Waziri wa maliasili za Utalii Balozi Khamis Kagasheki akihojiwa na
kituo cha Televisheni ya Taifa TBC mara baada ya kutembelea mabanda ya
makampuni ya Tanzania yanayoshiriki katika maonyesho ya Utalii ya World
Travel Market yanayoandaliwa na kufanyika katika eneo la Excell jijini
London nchini Uingereza, yakishirikisha makampuni mbalimbali ya utalii
kutoka pande zote za dunia, Mwaka huu Tanzania inawakilishwa na
makampuni zaidi ya 55 yakiwa chini ya Bodi ya Utalii nchini Tanzania
(TTB).
Waziri Balozi Kagasheki amesifushiriki wa makampuni ya Tanzania
katika maonyesho hayo lakini amesisitiza kwamba makampuni hayo yaongeze
juhudi za kutangaza utalii wa Tanzania mpaka kufikisha lengo la idadi ya
watalii milioni moja kila mwaka, ameongeza kwamba kuna haja ya kuongeza
vitanda zaidi nchini Tanzania ili kuongeza idadi ya watalii
watakaotembelea katika mbuga zetu na kufanya utalii kuka zaidi,
Maonyesho hayo yatazinduliwa rasmi kesho.
Fullshangweblo iko jijini London nchini Uingereza ikikumuvuzishia matukio haya moja kwa moja kutoka katika maeneo ya Excell ambako ndiko maonyesho hayo yanafanyika.
PICHA NA FULLSHANGWEBLOG.COM
Waziri
aliasili na Utalii wa Balozi Khamis Kagasheki akisalimiana na Issa
Ahmed Othman Mshauri wa Rais masuala ya Utalii Zanzibar wakati
alipotembelea banda la Tanzania katika maonyesho ya utalii ya (WTM)
jijini London leo nchini Uingereza
Waziri Balozi Khamis Kagasheki akizungumza na Leila Ansel Mkuu wa
mauzo na masoko kampuni ya Tanzania Zara Adventures wakati alipotembelea
katika banda hilo leo kwenye maonyesho ya utalii ya WTM nchini
Uingereza.
Yvone Baldwin Afisa mauzo wa kampuni ya ndege ya Precision Air
akimkabidhi zawadi Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mh. Peter
Kallaghe mara baada ya kutembelea banda hilo leo akiongozana na Waziri
wa Maliasili Balozi Khamis Kagasheki.
Waziri wa Maliasili Balozi Khamis Kagasheki akizungumza na Rashid
Adam Meneja Masoko wa Tanzania Zara Adventures wakati alipotembelea
maonyesho ya Utalii ya WTM katika banda la Tanzania leo jijini London,
wa pili kutoka kushoto ni Mh. Peter Kallaghe Balozi wa Tanzania nchini
Uingereza na katikati ni mama Balozi.
Waziri Balozi Khamis Kagasheki akizungumza na Laura Meneja wa
Maendeleo ya Biashara kampuni ya Laitolya Tours & Safari Ltd kushoto
wakati alipotembelea banda la kampuni hiyo kwenye maonyesho ya WTM leo,
kulia ni Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Devotha
Mdachi.
Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Devotha Mdachi
akiwahudumia watu mbalimbali waliotembelea katika banda la Tanzania leo
katika maonyesho ya Utalii ya WTM jijini London Uingereza
Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii ya Tanzania TTB Bw. Geofrey Meena
akiwa katika picha ya pamoja na wakurugenzi wa African Environments
Richard Beatty na Janice Beatty katika maonyesho hayo.
Leila Ansel Mkuu wa mauzo na masoko kampuni ya Tanzania Zara
Adventures akizungumza na mmoja wa wageni waliotembelea katika banda la
kampuni hiyo katikati ni Rashid Adam Meneja Masoko wa Tanzania Zara
Adventures.
Mh.
Peter Kallaghe Balozi wa Tanzania nchini Uingereza akizungumza na mdau
Juma Mabakila wakati akitembelea banda la Tanzania kwenye maonyesho ya
WTM
Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii ya Tanzania TTB Bw. Geofrey Meena
akiwasikiliza wageni mbalimbali waliofika katika banda la Tanzania
katika maonyesho hayo leo.
Balozi Khamis Kagasheki Waziri wa Maliasili Utalii wa pili
kutoka kulia akizungumza na Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii
Tanzania TTB Devotha Mdachi mara baada ya kutembelea Banda la Tanzania
katika maonyesho ya Utalii ya WTM nchini Uingereza , kulia ni Mh. Peter
Kallaghe Balozi wa Tanzania nchini Uingereza na katikati ni Mama
Balozi.
Mmoja wa washiriki kutoka kampuni ya Africa Adventure akihojiwa na
kituo cha televisheni cha TBC katika maonyesho ya Utalii ya WTM
yanayofanyika jijini London nchini Uingereza.
Waziri Balozi Khamis Kagasheki akizungumza na wafanyakazi wa Mamlaka
ya hifadhi ya Ngorongoro wakati alipotembelea maonesho hayo kushoto ni
Meneja wa Masoko wa Bodi ya Utalii nchini TTB.
Washiriki mbalimbali wakiwa katika banda la Tanzania wakipokea wageni
mbalimbali wanaotemelea kwenye banda hilo kwa ajili ya kupata taarifa
mbalimbali kuhusu utalii wa Tanzania.
No comments:
Post a Comment