Sunday, December 23, 2012

KAMA ULIKUA HUJUI, HUYU NDIO STAA WA AFRIKA ANAEPANGA KUNUNUA NYUMBA DAR ES SALAAM.


 
.
Mungu akijalia 2013 utakua mwaka ambao Tanzania itaingia kwenye headlines, Tanzania itapata mgeni miongoni mwa wageni ambao wamepanga kuja kuishi hapa.

Pamoja na ustaa alionao na utajiri alionao ambao umetokana na muziki anaoufanya, mkali ambae alichaguliwa kuiwakilisha Congo DRC kwenye kolabo na R. Kelly, mkali ambae alipenyeza mpaka kupata shavu la kufanya kolabo na staa Olivia wa G unit time hizo, Fally Ipupa ametangaza kwamba katika sehemu ya makazi yake Africa, anahitaji kuja kuishi Tanzania pia na mpango huo ameufikiria kuanzia mwakani.

Kwenye exclusive interview na AMPLIFAYA ya CLOUDS FM, Fally Ipupa ambae ni staa kwenye muziki Africa amesema mipango yake ya 2013 ni pamoja na kununua au kujenga nyumba na kuishi Tanzania.

Kwa sasa anaishi Congo ambako ndio kwao, ana miliki nyumba Paris Ufaransa pia ambako ameanza kuishi miaka 7 iliyopita, na baada ya kuvutiwa na Tanzania, Fally ameamua Tanzania iwe sehemu ya makazi yake pia na hiyo itakua Dar es salaam.

MWARICK JAPHET MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

No comments:

Post a Comment