Friday, July 19, 2013

HAPPY BIRTHDAY DR.CHENI, HIKI NDICHO ALICHOKIANDIKA LULU.



Mwigizaji maarufu Swahiliwood Muhsin Awadhi(Dr. Cheni leo anaadhimisha siku yake ya kuzaliwa(birthday). Kama kawaida kwa siku muhimu kama hii kwa kila mtu, watu mbalimbali humtakia mhusika afya njema na maisha marefu, mafanikio na kila la kheri huku wengine pia wakitoa au kuelezea hisia zao kwa mlengwa. 

Elizabeth Michael(Lulu) nae ameamua kumtakia Dr. Cheni kheri ya siku ya kuzaliwa kwa kumuelezea kuwa Dr. Cheni ni mtu muhimu sana katika maisha yake kwakuwa na upendo wa dhati kwake na kumthamini. "Daah..don't even know where to start!!!!okay....umekuwa ni mtu muhimu sana katika maisha yangu...mtu mwenye kunipenda kwa dhati na kunithamani...kila ninapokuwa najaribu kukuelezea huwa nakosa cha kuongea na najisikia kulia tu....!!!nina uhakika sina cha kukulipa zaidi ya kukuombea uishi maisha marefu yenye amani,afya na faraja!!!HAPPY BIRTHDAY DADDY CHENI......♥" alisema Lulu mmoja wa actresses maarufu katika Swahili movies.

Dr. Cheni ndiye aliyemuingiza Lulu katika sanaa kwa kumpeleka Kaole na hata baada ya kukumbwa na matatizo bado yupo bega kwa bega na Lulu. Dr. Cheni ni mmoja wa waigizaji wenye mchango mkubwa katika tasnia ya maigizo na filamu nchini akiwa ametamba na michezo kadhaa kipindi hicho ITV na baadaye katika filamu na kupelekea waigizaji wengi chipukizi kuhamasika kuingia katika sanaa ya filamu. Baadhi ya filamu alizoigiza ni pamoja na Nipende Monalisa, Danger Zone, Majanga, Jessica na nyinginezo.


HAPPY BIRTHDAY Muhsin Awadhi(Dr.Cheni)


                                       Lulu na Dr. Cheni



MWARICK JAPHET MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

No comments:

Post a Comment