Wednesday, June 27, 2012

Mkasi - SO3E05 with Ray


MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

Belle 9 - Amerudi


MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

Tuesday, June 26, 2012

WAHAMIAJI 42 RAIA WA EPHIOPIA WAFARIKI DODOMA


Kamanda Zelothe Stephen
WAHAMIAJI haramu 42 raia wa Ethiopia wamekufa katika Kijiji cha Chitego Tarafa ya Zoisa Wilayani Kongwa mkoani Dodoma wakiwa safarini kutoka Ethiopia kwenda Malawi.
Taarifa za awali kutoka eneo la tukio zinasema kuwa wengine 74 hali zao ni mbaya sana kutokana na kukosa chakula na maji hivyo wanaendelea kupatiwa matibabu. Baadhi ya mashuhuda ambao hawakutaka kutaja majina yao wamesema wahamiaji hao waligunduliwa na wananchi wa kijiji hicho waliokuwa wakienda katika shughuli zao za kilimo jana asubuhi. Taarifa hiyo inadai kuwa wahamiaji hao walikutwa porini wakiwa hoi usiku wa kuamkia leo (jana)baada ya kushushwa katika lori ambalo bodi lake ni la Kontena Taarifa hizo za awali zinasema kuwa wahamiaji hao walikuwa 116 ambao walikuwa wamefungiwa katika kontena hilo na hivyo kukosa hewa kutokana na kulundikana. Mpaka sasa haijulikani gari hilo lina milikiwa na nani kwani wahamaji walionusulika wengi wake wapo katika hali mbaya. Mpaka sasa hakuna mtu aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo huku wahamaji watano wanaendelea kupata matibabu katika Zahanati ya kijiji cha Chitego ambapo wengine waliobaki wamehifadhiwa katika kanisa la Anglikan wakipatiwa huduma mbalimbali. Huduma hizo mbalimbali ni pamoja na kupewa maji , uji na matibabu. Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma Zelothe Stephen amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuhaidi kutoa taarifa zaidi baadaye.
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

Tuesday, June 12, 2012

MAHAKAMA YASOGEZA KESI YA LULU HADI TAREHE 25 JUNI, 2012.


Lulu’ akishuka katika basi la magereza.
‘Lulu’ akiwa ndani ya mahakama.
‘Lulu akiteta jambo na wakili wake muda mfupi baada ya kufika mahakamani.
Akitoka mahakamani baada ya kesi yake kusogezwa hadi tarehe 25 mwezi huu, ambapo watetezi wa ‘Lulu’ wametakiwa kuwasilisha vielelezo vyenye uthibitisho wa umri wake ifikapo tarehe 13 mwezi huu, wakati upande wa serikali wameomba kuwasilisha vielelezo vyao tarehe 22 mwezi huu ili kumaliza tatizo la utata kuhusu umri wa mtuhumiwa huyo.
Ulinzi ulikuwa ni wa uhakika eneo lote nda na nje ya mahakama kuu wakati wa kesi hiyo.
HABARI TOKA http://dewjiblog.com
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

Monday, June 11, 2012

KENYA WATANGAZA SIKU TATU ZA MAOMBOLEZO YA SAITOTI


Kenya imetangaza siku tatu za maombolezi baada ya kifo cha Waziri wa Usalama wa Kenya, Profesa George Saitoti, na naibu wake, Orwa Ojode, kwenye ajali ya helikopta ya polisi katika eneo la Ngong, nje ya Nairobi. Mabaki ya ajali hiyo. Rais Mwai Kibaki alisema kifo cha Bwana Saitoti ni msiba mkubwa kwa taifa, na serikali imetangaza kuwa baraza la mawaziri litakutana Jumatatu, kujadili tukio hilo. Idara ya polisi imesema uchunguzi utafanywa kujua sababu ya ajali hiyo, na balozi wa Marekani mjini Nairobi, amesema Marekani iko tayari kusaidia kwenye uchunguzi huo, ikiwa itatakiwa kufanya hivyo. Msemaji wa polisi alieleza kwamba inavoelekea kuanguka kwa helikopta hiyo lilikuwa tukio la ajali. Raia wa Kenya walikuwa na masikitiko Jumapili, baada ya taarifa ya ajali hiyo kujulikana, na watu wamekuwa wakizuru nyumba ya kuhifadhi maiti mjini Nairobi kutoa heshima zao. Makamo wa rais wa Kenya, Kalonzo Musyoka, alipofika kwenye tukio la ajali alitoa rambi-rambi zake na alieleza wale waliokuwamo ndani ya ndege ambao wote wameteketea:"Ndege hiyo ya aina ya Eurocopter ya police airwing, ambayo ilikuwa inaelekea Yugis, ilikuwa imembeba Waziri George Saitoti, naibu waziri Orwa Ojode na maafisa rubani wa ndege, Nancy Gitwanja na Luke Oyugi, na vilevile askari wawili ambao wanakuwa wanaandamana na Waziri Saitoti, Inspector Tonkei na Thomas Murimi" Rambi-rambi zimekuwa zikimiminika nchini Kenya, pamoja na za Kofi Annan, Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, ambaye alipatanisha baada ya ghasia za uchaguzi uliopita nchini kenya. Profesa Saitoti alikuwa akizungumza kwa ukali dhidi ya al-Shabaab na inaaminiwa alihusika na uamuzi wa jeshi la Kenya kuingia Somalia mwaka jana. Bwana Saitoti aliwahi kuwa makamo wa rais na waziri wa fedha katika serikali ya Rais Moi, na akitarajiwa kugombea urais katika uchaguzi wa mwaka ujao. Alikuwa na umri wa mika 67.
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

Friday, June 8, 2012

HATUA ZA MWISHO ZA FILAM YANGU MPYA (LOST FAMILY) ZAONEKANA


HIZI NI BAADHI YA HATUA KATIKA LOST FAMILY TUKIJARIBU KUSHAURIANA NA DIRECTOR WANGU HAPA
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI FURSA YA WASANII WA TANZANIA KUSHINDA EURO 5,000 KATIKA SHINDANO LA KUTUNGA WIMBO RASMI WA KUNDI LA MATAIFA YA AFRIKA, KARIBIANI NA PASIFIKI (ACP GROUP OF STATES)


Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo limepokea mwaliko wa Wasanii wa Tanzania kujitokeza kushiriki shindano la kutunga wimbo utakaokuwa unatumiwa kama wimbo rasmi wa mataifa ya Afrika, Karibiani na Pasifiki (ACP Group of States). Shindano hili ambalo litahusisha mataifa 79 wanachama wa umoja huu limeandaliwa na Sekretarieti ya ACP kwa lengo la kupata wimbo ambao utabeba dhana ya mataifa ya Afrika, Karibiani na Pasifiki. Kwa mujibu wa taarifa ya Sekretarieti ya ACP, shindano hili linamhusu msanii mmoja-mmoja au Kikundi cha wasanii ambao watapaswa kutunga wimbo huo kwa kuzingatia lengo kuu la umoja huo ambalo ni Maendeleo Endelevu na Upunguzaji Umaskini sambamba na Ushawishi mkubwa kwenye Uchumi wa Dunia. Aidha, wimbo huo utatakiwa uwe wenye kujenga moyo, fikra na kutangaza malengo ya kundi hili la mataifa ya Afrika, Pasifiki na Karibiani. BASATA inatoa wito kwa wasanii wa Tanzania kujitokeza kwa wingi kushiriki shindano hili kwani ni heshima na fursa pekee tumepewa kama taifa kuonesha vipaji na uwezo wetu kimataifa katika eneo la utunzi wa nyimbo. Ni wazi kuwa, kujitokeza kwa wasanii wetu wengi kushiriki katika shindano hili si tu kutaonesha utayari wa sisi kama taifa katika kushindana na mataifa mengine wanachama bali utakuwa ni mwanya wa kuitangaza Sanaa yetu ya muziki nje ya mipaka yetu. Ikumbukwe kuwa, ushindi wa Msanii kutoka Tanzania kwenye shindano hili kutamjengea heshima msanii husika na taifa kwa ujumla. Maelekezo kuhusu Wimbo utakaotungwa • Tungo zote lazima ziandikwe katika moja ya lugha rasmi za ACP ambazo ni Kiingereza, Kifaransa, Kiispaniyola na Kireno. • Wimbo huo uliokamilika lazima uambatanishwe na tunzi (lyrics) zilizoandikwa na zitumwe katika mfumo wa MP3/DVD/WAV Format • Tungo ziguse maeneo yafuatayo i) Fikra ya umoja ambayo itaunganisha nchi wanachama wa ACP ii) Utajiri na tamaduni mbalimbali zilizo katika nchi wanachama wa ACP iii) Mataifa wanachama wa ACP na kuheshimu Demokrasia, Haki za Binadamu na Utawala Bora. iv) Nchi wanachama wa ACP na msisitizo katika maendeleo yenye usawa pia kusimamia mikataba ya kimataifa ya Haki na Amani. Jinsi ya Kushiriki Nyimbo zilizotungwa kwa kufuata mwongozo huo wa ACP zitumwe kupitia anuani ifuatayo ;- Josephine Latu-Sanft (Press Office) Avenue Georges Henri 451,1200 Brussels, Belgium E-mail : latu@acp.int. Mwisho wa kutuma Agosti 31, 2012 Imetolewa na; Ghonche Materego Katibu Mtendaji - BASATA
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

Monday, June 4, 2012

Habari kwa Kiswahili: FBI Kuzima Kompyuta 350,000 Zilizoambukizwa na Virusi.


Mmoja kati ya watengeneza virusi aliyewekwa chini ya ulinzi na watu wa usalama FBI kutokana uhalifu wake. Hivi sasa FBI iko katika maandalizi ya kuzima kompyuta 350,000 duniani kote kutokana kuambukizwa na kirusi aina ya Trojan aliyetengenezwa na kundi la Kiestoni ambalo ni la wahalifu. Pia FBI wamefanikiwa kukamata kifaa aina DNS changer ambacho hutumika kutengenezea Vurusi hao. Walinzi wa kimarekani ambao wanashughulika na uhalifu huo wanafahamu kompyuta na Macs zote zilizoambukizwa na hicho kirusi aina ya Trojan , hivyo basi hitimisho la wamiliki endapo watachukua hatua ya kutatua tatizo, njia ni moja ya kuviondoa vifaa hivyo katika mtandao (Internet). Kifaa hicho cha kutengeneza virusi DNS changer, kilitengeneza na kuachia virusi hao kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 2007. Kiliweza kuhasiri watumiaji, kwani kompyuta ilitenda kazi kinyume na inavyoweza. Na tatizo kubwa kwa watumiaji ilikuwa kompyuta kufanya kazi kwa taratibu sana katika mtandao. Pia virusi hivyo viliweza kulemaza antivirus programu na maelekezo ya kompyuta kuwa ya udanganyifu. Virusi hivyo viliachiwa na kundi la wahalifu wa Kiestoni na kuaminika kuwa, idadi ya virusi vilivyoachiwa katika mtandao ni dola milioni 16. Baada ya kashfa hiyo kugundulika, FBI walizima kifaa hicho kilichotumiwa na wahalifu cha kutoa mawasiliano ya mtandao (server) na mmoja wao kuchua nafasi hiyo, lakini Bureau alitaka kifaa hicho (server) kizimwe kabisa kwa sababu kinagharamia makumi ya maelfu ya dola kukiendesha. Bureau iliweka kifaa maalumu cha kutoa mawasiliano ya mtandao (Server) kwa maombi ya DNS kutoka kwa kompyuta zilizoambukizwa, kwani bila kifaa hicho (server) kompyuta hizo zilizoambukizwa zisingeweza kuunganishwa na mtandao. Jinsi ya kuunganishwa na mtandao Amri ya mahakama iliruhusu kifaa cha kotoa mawasiliano ya mtandao (Sever) cha FBI kupitisha anwani ya IP ya wale walioambukizwa na muda wake kumalizika Julai 9, wakati kompyuta hizo zitakapokuwa zimeondolewa katika mtandao (offline). hatua hiyo, kompyuta zote zilizoambukizwa na virusi aina ta Trojan hazitaweza kuunganishwa katika mtandao. Kuepukana na kompyuta yako kuzimwa na mtandao wa kuhakiki kompyuta zilizoambukiza "DNS ya FBI. ambao unaruhusu kwa sasa watumiaji kuangalia kama wana virusi na kuviondoa mapema. Kwani inasemekana kuwa tayari kuna baadhi ya kompyuta 150,000 zimesafishwa virusi hao. Lakini baadhi ya wakosoaji wanaonya hii, kuwa haitoshi hivyo ni bora kutangaza na uhamasishaji unahitajika. Ni lazima kuelewa kwamba kirusi aina ya Trojan kimeambatana na kirusi aina ya root kit ambacho ni kigumu kukiondoa katika kompyuta, hivyo kusababisha mtumiaji kufuta mpangilio na kuhifadhi upya. Hata hivyo makampuni ya usalama wa mipangilio ya kompyuta ambayo ni Norton, Kaspersky, Trend Micro, Microsoft, McAfee na wengine, husaidia kukiondoa kirusi aina rootkit bila kufuta mipangilio ya kompyuta yako. Kifaa hicho cha kutengeza virusi DNS Changer kimekuwa katika habari tangu Novemba 8, 2011, wakati botnet kubwa ya kusambaza virusi chini ya jina la kampuni ya Rove Digital, iliwekwa chini ya ulinzi na muungano wa msako ambao ni FBI pamoja na kundi la Kiestoni wahalifu. Na kutokea kukamatwa kwa wanaume sita. HABARI TOKA http://cheraboy.blogspot.com
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

Sunday, June 3, 2012

BIRTHDAY YA BONIFACE MASELE "BONTA THE GREAT"


BONTA THE GREAT
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

HISTORIA FUPI YA MAREHEMU (DAUDI KILUNGUMIKA LUFEGA) ALIYEKUWA MWENYEKITI WA MTAA WA BANK WILAYANI MAGU KUPITIA CHAMA CHA WANANCHI (CUF)


HISTORIA FUPI YA MAREHEMU DAUDI KILUNGUMIKA LUFEGA KUZALIWA Marehemu alizaliwa mnamo mwaka 1960 akiwa ni Mtoto wa Saba katika familia ya Mzee Lufega Masalu, Alizaliwa katika Kitongoji cha Benki eneo ambalo kwa sasa Cadirac Hotel. Katika Wilaya ya magu na Ndani ya Mkoa wa Mwanza. ELIMU Daud Kilungumika Lufega alipata Elimu yake ya msingi Katika Shule ya Msingi Nyalikungu mwaka 1972 na kuhitimu darasa la saba mwaka 1978. 1980 Alijiunga na Chuo cha Kilimo na Mifugo Ukiligulu Mwanza na kutunukiwa cheti cha Afisa Usimamizi Kilimo na Mifugo. UBATIZO: Daudi Kilungumika Lufega alikuwa ni Muumini wa Kanisa katoliki. Mwaka 1993 alibatizwa katika Parokia ya Magu. Mwaka 1993 alipata kipaimara katika Parokia ya Magu. NDOA Mwaka 1985 alimwoa Bi. Fausta Mayengela. KAZI/SHUGHULI Mwaka 1981 -1984 Afisa Mazao wa Mamlaka ya Pamba –Tanzania Kanda ya Manawa Ginnery. 1984-1994- Afisa Ukusanyaji mapato(Revenue Collector) HALMASHAURI YA Wilaya ya Magu. UONGOZI NA UZOEFU: Mwaka 1999-2009 Balozi wa nyumba kumi na Mwenyekiti wa Kitongoji cha Benki. Kwa Tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mwaka 2009-2012 Mwenyekiti wa Mtaa wa Benki katika Mamlaka ya Mji Mdogo wa Magu Mjini Kwa tiketi ya Chama Cha Wananchi –CUF. Mwaka 2010-2012 Kada wa Chama na Mjumbe wa kamati ya Utendaji Wilaya –CUF. UGONJWA na MAUTI Daudi Kilungumika Lufega alianza kuugua Mwezi Marchi 2012 akisumbuliwa na matatizo ya Inni na Figo, Alibahatika kupata Matibabu katika Hospital ya Wilaya ya Magu pia alifakiwa kupata matibabu ya Tiba mbadala 1. Lakini kwa vile Andiko linasema “Kila nafsi itaonja mauti” 2. Na Kwa kuwa Mauti ni kitanda ambacho kila Mwanadamu atakilalia. 3. Mauti ni Mlango ambao kila Mwanadamu atauingia. 4. Mauti ni vazi ambalo kila Mwanadamu atalivaa. Na Tarehe 31-05-2012 Majira ya saa 12:30 asubuhi Daudi Kilungumika Lufega alifariki Dunia. Marehemu ameacha 1. Mjane 2. Watoto 9 wakiume 4 na Wakike (5)Watano, na 3. Wajukuu 4 SHUKRANI: Familia ya Marehemu inatoa Shukrani zake za dhati kwa Waganga na Wauguzi wote wa Hospital ya Wilaya ya Magu kwa juhudi zao kumhudumia Marehemu kipindi alipokuwa amelazwa Hospitalini hapo. Wataalam wa Tiba mbadala kwa Jitihada zao zote za Kutaka kuokoa Maisha yake japo haikuwezekana. Shukrani kwa Majirani, Ndugu, Jamaa, Marafiki, Vyama vya Siasa, Mamlaka ya Mji Mdogo Magu Mjini na wote walioshiriki kwa namna moja ama nyingine katika hali na Mali kufanikisha Mazishi na Maziko ya marehemu Mpendwa wetu. Marehemu alikuwa Mtu wa Watu, Mcheshi, Mtu huru na mtu mwenye maamuzi ya kweli. BWANA AMETOA, BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE, AMINA.
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.