Timbwili
I zito limeibuka baada ya mwanaume aliyetajwa kwa jina moja la Samora
kumnasa ‘live’ mkewe Hadija akimsaliti kwa kuvunja amri ya sita na
hawara ndani ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, tena kwenye chumba chao..
Habari kutoka chanzo cha uhakika kilitonya kuwa Samora na Hadija ni
wanandoa waliooana Bomani pale Magomeni, Dar, mwaka 2009 na katika ndoa
yao wamebahatika kupata mtoto mmoja wa kiume.
Tukio hilo la fumanizi
lilijiri maeneo ya Kinondoni-Kwamsisiri, Dar nyumbani kwa wanandoa hao,
majira ya saa 1:00 usiku, Julai 29, mwaka huu.
Habari zilieleza kuwa
mwanzoni mwa mwaka huu, ndoa ya wawili hao ilitumbukia nyongo na kuingia
kwenye mgogoro ambapo pamoja na kuweka mambo sawa, waliendelea
kukwaruzana mara kwa mara.
Ilidaiwa kuwa chanzo cha wawili hao kuhitilafiana ni kutokana na mwanaume kumtuhumu mkewe kutoa tunda nje ya ndoa.
Ikasemekana
kuwa baadaye wapambe walimfuata Samora na kumtonya kuwa mkewe amekuwa
na uhusiano wa kimapenzi na kidume mwingine nje ya ndoa yao ndiyo maana
amekuwa akimletea nyodo .Iliendelea
kudaiwa kuwa baada ya ndoa kutibuka, Samora alikuwa mnyonge na mwenye
msongo wa mawazo hivyo ikabidi aikimbie nyumba kwa muda na kwenda kwa
wazazi wake.
Ilisemekana kuwa, Samora alirejea nyumbani huku akifanya
uchunguzi wa nguvu akiwatumia majirani kumpatia taarifa kuhusu kila
mwanaume aliyeingia na kutoka nyumbani kwake yeye akiwa hayupo.
Uchunguzi wa Samora ulibaini kuwa, Hadija alikuwa ‘akibanjuka’ nje ya
ndoa na mwanaume aliyetajwa kwa jina moja la Rwekaza ambaye ni
mfanyakazi serikalini.
Habari za kina zilisema kuwa, Samora alitonywa
kwamba jamaa alikuwa akitimba na gari aina ya Suzuki Swift 1.3 na siku
nyingine alikuwa akilala hadi asubuhi bila tone la soni kuwa Hadija ni
mke wa mtu.
Baada ya kupata uhakika huo ndipo Samora akajipanga kwa
kuwatafuta vijana wa mtaani ili Rwekaza atakapofika nyumbani hapo kulala
na mkewe wamvamie na kumfanyizia.
Bila kufahamu kuwa anasubiriwa kwa
hamu majira yaa saa 1:00 usiku, Rwekaza huyooo, akatinga nyumbani hapo
na moja kwa moja akafikia chumbani kama kawaida yake.
Wakiwa
chumbani, ilidaiwa kuwa waliendelea na mambo yao huku Rwekaza akiwa
tumbo wazi na suruali yake amefungua zipu huku Hadija akiwa amesaula na
kubaki na ‘kufuli’, kisha akajifunga khanga moja.
Katika fumanizi
hilo, Samora alitinga chumbani humo akiwa ameambatana na kundi la vijana
kibao ambao walikuwa na lengo moja tu, kumfanyia kitu mbaya Rwekaza.
Wakiwa
chumbani, kuliibuka bonge la timbwili baada ya Samora kumshuhudia
mwenza wake aliyekula kiapo cha kutotengana naye akisaliti ‘laivu’ penzi
lao.
Baada ya kuona machafuko makubwa ya hali ya hewa chumbani,
mwanahabari wetu aliwataarifa polisi katika Kituo cha Kwamsisiri ambao
walifika maeneo hayo na kufanya kazi kubwa na nzuri ya kuepusha balaa au
mauaji kwa kuwa Samora alikuwa na hasira kali.
Ili kuthibitisha kuwa
ni mkewe wa ndoa, Samora alizama kabatini na kuchomoa cheti cha ndoa na
picha walizopiga siku ya ndoa yao zikiwaonesha wakiwa na tabasamu la
‘mimi na wewe milele’ kabla ya shetani ‘kufanya yake’ kwenye unganiko
lao.
Kwa mujibu wa majirani, tukio hilo liliwasikitisha wengi huku
wakiamini kabisa kuwa ni nadra matukio ya mafumanizi kutokea katika
kipindi cha mfungo.
“Jamani hata Mwezi Mtukufu? Ni aibu sana kwa mke
kuingiza mwanaume mwingine kwenye chumba cha mumewe. Kweli hili fumanizi
ni kiboko,” alisikika mmoja wa majirani hao walioshuhudia tukio hilo
muda mfupi baada ya kufuturu.
Source: Global publisher
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment