Wednesday, July 16, 2014
Saturday, May 31, 2014
Penzi la Kitale Aka Mkude Nsimba na Penny Lafuka Moshi..Tena Moshi Mweupeee
Juzi niliposti picha ya KITALE (Kwasasa unaweza kumuita MKUDE SIMBA)
akiwa anapigwa KISS ZITO na PENNY lenye hisia kali (Daah mtoto P hadi
akafumba macho).....Nikawaachia wadau MKOMENT..Sasa leo tena mwanadada
Penny Kupitia akaunti yake ya INSTAGRAM ametupia hii....
Sina cha ku-comment zaidi ya kukumbuka msemo wa PANAPOFUKA MOSHI....UJUE KUNA MOTO!
EXCLUSIVE PHOTO’S: Masaa 4 kabla ya kifo cha GEOGRE TYSON pamoja na gari alilopata ajali ziko hapa EXCLUSIVE PHOTO’S: Masaa 4 kabla ya kifo cha GEOGRE TYSON pamoja na gari alilopata ajali ziko hapa
Marehemu Geogre Tyson pichani hapa
alikuwa yupo kijiji cha Chilonwa Chamwino kwenye utoaji wa madawati
katika shule ya msingi Chaula iliyopo Dodoma. Baada ya kumaliza shughuli
hii huku akiwa kama producer wa The Mboni Show mauti yalimkuta majira
ya saa 12 jioni masaa 4 tu toka tuanze safari ya kurudi Dar es Salaam
maeneo fulani hivi kama unataka kukaribia GAIRO mjini.
Katika gari hilo walikuwa watu 8 ila yeye
pekee ndio aliyepoteza mauti na wengine kupata majiraha mwilini pamoja
na dereva wa gari hilo. Kwa sasa mwili wa marehemu umehifadhiwa hapa
Morogoro katika hospital ya mkoa Morogoro, baadae asubuhi mwili utaanza
safari ya kurudi Dar es Salaam
Tuesday, May 13, 2014
Makamu wa Rais Dkt. Bilal azindua Mfuko wa Ubunifu na Maendeleo ya Watu (HDIF)
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akikata utepe kuzindua rasmi Mfuko wa Ubunifu na Maendeleo ya Watu,
unaosimamiwa na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) wakati wa hafla
hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam, leo. (Picha na OMR).
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mfuko wa Ubunifu na Maendeleo
ya Watu, unaosimamiwa na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) wakati
wa hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam, leo.
Baadhi ya wadau waliohudhuria uzinduzi huo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na
Teknolojia Prof. Makame Mnyaa na baadhi ya viongozi wa Costech, baada ya
uzinduzi huo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisalimiana na Eng. George Mulamula, wakati alipowasili kuzindua
Mfuko wa Ubunifu na Maendeleo ya Watu, unaosimamiwa na Tume ya Sayansi
na Teknolojia (COSTECH) wakati wa hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar es
Salaam, leo. (Picha na OMR).
Friday, February 21, 2014
Tuesday, February 11, 2014
HUU UNYAMA GANI HUU JAMANI MTOTO ALIYETAFUNWA USO NA BABA YAKE SASA NI MATESO.
Stori: Jelard Lucas na Makongoro Oging’
SUSULUKA Imani Paul, kijana mwenye umri wa miaka 18, ambaye Novemba mwaka jana alikutana na unyama wa aina yake, baada ya kutafunwa sehemu kubwa ya uso wake maeneo ya mdomoni, analia kutokana na mateso makubwa yanayotokana na maumivu ya mwili pamoja na ukosefu wa fedha za matibabu na mahitaji.
Susuluka, mkazi wa Kijiji cha Nyabibuye Kakongo, wilayani Kibondo mkoani Kigoma, alijeruhiwa vibaya kwa kutafunwa usoni na baba yake mzazi, Imani Paulo (36) kwa kung’atwa kisha kunyofolewa macho, pua na meno kubaki nje.
Inadhaniwa kuwa wakati wa tukio hilo, baba yake mzazi alikuwa hana akili za kawaida na inadaiwa kuwa hadi sasa bado anashikiliwa na polisi huku uchunguzi zaidi wa tukio hilo ukifanywa.
Kwa sasa, kijana huyo ambaye anadai kuishi katika mazingira magumu kutokana na kukosa kwake fedha za kujikimu, yupo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili akitibiwa.
“Nateseka sana, inaniuma sana, baba yangu mzazi alinitafuna uso mzima, kwa sasa sina cha kuniokoa katika maisha, fedha za kwenda India sina japo serikali imeahidi kunipeleka, lakini natakiwa kuwa na fedha za kujikimu kama shilingi milioni 1.8, hizo zitasaidia kupata vibali vya kusafiria na mahitaji binafsi, naomba Watanzania waokoe maisha yangu,” alisema Sululuka ambaye anatarajiwa kupelekwa India na serikali hivi karibuni.
Awali taarifa za kijana huyu zilieleza kuwa alikuwa ametafunwa na mwajiri wake lakini sasa ameamua kufunguka kwa madai kuwa aliogopa baba yake angekamatwa na polisi.
Kama umeguswa na kilio cha kijana huyu wa Kitanzania, mchangie ulichonacho na Mungu atakupa baraka zake na ili aweze kujikimu na hata kumsaidia kwa matibabu kwa namba zifuatazo.
Tigopesa 0653715400 na M-Pesa 0768454656.
SOURCE:GBL
Sunday, February 2, 2014
Subscribe to:
Posts (Atom)



























