Gari aliyokuwa amepanda MAALIM SEIF ikiwa imeharibika vibaya Na Karoli Vinsent |
Habari zilizotufikia mda huu Zinasema MSAFARA
wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na
Katibu Mkuu Taifa wa Chama cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad
umepata Ajali mbaya Mkoani Mwanza na kupelekea Viongozi mbalimbali wa
Chama hicho kuwa na hali mbaya.
Vilevile
Mkurugenzi huyo wa Habari wa Chama hicho alisema kwa sasa Majeruhi hawo
wamekimbizwa kwenye Hospitali ya Bugando kupatiwa matibabu na hali yao
inaendelea vizuri isipokuwa Katibu chama cha Cuf kutoka Wilaya ya
Nyamagana Rehema Mwenda hali yake sio Nzuri kutokana na kupoteza Fahamu,
Mkurugenzi wa habari wilaya'na MH SHIDO Ambae ni mwenyekiti wa serikal ya mtaa uliyopo kata ya miringo,wameumia vibaya wamelazwa hospitali ya BUGANDO
|
Akithitisha kutokea kwa Ajali hiyo wakati anaongea na Mwandishi wa
Mtandao huu, mda huu kwa njia ya simu kutoka Mkoani Mwanza kwenye Ajali
hiyo, Naibu Mkurugenzi wa Habari kutoka Chama cha Wananchi CUF bwana
Kambaya alithibitisha kutokea kwa Ajali hiyo na kusema Makamu wa Kwanza
wa Rais wa Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Maalim na Katibu Mkuu Taifa
wa Chama cha Wananchi (CUF) Seif Sharif Hamad ajadhurika na yuko
salama bali waliodhurika na Ajali hiyo ni viongozi wa chama hicho,
Rehema Mwendaalikuwa kwenye msafara huo aiugulia maumivu |
“Ni
kweli Msafara wa Makamu wa rais na Katibu mkuu Taifa umepata ajali ila
yeye yuko salama,lakini viongozi wetu wa chama akiwemo katibu
wa Chama cha Wananchi CUF Wilaya ya Nyamagana Be Rehema Mwenda Pamoja
na Mkuu wa Kitengo cha cha Habari wa chama Chetu wilaya ya nyamagana
Hassan Shido ndio wamepata majeraha kutokana na Ajali hiyo,”alisema Kambaya.
Kambaya
alizidi kusema Ajali imetokana na Dereva wa Gari aina Scania kwenda
kuligonga Gari lilokuwa limewabeka viongozi hao,ambapo gari hilo
lilikuwa la nne kutoka gari lililombeba Maalim Seif kwenye msafara
huo,
No comments:
Post a Comment