Thursday, February 21, 2013

EXCLUSIVE:KAULI YA DIMOND KUHUSU MGANGA WAKE,KUTAPELI MIL 9 ZA WANYARUANDA,UHUSIANO NA MREMBO PENNY,SHUTUMA ZA Q-CHIEF NA KUFULIA KATIKA SHOW YA MWANZAJana Diamond Platnumz kupitia kipindi cha XXL cha Clouds FM, ameamua kufunguka kwa undani kuhusiana na shutuma zinazoelekezwa kwake kuanzia kudaiwa kutumia waganga wa kienjeji kuosha nyota yake na scandal zingine. Kuhusiana na mganga anayedai kuwa atamshusha Diamond baada ya kumtelekeza Diamond amesema:
Mganga wa ukweli hawezi akaenda kulalamika kwenye media eti ‘ mteja wangu kanikimbia nini na nini’ mganga anaenda kulalamika katika killing! Kama ni mteja wako kweli utaenda kuripoti kwa mzee wako aliyekupa ndumba kwamba yule ashuke, akishuka mwenyewe atarudi atakwambia ‘broo nimeshuka tuyamalize,’ lakini mtu anaenda kwenye redio eti namba yangu ya simu napatikana hii eti napatikana kwenye Facebook (anacheka) ……….mara ya kwanza nilivyosikia nilicheka sana nikasema da!!!! Mwenyezi Mungu kanipa nyota kubwa sana mpaka baadhi ya waganga wanataka ku hit kupitia nyota ya Diamond hiki ni kitu cha kuchekesha! Halafu kikanishangaz.
Kuna siku nilienda katika tv station moja nilipofika nikaona jina lake nikasema mimi nataka niwekwe naye meza moja tukae nizungumze nisikie anasemaje lakini mwisho wasiku akakataa ananikimbia anasema ‘mimi sitaki kulumbanan nae nini na nini’ sasa ukitazama unaona tu.
Unajua kuna kitu kimoja ambacho kipo Tanzania mtu anapoanza kufanya vizuri kutengeneza ramani nzuri watu baada ya kumsaidia kumsapoti kutoka juu aende mbali zaidi wanataka kumgandamiza kumshusha na hili ndilo tatizo tunalipata hata kwenye mipira tunakosa wachezaji wakucheza nje na nini, kwasababu watu kama akina Ngassa wakiwa wanajitahidi badala ya kuwasapoti mwisho wa siku mtu akitaka kusajiliwa na timu fulani kucheza oo!! mara watu wanaanza kuzusha kapewa chakula hajamaliza kapewa kuku mzima hajamaliza wewe unatakiwa umsapoti.
Kuhusu kama aliwashahi kumuona mganga huyo
Sijawai kumuona nilimuona kwenye gazeti na kwenye mtandao wa vitukovyamtaa.blogspot.com pia kwenye gazeti niliona picha yake inakuwa vipi , kilicho nistaajabisha ikanibidi mimi lazima nitafute source imekuwaje? nikatoka unajua kila kitu lazima nimlalamikie mama yangu,mama akaenda kumtafuta papaa akamwambia kwasababu alikuwa anasema alikuwa ananitumia toka zamani basi hii link imetoka huko. Papaa akaulizwa akasema ‘kuna watu mwanzo tulikuwa tunafanya nao kazi hadi tukavunja mkataba mimi na Papaa hadi nikamlipa pesa papaa wale watu walikasirika kwanini papaa umevunja mkataba na Diamond, wakati Diamond anazidi kufanya vizuri tungekuwa tunavuna mapesa ,kwahiyo wale watu ndio wanaunda fitina hivyo wanamtishia papaa. Huwezi kuamini hawa watu walikuja kuniibia tuzo moja ama kwamba waende wakaizindike wenyewe wanavyodai ili wakaichimbie kwenye shimo lile shimo ndilo linalopandisha msanii, kwahiyo atashuka, cha ajabu nikapata tuzo nyingine.
Kuhusu Q-Chief
Kiukweli naomba niongee ukweli maana kuna vitu vina fichwa fichwa mimi nawaheshimU sana wasanii waliotangulia sababu najua hata nikifanya nini siwezi kuwafikia, wao alioanza kaanza tu. Lakini nasononeshwa na mimi eti kujitangaza kwangu namkubali Q chief yeye mwenzangu anasema mimi natembelea nyota yake, kampigia simu dada yangu Halima anamtukana hadi meseji zipo eti Diamond anasifia nyota yangu, sijui nini na nini! Come on mimi naanza kutoka maskini ya Mungu na Nenda Kamwambie Q chief kishapotea, mimi mapenzi yangu tu namkubali kwanini nisingesema labda.. brother Dully wajua kaka yangu kabisa siwezi kusema ndugu lakini ananisaidia katika vitu vingi ningekuwa mnafiki ningesema labda namkubali sana Dully ndio msanii wangu namna moja namkubali.
Lakini nasema hhaa namkubali Q Chief.
Lakini yeye kumheshimu kwangu mimi anasema eti mimi namroga. Kuna siku unajua alinikuta kwa Manecky akaniambia “ mdogo wangu mwanzo mimi nilikuwa nafikiri unaniroga mimi nilikuwa nikienda kila kwa mganga ananiambia haunirogi, dah nilikuwa nakumind kinoma”. Kila nikienda namkuta Khalid sasa yeye kasema mwanzoni TID alikuwa anamroga, alivyotoka Cassim Mganga akasema Cassim anamroga, alipotoka Ali Kiba akasema anamroga sasa kila msanii anayetoka anasema kamroga yeye tu kwa nyota ipi? Ya kuvuta unga ya kufanya vitu gani! Mimi sipendezewi anavyowaambia watu kuwa mimi namroga, kwanini nisitembelee nyota ya watu kama akina Omary, akina Ben Pol. Alumbane na wakubwa wenzie akina Dully Sykes, mimi sitaki, namheshimu abishane na wakubwa wenzie, mimi mdogo aniache na wadogo wenzangu.

Kuhusu tetesi kuwa show zake zimepunguza mahudhurio ya watu kuliko mwaka jana
Picha ya show yake ya Mwanza hivi karibuni

 Picha ya show yake ya Mwanza hivi karibuni
Hizo ni drama tu watu wanatengeneza watu kuna zile kuvizia mwanzo wa show, maake kuna show nimeziona watu wamevizia watu wanavyoingia mwanzo eti wanapiga picha, wanatengeneza tengeneza vipicha halafu wanasema hivyo. Show yangu ya mwisho nimefanya Arusha tarehe 16 kiingilio 150,000 watu walivyoingia pale ukiingia katika thisisdiamond unaona. H kufanya msanii yeyote kiingilio laki na hamsini nimefanya Arusha.
Diamond akiperform kwenye show ya Arusha kwenye ukumbi wa  CLUB SAFARI CARNIVAL
Diamond akiperform kwenye show ya Arusha kwenye ukumbi wa CLUB SAFARI CARNIVAL
Mtu anasema yeye ananiroga mimi nashuka mwezi mzima ntakuwa na show Europe, Jumamosi nina show Hyatt pale, Jumapili nina show Mombasa wiki inayofuata ninasafiri naenda nje nina show kama kumi yaani ukinibook mimi mpaka mwezi wa saba nimejaa wewe unaniambia mimi nimeshuka vipi!
Kuhusu uhusiano na Penny
001867ec785a11e2b12d22000a9e295b_7

No Penny tunafanya movie anacheka, kuna movie tunarekodi sio wapenzi
Fetty: Diamond unadanganya bro

B12: Kwasababu kuna picha nyingi zinasambaa kwenye Instagram yale ni mapozi ya kutengeneza hiyo movie au?
Diamond: anacheka yeah pale tulikuwa tunarekodi sababu ni movie ambayo tuna mahusiano kwahiyo wakati tuna rekodi kuna picha zinakuwa zinapigwa, ni dramatic za kuuza movie unajua!
B12: Movie inaitwaje na inatoka lini? Adam: na kampuni gani?
Diamond: aaaaaaaaaah vitu vingine vya siri (wote wanacheka)
Fetty: kuna story za chini chini sana, the reason why unamuita baby mama (Penny) kwamba she is expecting….
Diamond: Analikwepa swali huku akicheka na kudai muda wa kipindi cha XXL umeisha wawapishe wengine.

Kuhusu wimbo aliomshirikisha Tanzanite uitwao Mapenzi
Diamond anasema hajamshirikisha Tanzanite na kwamba amekuwa akimchokonoa tangu aseme wimbo Mbagala ulikuwa wake na baadaye kudai Diamond anamroga. Anasema alichokifanya sasa ni baada ya kupata wimbo wa Diamond uliovuja ambao ulikuwa na verse moja tu, Tanzanite aliuchukua na kurekodi verse yake kisha kujifanya kuwa ameshirikishwa na Diamond. Diamond anasema amefanya hivyo bila ridhaa yake. Amedai kuwa atamfanya kitu kibaya kama akiendelea kumtafuta.

Kuhusu kushindwa kwenda show ya Rwanda
Amedai kuwa Micho ni msanii anayefanya vizuri nchini Rwanda ambaye alimpigia simu kumuomba wafanye collabo. Anasema Mico alikuja Tanzania na Diamond akakubali kufanya collabo naye bure kwenye studio za MJ Records. Anasema msanii huyo alimtaka aende kufanya naye show Rwanda na kumpa advance Diamond dola 1,000 kati ya 6,000 alizotakiwa kutoa kwaajili ya show hiyo. Micho aliahidi angempa tena dola 2,000 tarehe 20 January lakini aliendelea kumpiga chenga Diamond.
Tarehe 11 Feb alimtumia dola 2,000 kwa njia ya western union lakini kuhusu tiketi za ndege Diamond anasema Mico alidai kuwa ndege zimejaa hivyo aende peke yake na yeye akamwambia kuwa lazima aende na dancers wake na mpiga picha wake.Diamond anasema Micho aliendelea kumpiga sound mpaka siku ya show na siku hiyo ndio akamtumia tiketi saa kumi kasora muda ambao Diamond asingeweza kusafiri. Diamond anasema hilo ni kosa la Mico.
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

No comments:

Post a Comment