Friday, August 2, 2013

AIBU NDANI YA MWEZI MTUKUFU: MKE AFUMANIWA AKIGAWA URODA CHUMBANI KWA MUMEWE


clip_image001Timbwili I zito limeibuka baada ya mwanaume aliyetajwa kwa jina moja la Samora kumnasa ‘live’ mkewe Hadija akimsaliti kwa kuvunja amri ya sita  na hawara ndani ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, tena kwenye chumba chao.. Habari kutoka chanzo cha uhakika kilitonya kuwa Samora na Hadija ni wanandoa waliooana Bomani pale Magomeni, Dar, mwaka 2009 na katika ndoa yao wamebahatika kupata mtoto mmoja wa kiume.
Tukio hilo la fumanizi lilijiri maeneo ya Kinondoni-Kwamsisiri, Dar nyumbani kwa wanandoa hao, majira ya saa 1:00 usiku, Julai 29, mwaka huu.
Habari zilieleza kuwa mwanzoni mwa mwaka huu, ndoa ya wawili hao ilitumbukia nyongo na kuingia kwenye mgogoro ambapo pamoja na kuweka mambo sawa, waliendelea kukwaruzana mara kwa mara.
Ilidaiwa kuwa chanzo cha wawili hao kuhitilafiana ni kutokana na mwanaume kumtuhumu mkewe kutoa tunda nje ya ndoa.
Ikasemekana kuwa baadaye wapambe walimfuata Samora na kumtonya kuwa mkewe amekuwa na uhusiano wa kimapenzi na kidume mwingine nje ya ndoa yao ndiyo maana amekuwa akimletea nyodo .
clip_image001[6]
Iliendelea kudaiwa kuwa baada ya ndoa kutibuka, Samora alikuwa mnyonge na mwenye msongo wa mawazo hivyo ikabidi aikimbie nyumba kwa muda na kwenda kwa wazazi wake.
Ilisemekana kuwa, Samora alirejea nyumbani huku akifanya uchunguzi wa nguvu akiwatumia majirani kumpatia taarifa kuhusu kila mwanaume aliyeingia na kutoka nyumbani kwake yeye akiwa hayupo.
Uchunguzi wa Samora ulibaini kuwa, Hadija alikuwa ‘akibanjuka’ nje ya ndoa na mwanaume aliyetajwa kwa jina moja la Rwekaza ambaye ni mfanyakazi serikalini.
Habari za kina zilisema kuwa, Samora alitonywa kwamba jamaa alikuwa akitimba na gari aina ya Suzuki Swift 1.3 na siku nyingine alikuwa akilala hadi asubuhi bila tone la soni kuwa Hadija ni mke wa mtu.
Baada ya kupata uhakika huo ndipo Samora akajipanga kwa kuwatafuta vijana wa mtaani ili Rwekaza atakapofika nyumbani hapo kulala na mkewe wamvamie na kumfanyizia.
Bila kufahamu kuwa anasubiriwa kwa hamu majira yaa saa 1:00 usiku, Rwekaza huyooo, akatinga nyumbani hapo na moja kwa moja akafikia chumbani kama kawaida yake.
Wakiwa chumbani, ilidaiwa kuwa waliendelea na mambo yao huku Rwekaza akiwa tumbo wazi na suruali yake amefungua zipu huku Hadija akiwa amesaula na kubaki na ‘kufuli’, kisha akajifunga khanga moja.
Katika fumanizi hilo, Samora alitinga chumbani humo akiwa ameambatana na kundi la vijana kibao ambao walikuwa na lengo moja tu, kumfanyia kitu mbaya Rwekaza.
Wakiwa chumbani, kuliibuka bonge la timbwili baada ya Samora kumshuhudia mwenza wake aliyekula kiapo cha kutotengana naye akisaliti ‘laivu’ penzi lao.
Baada ya kuona machafuko makubwa ya hali ya hewa chumbani, mwanahabari wetu aliwataarifa polisi katika Kituo cha Kwamsisiri ambao walifika maeneo hayo na kufanya kazi kubwa na nzuri ya kuepusha balaa au mauaji kwa kuwa Samora alikuwa na hasira kali.
Ili kuthibitisha kuwa ni mkewe wa ndoa, Samora alizama kabatini na kuchomoa cheti cha ndoa na picha walizopiga siku ya ndoa yao zikiwaonesha wakiwa na tabasamu la ‘mimi na wewe milele’ kabla ya shetani ‘kufanya yake’ kwenye unganiko lao.
Kwa mujibu wa majirani, tukio hilo liliwasikitisha wengi huku wakiamini kabisa kuwa ni nadra matukio ya mafumanizi kutokea katika kipindi cha mfungo.
“Jamani hata Mwezi Mtukufu? Ni aibu sana kwa mke kuingiza mwanaume mwingine kwenye chumba cha mumewe. Kweli hili fumanizi ni kiboko,” alisikika mmoja wa majirani hao walioshuhudia tukio hilo muda mfupi baada ya kufuturu.
Source: Global publisher
MWARICK JAPHET MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

PINDA HANA KESI YA KUJIBU-DPP


clip_image001WAZIRI MKUU-MIZENGO PINDA.
 
MKURUGENZI wa Mashitaka (DPP), Eliezer Feleshi, amesema haoni mantiki yoyote au uhalali wa Kituo cha Haki za Binadamu (LHRC), kumshitaki Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
 
Alisema hayo jana wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari, baada ya kufungwa kwa mkutano wa siku tatu wa mawakili wa Serikali wafawidhi, wakuu wa upelelezi wa mikoa na vikosi vingine vya Polisi Alisema kauli aliyotoa Pinda bungeni, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Kilwa Kaskazini, Murtaza Mangungu kuhusu Polisi kutumia nguvu kwa wananchi, ililenga wanaokaidi kukamatwa na kufikishwa mbele ya sheria na si kupiga na kuua kama ilivyotafsiriwa na wengi.
 
“Sijapata taarifa kwa maandishi juu ya azma ya kumshitaki Waziri Mkuu, lakini Pinda hajavunja sheria kwa kauli yake aliyotoa,” alisema.
 
Alisema kwa jinsi alivyosikia maelezo ya Waziri Mkuu bungeni, kama LHRC wanamshitaki kwa jinai Waziri Mkuu, haoni uhalali wa mashitaka hayo. 
 
Usahihi wa Pinda Alisema Waziri Mkuu alieleza hatua zinazochukuliwa dhidi ya mvunja sheria, na kufafanua kuwa Mtanzania yeyote ana haki kwa mujibu wa sheria, lakini pia ana wajibu, ndiyo maana vipo vyombo na kila chombo kimepewa mamlaka na wajibu wa kutekeleza.
 
Alifafanua, kwamba kilichoongelewa ni dhana ya mkusanyiko ambayo ni haki kwa mujibu wa Katiba, ikiwemo uhuru wa kukutana, kutoa mawazo na kufanya mawasiliano.
 
Hata hivyo, alikumbusha kuwa Sheria ya Jeshi la Polisi, inasema ili mkusanyiko ufanyike, lazima taarifa itolewe kwa kiongozi wa Polisi wa eneo husika.
 
Sheria hiyo inasema, kama mkusanyiko una nia ya kutenda kosa na ikafanyika hivyo, kuna chombo kilichopewa dhamana ya kuhakikisha mkusanyiko haramu unatawanyika na sheria hiyo inaruhusu Polisi kutawanya mkusanyiko haramu.
 
“Unatarajia nini kama kuna watu wanafanya fujo na polisi wana mamlaka ya kuwakamata waliofanya fujo?” Alihoji Feleshi na kuongeza kuwa dhana ya matumizi ya nguvu ni ya kisheria pia.
 
kwa upande wake Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema,  alisema utaratibu wa Polisi kulazimika kutumia nguvu upo. Aliutaja utaratibu huo kwamba unatumika hasa katika mikusanyiko isiyotakiwa, ambapo Polisi hulazimika kutoa tangazo la angalizo mara kadhaa kutaka watu watawanyike.
 
“Tangazo linapotolewa naPolisi kwa kutumia kipaza sauti husema, tawanyikeni, tawanyikeni na kusisitiza hivyo mara kadhaa, hapo wanaopaswa kutawanyika wakikaidi, nguvu hutumika ingawa inaweza isiwe ya kupiga risasi, pengine virungu, yote hiyo si kupiga?
 
“Risasi ni kitu cha mwisho, labda uwe unashambuliwa wewe (polisi), hata ikiwa hivyo, ukipiga risasi kuna maeneo ya kupiga, si kichwani, polisi wana mafunzo ya kupiga maeneo ya miguuni, hivyo kutumia nguvu kwa polisi kupo,” alisema Jaji Werema.

MWARICK JAPHET MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

BAADA YA KUWEKA REKODI YA KWANZA YA KULIA BUNGENI, HII NI REKOD NYINGINE KWA WAZIRI MKUU


clip_image001

















HATIMAYE PINDA KUWA WA KWANZA KUBURUZWA MAHAKAMANI ...Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimemfungulia mashtaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kutokana na kauli yake aliyoitoa bungeni hivi karibuni kwamba wanaokaidi maagizo ya dola wapigwe.
Hatua hiyo ya LHRC imepingwa vikali na Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP), Dk Elieza Feleshi akisema hakuna uhalali wa mashtaka yoyote dhidi ya kiongozi huyo sababu kauli ya Pinda kuwa pigeni haikuwa piga ua.
Mkurugenzi wa LHRC, Dk Hellen Kijo Bisimba alifungua mashtaka hayo katika Mahakama Kuu jana akisema kuwa wanamshtaki Waziri Mkuu kwa maelezo kuwa amekiuka kifungu cha Katiba Ibara 13 (1). Pinda ametajwa kuwa ni mdaiwa wa kwanza katika kesi hiyo namba 24.
Mkurugenzi wa Maboresho na Utetezi wa LHRC, Harold Sungusia alisema jana kwamba, mwingine aliyeunganishwa katika kesi hiyo ya kikatiba iliyofunguliwa na LHRC na Chama cha Wanasheria Tanzania (TLS) ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema.
Alisema katika kesi hiyo, kuna jopo la mawakili wasiopungua 20 na kwamba wamepata saini za wananchi 2,029 wanaopinga kauli hiyo ya Pinda na kuunga mkono kufunguliwa kwa kesi hiyo.
Mjumbe wa Bodi ya LHRC, Wakili Dk Ringo Tenga alisema katika kesi hiyo wameangalia zaidi sheria na hasa haki za msingi za binadamu na kwamba kauli hiyo ya Waziri Mkuu Pinda inahatarisha haki hizo.
Kauli yenyewe
Wakati wa Kipindi cha Maswali ya Papo kwa Papo kwa Waziri Mkuu bungeni, Juni 19, mwaka huu, Waziri Mkuu akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Kilwa Kaskazini (CCM), Murtaza Mangungu aliyeuliza: “Serikali ipo tayari kiasi gani kubainisha na kuchukua hatua stahiki, badala ya kusakama makundi fulani, tujue chanzo halisi cha vurugu hizi na matatizo haya na jinsi gani vyombo vya dola vinavyoshughulikia kwa sababu yapo malalamiko katika baadhi ya maeneo kama Mtwara kwamba wananchi wanapigwa na vyombo vya dola?”
Waziri Mkuu alijibu: “Ni lilelile nililosema... mwishowe unaona anasema vyombo vya dola vinapiga watu. Ukifanya fujo, umeambiwa usifanye hiki, ukaamua kukaidi, utapigwa tu... hamna namna nyingine, maana wote tukubaliane kwamba nchi hii tunaiendesha kwa misingi ya kisheria.
“Sasa kama wewe umekaidi, hutaki unaona kwamba ni imara zaidi... wewe ndiyo jeuri zaidi watakupiga tu.... Mimi nasema muwapige tu, kwa sababu hakuna namna nyingine... maana tumechoka.” Kesi hiyo itakayosikilizwa na majaji watatu, haina uhusiano na kesi nyingine ambazo wajibu maombi hupewa siku 90 kujibu hoja zilizowasilishwa. Kesi hiyo imefunguliwa kwa mujibu wa Katiba Sura ya Tatu.
Akizungumza juzi kwenye Viwanja vya Bunge mjini Dodoma baada ya kufungwa kwa Warsha ya Wapelelezi na Waendesha Mashtaka wa Serikali ngazi ya mikoa, Dk Feleshi alisema hakuna uhalali wa mashtaka hayo kwa sababu kauli ya Pinda kuwa pigeni haikuwa piga ua.
“Hii haikuwa kuchochea apige watu, alichosema ni kupiga wale wasiotaka kutekeleza amri halali na zaidi alisema piga lakini si kupiga na kuua,” alisema.
Mkutano huo uliendeshwa chini ya ulinzi mkali huku kukiwa na udhibiti wa kuvuja siri kwa kiwango cha juu. Pamoja na mambo mengine, ulikuwa ukijadili mbinu za kisasa katika kuendesha kesi pamoja na kujiuliza sababu za Serikali kushindwa katika kesi nyingi.
“Kwa sababu lile neno kupiga ni lazima lipewe maana pana huwezi kumpiga tu mtu hivihivi ambaye hakuvunja sheria lakini nilivyoelewa, ilikuwa ni hivyo, ni sawa na mtu ambaye anamshambulia askari,” alisema Dk Feleshi.
Alisema kuna sheria ya kutumia nguvu pale ambako kuna mkusanyiko usiokuwa wa halali pindi raia wanapokaidi kutawanyika kwa hiari hivyo hakuna shaka kauli ya Waziri Mkuu ililenga hivyo.
 
Hata hivyo, alisema hajapata taarifa za LHRC kumshtaki Waziri Mkuu kimaandishi na kwamba akizipata atatoa ufafanuzi baada ya kuona lengo la mashtaka. 

Msimamo 
Akizungumza baada ya kufungua mashtaka hayo, Dk Bisimba alisema Waziri Mkuu anaweza kushtakiwa kwa kuwa alizungumza kwa nafasi yake ya Waziri Mkuu na si mbunge na kusisitiza kwamba hakuna aliye juu ya sheria na kudai kwamba kauli hiyo ni kinyume cha Katiba.
Alisema kuwa kila anayevunja Katiba lazima ashughulikiwe kisheria na kwamba mahali pake ni mahakamani tu. Alisema kwa mujibu wa hati hiyo ya madai, kauli na amri kama hizo zinapotolewa na kiongozi mwenye hadhi kama ya mdaiwa wa kwanza (Waziri Mkuu) huchukuliwa kama sheria inayopaswa kutekelezwa na wakala wa utekelezaji wa sheria kama vile polisi. Wadai hao wanadai kuwa kwa ufahamu wao polisi wanaweza kuchukulia kauli hiyo kama amri halali kutoka kwa mkubwa wao na hivyo kuwapiga na kuwatesa watu wasio na hatia, kinyume cha Katiba.
 
Pia wanadai wanatambua kuwa Ibara ya 100 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatoa kinga kwa wabunge na uhuru wa maoni bungeni. Hata hivyo, wanatambua kuwa Ibara ya 100 (2) ya Katiba hiyo inawawajibisha wabunge wote chini ya masharti ya Katiba na kwamba kauli aliyoitoa Waziri Mkuu Pinda inakiuka Ibara ya 12(12).
Hivyo wanaiomba Mahakama hiyo itamke kuwa kauli na amri hiyo aliyoitoa Pinda inavunja Katiba.
Mkurugenzi wa taasisi inayofuatilia Mwenendo wa Bunge (Watch), Marcos Albania alidai kwamba wamegundua kuwa kauli hiyo ya Pinda ni moja kati ya matamko makubwa yanayovunja Katiba.
Alisema mbali na shtaka hilo, kuna la pili dhidi ya Waziri Mkuu Pinda, ambalo hawajalifikisha mahakamani ambalo pia linatokana na kauli hiyo aliyoitoa bungeni kwamba: “Sasa wamechoka.”
 
SOURCE: CHAHALI.COM
MWARICK JAPHET MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

MCHUMBA WAKE ROSE NDAUKA AFAFANUA FUMANIZI LA ROSE KUNASWA GEST


clip_image001















BAADA ya msanii wa filamu nchini Rose Ndauka kuripotiwa kufumaniwa akiingia gesti na msanii chipukizi wa muziki wa bongo fleva Nassoro Ayoub 'Dogo Nasry' huku akiwa amevaa baibui kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani,  mumewake mtaarajiwa Maliki Bandawe 'Chiwaman' amjia juu msanii huyo kwa madai ya kumchafua mpenzi wake.
Akizungumza jijini Dar es Salaam Chiwaman aliweka wazi kuwa msanii huyo Nasry ambaye alimuomba Rose aweze kushiriki kwenye video yake, walishindwa kufikia maamuzi kutokana na kiwango cha malipo kuwa madogo, na badala yake msanii huyo alimuomba wapige picha kama ukumbusho.
Alisema kuwa kitendo hicho cha kupiga picha na msanii huyo wakati wapo katika mazungumzo ya awali ya kukubaliana malipo ndizo picha alizotumia msanii huyo na kudai kuwa alikuwa naye nyumba ya wageni kitendo ambacho si cha kweli.
"Hawa wasanii wachanga wanatafuta umaarufu vibaya kwa kuwachafua watu, ilikuwa amemuomba Rose ashiriki kwenye video yake na ndipo walipokutana kwa ajili ya mazungumzo hayo na alikuwa na mdogo wangu sasa hapo masuala ya gesti yametokea wapi" alisema Maliki.
Aliongezea kuwa "kama nilikuwa sijui hicho kitu na kwa jinsi mambo yalivyokuwa ningeweza kumuacha mchumba wangu ninayempenda kwa dhati, ila msanii huyo alichokifanya siyo jambo sahihi, kwani alimuomba apige naye picha na Rose alikubali huku bila kujua nia yake ".
Maliki alisema kuwa huyo msanii anatafuta umaarufu kwa kuchafua majina ya watu wengine, kitu ambacho hakina mashiko kwenye jamii.
MWARICK JAPHET MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

Thursday, August 1, 2013

Wakazi Magu watumia maji ya madimbwi


Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Magu, Naomi Nko
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Magu, Naomi Nko

Zaidi ya wakazi elfu 25 wa mji mdogo wa Magu mkoani Mwanza wanalazimika kutumia maji yaliyotuama kwenye madimbwi kufuatia uhaba mkubwa wa maji unaoukabili mji huo kwa kipindi cha zaidi ya miezi mitatu sasa.
 
Baadhi ya wakazi wa mji huo wameeleza kuwa tatizo hilo limesababisha watumie muda wao mwingi kuyatafuta maji ambayo wakati mwingine sio safi wala salama kwa afya zao badala ya kufanya kazi za kuwaingizia kipato na hivyo kuwaweka kwenye hatari ya kukumbwa na magonjwa ya milipuko.

Adha ya ukosefu wa maji safi na salama katika mji wa Magu mkoani mwanza inawalazimu wakazi wa mji huo kutembea umbali wa zaidi ya kilometa tano ili angalau waweze kuambulia ndoo moja ya maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani kutoka katika vijiji jirani.

Wapo wananchi wa magu wanaodiriki kujitosa katika madimbwi ambayo yana kila  ishara ya kukosa hadhi ya kutumiwa na binadamu kutokana na maji yake kutuama.
Suala la upatikanaji usioridhisha wa maji katika mji wa Magu pia limeibua mjadala katika kikao cha baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya hiyo.

Hofu ya kuibuka kwa magonjwa ya milipuko sasa ni tele miongoni mwa baadhi ya madiwani wa magu.

mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya magu NAOMI NKO amekiri kuwepo kwa tatizo hilo.

Amicus Butunga, TBC Mwanza.
MWARICK JAPHET MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.