Tuesday, November 27, 2012

TAARIFA KAMILIKUHUSU KIFO CHASHAROMILLIONEA.



Taarifa kuhusu kifo cha Msanii wa
maigizo na Mziki wa Bongo fleva
kufariki zimasamba nchi nzima
masaa machache yaliopita.
Kwa mujibu wa Sam Misago.Com ni
kwamba amepata uthibitisho
kutoka kwa diwani Makame Seif
ambaye ni rafiki yake wa karibu
sana wa Marehemu Hussen
Ramadhani Mkiete maarufu kama
Sharo Millionea amepata ajali mida
ya saa mbili eneo la maguzoni
Tanga na amefariki dunia papo
hapo. Polisi wametambua ni Sharo
Millionea kwa vitambulisho vyake
na picha moja ya passport aliokuwa
nayo mfukoni ambavyo kwa sasa
viko na polisi.
Diwani huyu amemfahamisha
mwandishi kuwa Sharo Millionea
ameumia vibaya sana kichwani,
kifuani na kwenye mikono. Pia
Mjomba wa marehemu
amethibitisha kuwa Sharo Millionea
atazikwa Tanga na asubuhi ya leo
ratiba ya msiba itatolewa. Ndugu
na marafiki wa Sharo wameanza
kwenda hospitalini baada tu ya
taarifa hizi kuwafikia. Familia ya
Sharo imeshafika Hospitali ya Teule
ya Tanga.
Tunamuombea Ndugu yetu SHARO
MILLIONEA Apumzike Kwa
Amani....


MWARICK JAPHET MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

No comments:

Post a Comment