Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Nape Nnauye.
-Yataka usichukue muda mrefu
-Yataka ubaini pia mazingira ya kuuawa mwandishi huyo.
-Yatoa pole kwa wafiwa, Wanahabari na Watanzania.
CCM
imevitaka vyombo na tume zilizoundwa kuhusiana na kifo cha mwandishi wa
habari Daudi Mwangosi, vichunguze kwa umakini na weledi mkubwa ili
kubaini kila kitu ikiwemo chanzo cha vurugu zilizotokea na mazingira
yaliyosabaisha kipigo hadi kufa mwandishi huyo.
Aidha
imetaka uchunguzi usichukue muda mrefu ili ukweli kuhusiana na kadhia
hiyo ujulikane mapema na hatua zichukuliwe kwa kila atakayebainika kuwa
sababu au chanzo cha vurugu na kifo cha mwandishi huyo.
Aidha
imesema imepokea kwa masikitiko makubwa sana taarifa za kifo hicho na
kujeruhiwa kwa askari watatu wa Polisi wakati wa vurugu hizo na kimetoa
pole kwa wafiwa, wanahabari wote nchini na wote walioguswa na msiba huo
kwa namna moja au nyingine.
Hayo
yamesemwa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na
Uenezi, Nape Nnauye katika taarifa ya CCM kwa vyombo vya habari, leo
jijini hapa, kuhusiana na sakata la vurugu hadi kifo cha mwandishi huyo,
juzi mkoani Iringa.
“Itakumbukwa
tarehe Septemba 2, 2012 katika operesheni za CHADEMA mkoani Iringa
kulitokea vurugu zilizosababisha kuuawa kwa mwandishi wa habari
mzoefu,nDaudi Mwangosi na kujeruhiwa vibaya kwa polisi watatu wa kikosi
cha kutuliza ghasia. Chama Cha Mapinduzi kimepokea kwa masikitiko
makubwa sana taarifa za kifo hicho na kujeruhiwa kwa askari hao”, Nape
alisema katika taarifa hiyo, na kuongeza:
“CCM
inachukua nafasi hii kutoa pole kwa wafiwa, wanahabari nchini na wote
walioguswa na msiba huu kwa namna moja au nyingine na tunatoa mwito kwa
vyombo na tume mbalimbali zilizoundwa kuchunguza swala hili, vichunguze
kwa umakini na weledi mkubwa ili kubaini yote – ikiwemo chanzo cha
vurugu zilizotokea na mazingira ya kifo cha ndugu yetu”.
Alisema
CCM inasikitishwa na mfululizo wa matukio ya watu kupoteza maisha au
kujeruhiwa katika mikutano na operesheni mbalimbali zinazoendeshwa na
CHADEMA nchini hasa zile zilizofanyika kwa kukaidi amri halali za vyombo
vya ulinzi na usalama.
Alikumbusha
baadhi ya matukio hayo kuwa ni pamoja na lile la kuuawa kwa kada wa CCM
Mkoani Singida, kuuawa kwa Ally Hassan mjini Morogoro na la juzi la
kuuawa kwa Mwangosi Mjini Iringa, kujeruhiwa kwa askari polisi Iringa na
matukio mengine mengi ambayo yametokea wakati CHADEMA wakiendesha
operesheni zao mbalimbali nchini.
“Matukio
haya si mazuri kutokea kwenye shughuli za Chama cha siasa. Kwakweli ni
aibu, inayohitaji uwajibikaji,hata kama ni wa kisiasa. Inapotokea
shughuli za chama chako zinasababisha kupotea kwa maisha ya watu kila
unapozifanya na bado usitake kuwajibika, inahitaji roho ngumu na ujasiri
wa aina yake” alisema Nape katika taarifa hiyo na kuongeza;
“Inakuwa
mbaya zaidi pale vifo hivi vinaposababishwa na Chama hicho kutotii amri
halali zilizotolewa kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi inayovipa
pia uhalali vyama vya siasa kuwepo na kuendesha shughuli zake kwa
mujibu wa sheria”.
“Laiti
Chama hicho kingesubiri siku chache zilizobakia kabla ya Sensa kuisha
kabla ya kuendelea na mikutano yake ni dhahiri mauaji haya yasingetokea.
Lakini kauli za kukebehi na uamuzi wa kukaidi amri ya Jeshi la Polisi
na kusema “tupo tayari kwa lolote” ni ishara kwamba Chama hiki kiliandaa
na kujiandaa na fujo zilizotokea”, alisema Nape.
CCM
imetoa mwito kwa vyama vya siasa na wanasiasa kwa ujumla kujenga
utamaduni wa kuheshimu utawala wa sheria na kusema kwamba amani na
utulivu vilivyopo nchini ni kazi nzuri iliyojengwa kwa muda mrefu na
waasisi wa taifa la Tanzania kwa kujenga utamaduni wa kuzingatia utawala
wa sheria.
Via: Mo Blog
No comments:
Post a Comment