Hamis Mandi ‘B 12’.
Clouds Fm imeamua
kuchukua maamuzi magumu ya kuwasimamisha kazi kwa muda usiofahamika
watangazaji wake maarufu yaani Hamis Mandi ‘B 12’, Adam Mchomvu na
Loveness Malinzi ‘Diva’ . Kwa mujibu wa gazeti la Risasi Mchanganyiko
zinasema kuwa uongozi wa Clouds umefikia hatua hiyo baada ya kuchoshwa
na tabia ya utovu wa nidhamu wa watangazaji hao.
Adam Mchomvu.
“Ni kweli tumefikia
uamuzi wa kuwasimamisha B 12, Diva na Mchomvu baada ya kukiuka baadhi ya
makubaliano baina yao na ofisi hivyo kusababisha usumbufu mkubwa ambao
ulitulazimu kuingia gharama ambazo hazikutarajiwa” alisema mkurugenzi wa
Uzalishaji na Vipindi wa clouds Media Ruge Mutahaba.
“Hatutakuwa nao kwa muda usiojulikana ingawa watu wengi wamekuwa
wakinihoji juu ya hilo lakini watachotakiwa kuelewa ni kwamba hakuna
ofisi isiyokuwa na sheria na taratibu za kuongoza watu wake, sasa hao
wamevunja taratibu zetu,” Aliongezea Bwana Ruge Mutahaba.
Loveness Malinzi ‘Diva’.
Alipoulizwa ni taratibu zipi watangazaji hao walizovunja alisema:
“Nashindwa kueleza kosa la kila mmoja ila naomba nieleweke kuwa hao
watangazaji kwa sasa tumewasimamisha kwa muda usiojulikana wakati
tukifikiria cha kufanya. Muhimu hapo ni kwamba wamekwenda kinyume na
tulivyokubaliana.
-GPL
No comments:
Post a Comment