Friday, July 19, 2013

KIFO CHANGU KITASABABISHWA NA PRESHA.....WOLPER


STAA wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper ameeleza kuwa, tatizo alilonalo la presha ya kushuka huenda siku moja likawa chanzo cha kifo chake kwani linapomjia, huwa katika hali mbaya sana.

Akizungumza hivi karibuni Wolper alisema, tatizo hilo amekuwa nalo kwa muda mrefu na kufikia hatua ya kwenda kutibiwa nchini Afrika Kusini likapungua lakini sasa limerejea na linamkosesha amani.


“Kwa kweli hili tatizo la presha ya kushuka nililonalo ipo siku litaniondoa duniani, unajua wakati mwingine hali hiyo ikinijia natokwa na damu nyingi puani, huoni ni tatizo kubwa hili!”
alisema Wolper.

MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

No comments:

Post a Comment