Marehemu Geogre Tyson pichani hapa
alikuwa yupo kijiji cha Chilonwa Chamwino kwenye utoaji wa madawati
katika shule ya msingi Chaula iliyopo Dodoma. Baada ya kumaliza shughuli
hii huku akiwa kama producer wa The Mboni Show mauti yalimkuta majira
ya saa 12 jioni masaa 4 tu toka tuanze safari ya kurudi Dar es Salaam
maeneo fulani hivi kama unataka kukaribia GAIRO mjini.
Katika gari hilo walikuwa watu 8 ila yeye
pekee ndio aliyepoteza mauti na wengine kupata majiraha mwilini pamoja
na dereva wa gari hilo. Kwa sasa mwili wa marehemu umehifadhiwa hapa
Morogoro katika hospital ya mkoa Morogoro, baadae asubuhi mwili utaanza
safari ya kurudi Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment