MAKALA NA TRIM SALEEM (Trim Saleem)
Suala
la usambazaji wa films za kitanzania ni moja ya vitu vinavyolalamikiwa
sana kuwa limejaa upendeleo kwa wasanii wenye majina makubwa na wachanga
kupuuzwa, vile vile hata hao wenye majina nao wananyonywa kama kawa
licha ya
kwamba
uharamia nao unaonekana kuota mapembe bila juhudi thabiti za
kuuteketeza ingawa upo duniani kote. ila inatakiwa wasanii kuungana na
pia kuishinikiza serikali ili ijenge majumba ya cinema maana haya huwa
ndiyo chanzo kikubwa cha mapato ya films na hata kuamuliwa kama film ni
hit or flop kutokana na kuwa wazi zaidi hasa katika suala la uuzaji wa
tiketi kuliko uuzaji wa dvd, vcd, net au tv broadcast ingawa vyote hivi
ni vyanzo vikuu vya mapato ila majumba ya sinema ndo hutegemewa zaidi.
Hapa
nchini kuna majumba machache ya sinema lakini ukiyaangalia sana ni kama
hayapo Tanzania maana mara nyingi yanaonyesha films za hollywood na
bollywood/ india ingawa pia watengenezaji wa films za kitanzania
wanaonekana kukosa ufahamu au weledi wa kutumia majumba haya, ila ikiwa
wasanii wataungana na kufanya harambee za kukusanya pesa kwa kuanzia
hata na majumba 2 au 3 kwa msaada wa serikali na wao wenyewe hili
linawezekana na ni moja ya njia ya kuwashikisha adabu baadhi ya
wasambazaji waliojaa unyonyaji huku wakikosa ubunifu wa namna ya
kutangaza films ambazo sio za kimapenzi ili ziuzike yaani wasambazaji
hawa ni kama hawana nia ya dhati ili films zetu zifike mbali ila mapenzi
tu ndio films! suala hili linawezekana ikiwa wasanii wataacha kufanya
sherehe au party zisizo na kichwa wala miguu kila siku na kuchangishana
pesa nyingi kwenye harusi halafu ndoa zenyewe nyingi hazidumu zikiwa na
lengo la kujionyesha tu mbele za watu ,na ikumbukwe kuwa kuna
wafanyabiashara wazalendo wengi tu ambao wanaweza kuwa interested na
hata kuwekeza kwenye project kama hizi ikiwa wataona wasanii wenyewe
wana maono ya mbali ili kufanikiwa, na ikiwa hili litatiliwa maanani
basi hata ndani ya miaka 5 ijayo tayari njia nzuri itakuwa ishaanza
kuonekana kuliko hali ilivyo sasa msambazaji ndio huamua kuwa film
imeuza au haijauza hata kabla haijaingia sokoni wakati wa kuliamua hili
ni wanunuzi au mashabiki wenyewe baada ya kuona film sokoni .
Ukweli ni
kuwa Tanzania ina nafasi kubwa sana ya kufanya vizuri kuliko hata
Nigeria maana Nigeria yenyewe imeanza muda kidogo ila kuna films nyingi
ukiziangalia zina makosa kibao kama za kibongo na hii ndiyo sababu licha
ya Nigeria kuzalisha utiriri wa films kibao kila siku lakini nyingi
zinashindwa kushindana na chache kutoka south Afrika ambazo zinatamba
mpaka nje ya bara la afrika wakati za Nigeria nyingi zimeishia barani
afrika. Ikiwa tutaendelea kutegemea uuzaji wa dvd na vcd kama chanzo
kikuu cha mapato wakati india na hollywood huwa chanzo kingine baada ya
majumba ya cinema hatuwezi kuwa mabilionea kupitia films hata siku moja
na amin usiamini majumba ya sinema yakijengwa wasambazaji watakuwa na
nidhamu kwa maproducer na hata kuwashobokea ili wafanye biashara kuliko
sasa, pia haya majumba machache yaliyopo yataacha kasumba zao na
kugeukia films za kitanzania. ila hili litawezekani kwa asilimia kubwa
huku tukiwa tunazidi kuziboresha films zetu ili huko kwenye cinemas
tusije kuwachosha watu kama ilivyo sasa mtu hata nyumbani kwake film ya
kibongo inamboa . suala la kuwa sisi ndo kwanza tumeanza lisiwe kigezo
cha sisi kuchukuwa miaka kibao ili kufika mbali maana walioanza zamani
mazingira yao yalikuwa magumu kuliko ulimwengu wa leo. pichani ni THEA 1
wa waigizaji wetu wachache wenye viipaji halisi ambavyo vinatakiwa ili
kuifikisha tasnia hii anga za kimataifa
via:bongofilmdatabase.blogspot.com
No comments:
Post a Comment