Wednesday, January 15, 2014

Kajala aelezea tuhuma za kuiba mume wa mtu. Ni zile zilizozagaa kwenye mitandao siku za nyuma



Kajala aelezea tuhuma za kuiba mume wa mtu. Ni zile zilizozagaa kwenye mitandao siku za nyuma 
 
Kajala aelezea tuhuma za kuiba mume wa mtu. Ni zile zilizozagaa kwenye mitandao siku za nyuma 1

Ni zile stori za town sasa hivi ambapo mwigizaji Kajala amezungumza kwa mara ya kwanza kuhusu ishu yake ya kuandikwa kwenye blogs na magazeti ya bongo kuhusu tuhuma za kuchukua mume wa mtu.
Kajala anasema picha iliyopigwa akiwa na huyo mume wa mtu, kwanza ilipigwa bila yeye kujua lakini pia anasisitiza kwenda club au kwenda sehemu na kukutana na mtu na kupiga nae picha sio kwamba ndio umemuiba.


Anasema siku ya tukio ilikua ni siku ya kuzaliwa kwa mmiliki wa club hii ndio ikawa party hivyo kila mtu alikua anapiga picha ovyo ovyo ndio maana hata yeye hakujua kama anapigwa.

Kajala ambae ni mama wa mtoto mmoja mwenye umri wa miaka 14, anasema picha hii na taarifa za kuiba mume wa mtu zimemletea tatizo na maswali kwa familia yake hasa Mtoto na Mama yake.

Anasema mama yake mzazi aliumwa kwa mshtuko alioupata kwa sababu alidhani mwanae kaenda China kikazi na sio kuchukua mume wa mtu.
MWARICK JAPHET MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

EXCLUSIVE AUDIO KUTOKA KWA DIAMOND PLATNUMZ FT CHEGE, ISIKILIZE HAPA KWA MARA YA KWANZA



Zitumie hizi dakika kadhaa kumsikiliza alichokifanya Diamond kwenye hii beat ya Chegge Chigunda ya Uswazi Take away,uongozi wake umetubariki kuwapa watanzania hii kama Exclusive kwenu kuisikiliza hii nyimbo afu tupe  maoni yako hapo chini kwa kucoment.

 https://soundcloud.com/king-sele-blog/diamond-feat-chege_nitashinda
MWARICK JAPHET MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

Hamis Mandi ‘B 12’, Adam Mchomvu na Loveness Malinzi ‘Diva’, wamepigwa chini na Clouds Fm



 

Hamis Mandi ‘B 12’. 

Clouds Fm imeamua kuchukua maamuzi magumu ya kuwasimamisha kazi kwa  muda usiofahamika watangazaji wake maarufu  yaani  Hamis Mandi ‘B 12’, Adam Mchomvu na Loveness Malinzi ‘Diva’ . Kwa mujibu wa gazeti la Risasi Mchanganyiko zinasema  kuwa uongozi wa Clouds umefikia hatua hiyo baada ya kuchoshwa na tabia ya utovu wa nidhamu wa watangazaji hao. 
 
         Adam Mchomvu.

“Ni kweli tumefikia uamuzi wa kuwasimamisha B 12, Diva na Mchomvu baada ya kukiuka baadhi ya makubaliano baina yao na ofisi hivyo kusababisha usumbufu mkubwa ambao ulitulazimu kuingia gharama ambazo hazikutarajiwa” alisema mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi wa clouds Media Ruge Mutahaba.

“Hatutakuwa nao kwa muda usiojulikana ingawa watu wengi wamekuwa wakinihoji juu ya hilo lakini watachotakiwa kuelewa ni kwamba hakuna ofisi isiyokuwa na sheria na taratibu za kuongoza watu wake, sasa hao wamevunja taratibu zetu,” Aliongezea Bwana Ruge Mutahaba.
 
Loveness Malinzi ‘Diva’. 

Alipoulizwa ni taratibu zipi watangazaji hao walizovunja alisema: “Nashindwa kueleza kosa la kila mmoja ila naomba nieleweke kuwa hao watangazaji kwa sasa tumewasimamisha kwa muda usiojulikana wakati tukifikiria cha kufanya. Muhimu hapo ni kwamba wamekwenda kinyume na tulivyokubaliana.
 
 
 -GPL
MWARICK JAPHET MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

Friday, January 10, 2014

Mmmh! Ni noma! Wema apost Video ya Diamond akiwa kitandani kifua wazi. Hatari sana


Mmmh! Ni noma! Wema apost Video ya Diamond akiwa kitandani kifua wazi. Hatari sana


Leo mwanadada wema sepetu amezidi kuudhihirishia ulimwengu wa fans wake kuwa kijana raisi wa wasafi aka Diamond Platnumz ndio mahabuba wake baada ya kupost video ya mwanamuziki huyo akiwa kitandani kifua wazi kabisaaa huku akiandika “In da middle of his writing session…jus had to distrub him a little”. Mmmh hatari sana!   
MWARICK JAPHET MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.