STAA wa filamu na muziki Bongo, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ amekiri kuwa
katika wakati mgumu kutokana na kukabwa na mashetani usiku na
kumsababishia maumivu makali ya mwili hadi kuhisi kufa.
Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’.
Hivi
karibuni Jini Kabula alipotea kwenye ulimwengu wa mastaa jijini Dar
hivyo paparazi wetu alipomtafuta na alipopatikana ndipo alipobaini hali
yake ni tete kiafya.
Akizungumza
na mwanahabari wetu wikiendi iliyopita, Jini Kabula alisema kwa muda
mrefu sasa amekuwa mtu wa kuumwaumwa na mwili kukosa nguvu ambapo
alishapima vipimo vyote lakini aligundulika kuwa na malaria, akatumia
dozi na kuimaliza lakini hali bado siyo nzuri.
Huku
akiwa amedhoofu mwili, Jini Kabula alisema kila ikifika usiku wa manane
akiwa amelala huwa anakabwa na mtu ambaye hamuoni, hali inayomfanya
ashindwe kupumua huku mwili ukikosa nguvu na kuuma kupindukia.
“Nahisi
kabisa nakufa kwa jinsi ninavyojisikia mwilini, natamani hata usiku
usiingie kwa sababu mateso ninayopata ya kukabwa ni makubwa, wakati
mwingine nakesha nikiangalia muvi kwa kuhofia nikilala tu lazima
nikabwe.
“Hata
rafiki zangu nimeshawaaga na kuwaambia kuwa muda wowote wakisikia
nimekufa wasishangae kwa sababu naumwa ila ninayemhurumia ni mwanangu,
jamani nitamuacha nani bado mdogo maskini wa Mungu sijui ni shetani gani
ametukumba wasanii,” alisema Jini Kabula kwa masikitiko.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment