Katibu
wa Jukwaa la Wahariri Bw. Nevil Meena akiongea kwa uchungu mbele ya
wanahabari wenzake ambapo pamoja na maazimio mengine wametangaza
kutoandika habari zinazohusiana na jeshi la polisi kwa siku 40.
Na Datus Boniface.
Wakiwa
katika nyuso za huzuni kubwa ya kuondokewa na mwenzao ambaye aliuawa
kwa kupigwa na bomu, kundi la Wanahabari wao wamemtimua Waziri wa Mambo
ya Ndani Mh. Emmanuel Nchimbi kutokana na kuwaingilia kwenye maandamano
yao.
Wanahabari
kote nchini leo wamefanya maandamano ya amani kwa lengo la Kulaani
mauaji ya mwenzao wa kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Daudi
Mwangosi.
Kufukuzwa
na kuzomewa kwa Waziri Nchimbi kumekuja baada ya kugundulika kuwa
ameingilia maandamano kwa lengo la kuyapokea bila kupewa mwaliko.
Kutokana
na zomea zomea hiyo ya wanahabari hao dhidi ya Waziri Nchimbi hali
ilionekana kuwa si shwari na kupelekea waziri huyo kuondolewa na rais wa
UTPC Keneth Simbaya na viongozi wengine wakiwemo askari polisi.
Akizungumza
na kundi la waandishi Katibu wa Jukwaa la Jukwaa la wahariri (TEF)
Neville Meena amesema “Hatuna ugomvi na Waziri Nchimbi kwani ni
mwenzetu, rafiki yetu, ila leo hana vazi la msiba”
Mara
baada ya kuondoka bila kupenda Waziri Nchimbi, hali ya utulivu ilikuwa
kama kawaida na shughuli zingine ziliendelea kama ilivyopangwa.
VIA . MO BLOG
No comments:
Post a Comment