KUTOKANA NA WASANII WENGI WAIMBAJI WA WILAYANI MAGU KUTO SIKIKA KATIKA ULIMWENGU WA MUSIC KWA MUDA MREFU IMEKUWA TATIZO!!!!!
Sasa GRAB SOUND RECORDS Ipo Wilayani Kufufua na Kuendereza Vipaji Vyote vya Hapa Wilayani na Tanzania Kwa Ujumla Sasa Kama na wewe Ni Mmoja wa Sanaa Hii Nzoo sasa au wasiliana nasi Kwa Simu namba: 0764 251064 King Sele au 0758 490328 P-Tod Prod
KUNA kila dalili kwamba Serikali
inajipanga kufuta kodi ya Sh1,000 kila mwezi kwa wamiliki wa laini za
simu baada ya kuwapo kwa malalamiko kutoka kwa wananchi, taasisi na
baadhi ya kampuni za simu nchini. (HM)
Hiyo inatokana na kauli ya Naibu
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba aliyoitoa
jana akisema kwamba wizara yake ilipinga tangu awali mpango huo kabla ya
kupitishwa na kuwa sheria na kwamba anaamini itaondolewa. Kauli hiyo ya
Makamba imekuja siku moja baada ya chama tawala, CCM, kukaririwa na
vyombo vya habari kikiitaka Serikali kuangalia vyanzo vingine vya mapato
badala ya tozo hiyo.
Akizungumza kwa simu jana Makamba
alisema: “Sikubaliani na hili suala na kupita kwake ilikuwa ni kuzidiwa
nguvu. Lakini najua haliwezi likatekelezeka ni lazima litabadilishwa kwa
kuangalia eneo lingine la kutoza kodi.”
Alisema msimamo wa wizara yake katika
suala hilo ni tofauti kwani imekuwa ikijitahidi kuhakikisha gharama za
mawasiliano zinapungua... “Wizara hatukubaliani na kodi hiyo. Nia yetu
ni kupunguza gharama za kupiga simu kwa kuwa ni kitu kinachowezekana.
“Nia yetu ni kushusha gharama iwe
sifuri kabisa, kitu chochote kinachopandishwa bei sisi hatukubaliani
nacho kwa kuwa ni kuwaumiza wananchi wetu hasa wa vijijini. Bidhaa
ambayo inatakiwa kushuka ni mawasiliano hivyo lazima iwe hivyo.”
Jana, Waziri wa Fedha, Dk William
Mgimwa alisema kwamba Serikali inapokea maoni ya wadau mbalimbali ili
kuona namna ya kufanya marekebisho ya tozo hiyo. Hata hivyo, alisema
uamuzi wa kuanzisha tozo hiyo haukuwa wa Serikali bali ulipitishwa na
kukubaliwa baada ya kujadiliana na Kamati ya Bajeti inayoongozwa na
Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), Andrew Chenge.
“Hayo yalipendekezwa na Kamati ya
Bunge siyo Serikali. Tena walipendekeza vyanzo 67 vya kodi likiwamo hilo
la kadi za simu. Walipendekeza tukate Sh1,450 kwa mwezi, lakini sisi
Serikali tukashusha hadi Sh1,000 yaani kila mwananchi akatwe Sh33.3 kwa
siku na mapato yatakayopatikana yatakwenda kuboresha miradi ya maji,
umeme vijijini na barabara,” alisema Dk Mgimwa.
Upinzani mkali
Wabunge wa Chadema, John Mnyika wa
(Ubungo) na Zitto Kabwe (Kigoma Kaskazini), wamekuwa mstari wa mbele
kupinga kodi kwa kuonyesha jinsi itakavyowanyanyasa wananchi.
Mnyika amekuwa akikusanya saini za
wananchi wanaopinga mpango huo wa Serikali ili awasilishe bungeni hoja
ya wananchi kupinga tozo hiyo. Hadi sasa ameshakusanya saini zaidi ya
26,000.
Kwa upande wake, Zitto alisema kodi
hiyo haikujadiliwa kabisa kwa kuwa iliondolewa katika mapendekezo ya
mapato lakini ikarejeshwa kupitia Muswada wa Fedha ambao hutafsiri
hotuba ya Bajeti kisheria.
“Kama kodi hii haikuwa kwenye hutuba,
haikujadiliwa na Bunge, msingi wa Muswada wa Fedha kuwa na kodi hii
haupo. Kodi hii ilirejeshwa kinyemela bungeni na kupitishwa bila
mjadala.”
Hata hivyo, Dk Mgimwa alipinga hoja akisema muswada huo uliokuwa na kipengele cha tozo hiyo ulijadiliwa na kupitishwa na Bunge.
Profesa wa Sayansi ya Siasa wa Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Gaudence Mpangala alisema kodi hiyo
imelenga kuwakandamiza zaidi wananchi. “Hiyo kodi itawakandamiza
wananchi wa chini wanaofanya kazi ndogondogo kujipatia kipato, lakini
wazalishaji wakubwa hawataathirika. Tuendelee kulalamika hadi ifutwe,
hatuwezi kuwa na ujenzi wa demokrasia kama watu wa ngazi ya chini
wanakandamizwa,” alisema.
Chanzo: mwananchi
Share Post
MWARICK JAPHET MUJUNGUWeb Developer
Jumuika Nami Kwenye:
ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.
No comments:
Post a Comment