Sunday, June 3, 2012

HISTORIA FUPI YA MAREHEMU (DAUDI KILUNGUMIKA LUFEGA) ALIYEKUWA MWENYEKITI WA MTAA WA BANK WILAYANI MAGU KUPITIA CHAMA CHA WANANCHI (CUF)


HISTORIA FUPI YA MAREHEMU DAUDI KILUNGUMIKA LUFEGA KUZALIWA Marehemu alizaliwa mnamo mwaka 1960 akiwa ni Mtoto wa Saba katika familia ya Mzee Lufega Masalu, Alizaliwa katika Kitongoji cha Benki eneo ambalo kwa sasa Cadirac Hotel. Katika Wilaya ya magu na Ndani ya Mkoa wa Mwanza. ELIMU Daud Kilungumika Lufega alipata Elimu yake ya msingi Katika Shule ya Msingi Nyalikungu mwaka 1972 na kuhitimu darasa la saba mwaka 1978. 1980 Alijiunga na Chuo cha Kilimo na Mifugo Ukiligulu Mwanza na kutunukiwa cheti cha Afisa Usimamizi Kilimo na Mifugo. UBATIZO: Daudi Kilungumika Lufega alikuwa ni Muumini wa Kanisa katoliki. Mwaka 1993 alibatizwa katika Parokia ya Magu. Mwaka 1993 alipata kipaimara katika Parokia ya Magu. NDOA Mwaka 1985 alimwoa Bi. Fausta Mayengela. KAZI/SHUGHULI Mwaka 1981 -1984 Afisa Mazao wa Mamlaka ya Pamba –Tanzania Kanda ya Manawa Ginnery. 1984-1994- Afisa Ukusanyaji mapato(Revenue Collector) HALMASHAURI YA Wilaya ya Magu. UONGOZI NA UZOEFU: Mwaka 1999-2009 Balozi wa nyumba kumi na Mwenyekiti wa Kitongoji cha Benki. Kwa Tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mwaka 2009-2012 Mwenyekiti wa Mtaa wa Benki katika Mamlaka ya Mji Mdogo wa Magu Mjini Kwa tiketi ya Chama Cha Wananchi –CUF. Mwaka 2010-2012 Kada wa Chama na Mjumbe wa kamati ya Utendaji Wilaya –CUF. UGONJWA na MAUTI Daudi Kilungumika Lufega alianza kuugua Mwezi Marchi 2012 akisumbuliwa na matatizo ya Inni na Figo, Alibahatika kupata Matibabu katika Hospital ya Wilaya ya Magu pia alifakiwa kupata matibabu ya Tiba mbadala 1. Lakini kwa vile Andiko linasema “Kila nafsi itaonja mauti” 2. Na Kwa kuwa Mauti ni kitanda ambacho kila Mwanadamu atakilalia. 3. Mauti ni Mlango ambao kila Mwanadamu atauingia. 4. Mauti ni vazi ambalo kila Mwanadamu atalivaa. Na Tarehe 31-05-2012 Majira ya saa 12:30 asubuhi Daudi Kilungumika Lufega alifariki Dunia. Marehemu ameacha 1. Mjane 2. Watoto 9 wakiume 4 na Wakike (5)Watano, na 3. Wajukuu 4 SHUKRANI: Familia ya Marehemu inatoa Shukrani zake za dhati kwa Waganga na Wauguzi wote wa Hospital ya Wilaya ya Magu kwa juhudi zao kumhudumia Marehemu kipindi alipokuwa amelazwa Hospitalini hapo. Wataalam wa Tiba mbadala kwa Jitihada zao zote za Kutaka kuokoa Maisha yake japo haikuwezekana. Shukrani kwa Majirani, Ndugu, Jamaa, Marafiki, Vyama vya Siasa, Mamlaka ya Mji Mdogo Magu Mjini na wote walioshiriki kwa namna moja ama nyingine katika hali na Mali kufanikisha Mazishi na Maziko ya marehemu Mpendwa wetu. Marehemu alikuwa Mtu wa Watu, Mcheshi, Mtu huru na mtu mwenye maamuzi ya kweli. BWANA AMETOA, BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE, AMINA.
MWARICK JAPHET MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

No comments:

Post a Comment