Na Mroki Mroki, Arusha
MAPOKEZI ya Kihistoria katika jiji la
Arusha yamefanyika leo wakati wafuasi, Mbunge wa Arusha Mjini kwa
Tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Godbless Lema
walipo miminika kwa Wingi kuanzia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Kilimanjaro (KIA) hadi katika Viwanja vya Kilombero mjini hapa
alipohutumia maelfu ya wana CHADEMA Arusha Mjini.
Mapokezi yahoo yamefanyika wakati
Godbless Lema alipokuwa akirejea mjini Arusha akitokea jijini Dar es
Salaam kusikiliza hukumu ya Rufani ya Keshi yake ya Kuvuliwa Ubunge
iliyotolewa maamuzi ya kumrejeshea Ubunge wake Desemba 21,2012.
Maelfu ya wananchi wakiwa katika
msafara mrefu zaidi ya pikipiki 500 na magari ulianzia Uwanja wa Ndege
KIA mara baada ya Mbunge huyo kuwasili uwanjanai hapo majira ya saa 4:20
Asubuhi.
Aidha Maandamano hayo ya Mapokezi ya
Mbunge huyo, hayakuwa na hata chembe ya Askari Polisi waliovalia sare
wala magari yao ya diria kama ilivyozoeleka na kuyafanya yafanyike kwa
amani na utulivu katika maeneo yote yaliyopita.
Huku wakiimba nyimbo za furaha hasa
zile za “Oya oya Jembe letu limerudi” Wanachadema hao walijigawa na
baadhi kulinda amani huku wengine wakiongoza magari.
Father Kidevu Blog ilishuhudua maelfu
ya wakazi wa mji wa Arusha wakiwa katika hali ya furaha na kusimama
kando ya barabara kushuhudia mapokezi ya Mbunge huyo.
“Haijawahji tokea hapa Arusha, kuwapo
kwa msafara mrefu namna hii wa mapokezi ya kiongozi yeyote Yule, tena
yakiwa na amani ya kiasi hiki,” alisikika akisema mmoja wa Watu
waliojitokeza kushuhudia tukio hilo.
Licha ya Kufanya mapokezi hayo na
Kumshukuru Mungu kwa Mbunge wao kurejea madarakani, lakini Wakazi wa
Arusha na Wapigakura wa Godbless Lema wamesema hivi sasa Mbunge huyo
anapaswa kutulia na kutumia kipindi kilicho baki cha miaka miwili ya
madaraka yake kuwatumikia wananchi katika kuhakikisha miradi ya
Maendeleo inafanyika Jimboni humo na kuachana kabisa na migomo na
maandamano ya kila mara.
“Sasa Lema anatakiwa kututumikia
wananchi maana sisi tumesha mtumikia yeye vya kutosha kwa kuwa nae bega
kwa bega katika kipindi chote cha uongozi na hata alipokumbwa na
msukosuko wa kuondolewa Ubunge, hivyo sasa ni wakati muafaka wa yeye
kuwaletea maendelea wana Arusha Mjini,” alisema Meshack Siriwa.
Godbless Lema alivuliwa Ubunge na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha Aprili 5, 2012
mbele ya Jaji Mfawidhi wa Kanda ya Sumbawanga, Gabriel Rwakibarila katika hukumu ya kesi ya kupinga matokeo ya Ubunge Jimbo la Arusha yaliyo wasilishwa na wanachama watatu wa CCM waliotaka Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kutengua ushindi wa Mbunge huyo.
mbele ya Jaji Mfawidhi wa Kanda ya Sumbawanga, Gabriel Rwakibarila katika hukumu ya kesi ya kupinga matokeo ya Ubunge Jimbo la Arusha yaliyo wasilishwa na wanachama watatu wa CCM waliotaka Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kutengua ushindi wa Mbunge huyo.
Wafuasi wa Lema wakishangilia barabarani wakati Mbunge huyo akipita.
Mbwembwe za waendesha pikipiki wengine ziliwashinda na kuanza kuanguaka.
Furaha hiyo ilikuwa kwa kilu aliye Mwanachadema
Skafu na vitru mbalimbali vilivyo na alama ya CHadema viliuzwa jijini Arusha kwa wingi.
Mke wa Mbunge Godbless Lema akiwa kwenye gari pamoja na mtoto wao wakati wa mapokezi hayo.
Lema Arusha anafananishwa na Barack Obama
Watu walining'inia katika magari bila hofu
Huyu na e'eti' alikua anachukua kumbukumbu za Video....
Lena akiwa nba Mbunge wa Arumeru Mashuari CHADEMA, Joshua Nasari.
No comments:
Post a Comment