thursday, November 21, 2013

TAMKO LA FAMILIA ILIYOKUMBWA NA MAUAJI JUZI JUMANNE UKWELI KUHUSU CHANZO CHA MAUAJI HAYO


Juzi jumanne asubuhi hapa Dar es salaam kulitokea tukio la kutisha la mauaji na kuliacha jiji hili la Dare es salaam na maswali mengi na kila mtu kusema lake.Tukio hilo la kutisha liliikuta familia ya Alfred  na Hellen Newa katika nyumba yao iliyopo Ilala sharif Shamba.Familia hiyo ina watoto wanne Caroline Newa,Alpha Newa,Christina Newa,na Mlowi kaka yao.
Mwanaume aliyefahamika kwa jina la Gabriel Munishi (35) mkazi wa kitangiri Mwaza alifika katika nyumba hiyo na kufanya mauaji na kujeruhi kwa kutumia bastola
 
Wahanga wa mauaji hayo
Captain Francis Khianga Shumila raia wa Kenya na ni mume wa Caroline (amefariki)
 Alpha Alfred Newa(alifariki)
 Christina Nando Alfred Newa mpenzi wa zamani wa Gabriel(alijeruhiwa)
Hellen Newa mama yao mzazi(alijeruhiwa)
Gabriel Munishi  mkazi wa Kitangiri Mwanza mpenzi wa zamani wa Christina(alijiua baada ya kuua na kujeruhi)
 
Chanzo cha mauaji haya
Gabriel na Christina walikuwa ni wapenzi  Gabriel akiwa anaishi Mwanza maeneo ya kitangiri.Katika mapenzi hayo yalijaa ukatili na unyanyasaji ambao Christina alishindwa kuvumilia na kuamua kuachana na Gabriel.Chanzo cha haya yote ni Gabriel kutokukubali kuachwa.
Mahusiano ya kimapenzi kati ya Gabriel Munishi na Christina Newa
Wawili hawa walikuwa wapenzi lakini mapenzi yaliyojaa mateso ya hali ya juu.Gabriel alikuwa akimtesa sana Christina kwa vipigo na vitisho vya bastola kuwa atamuua.Miezi miwili iliyopita Gabriel alikuwa amemfungia Christina ndani ya nyumba akimpa vipigo na akiwa hawezi kutoka nje.Tukio ambalo ilibidi ndugu zake watoke Dar es salaam mpaka Mwanza  na kuhusisha polisi Dar es salaam na polisi Mwanza kuomba msaada ilikumtoa ndugu yao ndani ya nyumba hiyo.Baada ya kufanikiwa kumtoa wakarudi Dar es salaam na Christina kusitisha uhusiano huo.Baada ya kufanya hivyo Gabriel akawa akitoa vitisho kwake akimwambia akimuacha ataiteketeza familia yake.
Kabla ya tukio Gabriel alikuwa akibembeleza sana Christina amrudie lakini Christina alimwambia apumzike kwanza kwa miezi mitatu na akamshauri atafute psychological help.Amekuwa akimuona ni mtu wa hasira kila wakati,vipigo visivyoisha na mbaya zaidi akimtishia kumuua mara kwa mara  kitu ambacho sio cha kawaida hivyo ni bora akamuone daktari.Akishapata msaada ndio atakuwa tayari kuwa nae tena ila kwa sasa amuache kwanza.
 
Siku ya tukio miezi miwili toka christina na Gabriel kuachana
Kabla ya tukio Gabriel alikuwa akifika mara kwa mara maeneo ya nyumbani hapo.Alikuwa akifikia katika hotel ya Double M anakaa juu gorofani na kuchunguza kila kinachoendelea kwenye nyumba yao.Maana ukiwa hotelini juu unauwezo wa kuona nyumbani kwao sababu ni pembeni tu ya hotel.
Siku ya tukio Christina alikuwa akisafiri kwenda syprus.Kwenye gari alikuwa akiendesha mume wa dada yao Caroline marehemu captain Fransis Shumila,pembeni alikaa mdogo wao Alpha ambae ni marehemu.Nyuma alikuwa amekaa Christina na mama yao mzazi.Wakiwa wanatoka nyumbani walikuwa wanaenda kumdrop Alpha kazini ambae alikuwa akifanya kazi Barclays bank,Christina akamalizie shopping zake za mwisho halafu wampeleke airport.Wakiwa wanatoka getini ndio Gabriel akatokea na bastola akafyatua risasi na kufanya mauaji ya Alpha na Fransis aliyefia hospital jana kisha kuwajeruhi mama yao mzazi pamoja na Christina.Alipomaliza aliona kashaua na yeye kujiua kwa kujipiga risasi.
 
Maelezo haya ni kwa mujibu wa dada yao Caroline Newa aliyezungumza na clouds fm leo.
Malalamiko ya Caroline kwa polisi
Caroline na familia wamesikitishwa na polisi kushindwa kuwapa ushirikiano.Baada ya kupokea vitisho kutoka kwa Gabriel kuwa atawauwa na kuteketeza familia nzima waliripoti polisi.Wanasema walishafika mpaka kwa CID Ilala kumueleza juu ya vitisho vilivyotolewa na Gabriel wakaomba wapewe hata RB lakini polisi waliwaona wazushi.Matokeo yake madhara yamekuja kutokea wakati polisi walikuwa na uwezo wa kutoa msaada kabla ya hili.Pia alielezea kwa familia ya Gabriel kushindwa kuwapa ushirikiano toka mwanzo wakiwajibu hayo ni mambo yao ya kimapenzi wao hayawahusu walivyokutana hawakuwepo.
 Marehemu Alpha na mumewe na watoto katika picha enzi za uhai wake
Alpha Alfred Newa alikuwa mfanyakazi wa bank ya barclays toka 2004.Wakati mauti yanamkuta alikuwa Corporate Service Manager wa bank hiyo  na hivi ndivyo wafanyakazi wenzake walivyopewa meseji official ya maombolezo ya msiba huo mzito wa mwenzao.
Marehemu kuzikwa Goba jumamosi hii shambani kwa mama yake ameacha mume na watoto wawili mmoja wao akiwa na miezi 6 tu.
 
Pole kwa familia zote zilizokumbwa na majanga haya Mungu awape wepesi wa kupita kwenye kipindi hiki kigumu.
Na Dina Marios

MWARICK JAPHET MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

No comments:

Post a Comment