Vyama
vya siasa ambavyo havina uwakilishi katika Bunge la Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania vimetangaza kusimamisha mgombea mmoja katika uchaguzi wa
serikali za mitaa unaotarajia kufanyika mwezi ujao.
Wakati
vyama vya upinzani vikiwa na umoja wao maarufu kama UKAWA na kutangaza
kuungana, vyama visivyokuwa na uwakilishi bungeni vimetangaza kuungana
na kuweka mgombea mmoja kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa lengo
likiwa kupambana na UKAWA na Chama Cha Mapinduzi.
Akitangaza jijini Dar es Salaam uamuzi wa kuungana katika uchaguzi wa
serikali za mitaa mwakilishi wa vyama Sita visivyokuwa na uwakilishi
ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha UPDP Bw. Fahmi Dovutwa amesema
kuwa wameamua kuungana ili kupambana na UKAWA na CCM ambapo vyama
vinavyounda umoja huo ni UMD, SAU, UPDP, AFP, Jahazi Asilia na
Demokrasia Makini.
Mmoja wa viongozi wa wanaounda vyama Sita vinavyounda vyama hivyo
ambaye ni wenyekiti wa Chama cha Wakulima (AFP) Bw. Rashid Rai amesema
kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa ni msingi wa maendeleo hivyo ametoa
wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki katika uchaguzi huo.
No comments:
Post a Comment