OFISI YA WAZIRI MKUU
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (OWM -
TAMISEMI)
AJIRA MPYA YA MAFUNDI SANIFU WA MAABARA NA
WALIMU KWA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI MWAKA 2014/15
A: Orodha ya Walimu na Mafundi Sanifu Maabara Ajira Mpya
Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI inatangaza ajira ya wahitimu
wa mafunzo ya ualimu na mafundi sanifu maabara katika mamlaka ya Serikali za
Mitaa kama ifuatavyo:-
i.
walimu wa cheti (Daraja IIIA) kwa ajili ya shule
za msingi 11,366;
i.
walimu wa stashahada 4,151 na shahada 12,490 kwa
ajili ya shule za sekondari
ii.
mafundi sanifu maabara 264 kwa ajili kusimamia
maabara na kuandaa masomo ya sayansi kwa vitendo katika shule za sekondari
B: Utaratibu Ajira Mpya kwa Walimu na Mafundi Sanifu Maabara
Kila mwajiriwa mpya anatakiwa kuzingatia yafuatayo:-
i.
walimu wenye sifa waliohitimu mafunzo kwa mwaka
wa masomo 2013/14 wamepangwa pamoja na walimu wa sekondari wa masomo ya sayansi
na hisabati waliohitimu miaka ya nyuma na wameomba kuajiriwa;
ii.
kuripoti kuanzia tarehe 01 Mei hadi 09 Mei 2015
kwenye Ofisi za Wakurugenzi wa Halmashauri kwa ajili ya kuajiriwa na kupangwa
vituo vya kazi;
i.
kuwasilisha vyeti halisi vya taaluma ya kuhitimu
mafunzo, elimu ya sekondari, cheti cha kuzaliwa pamoja na nakala zake;
ii.
hakutakuwa na mabadiliko ya vituo vya kazi; na
iii.
fedha za kujikimu kwa muda wa siku saba (7) na
nauli ya usafiri wa magari (ground travel)
zitatolewa kwenye halmashauri husika baada ya kuripoti.
Imetolewa
na
OFISI YA WAZIRI MKUU
- TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA.
kwa Maelekezo zaidi tafadhali soma taarifa zifuatazo: